Kwa nini tumefika hapa? Miaka hamsini ya uhuru bado mipaka ya nchi hii ina utata! Kweli Watanzania tunahitaji maelezo toshelevu.Kwa bahati mbaya kama Wamalawi wameshaona dalili za uhakika za uwepo wa mafuta mzozo huu utakuwa mgumu zaidi kutatua.Lakini ninaamini pia Wamalawi wanatujua vizuri sana jinsi tulivya serious katika kulinda mipaka yetu, kama wamesahau wajikumbushe yaliyompata Idd Amin.Wakituchezea tutafika hapo Lilongwe na Blantire kuwasabahi na huyo dada Joyce hatakuwa tena rais.
Kwenye maelezo yako hakuna ufafanuzi wowote , bora hata thread za watu wengine humu ndani zina maelezo ya kutosha.
Kama Waziri ndivyo alivyoeleza hivyo, basi hilo ziwa litachukuliwa na Wamalawi, na itabidi tubadili vitabu vyetu vya Jiografia haraka!
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ulinzi, usalama na Mambo ya Nje inatoa maoni yake sasa. Inahangaika zaidi na utendaji wa Membe ingawa haimtaji kwa jina. Imeponda mambo mengi utadhani maoni haya yameandikwa na kambi rasmi ya upinzani!
Nimelisikiliza tamko la waziri inaonekana kama tuliwaachia sana Malawi wafanye watakalo baada ya kelele nyingi serekali inakuja na tamko la kututia upofu waTanzania kwamba serekali iko makini na inajua kichoendelea wakati kila mmoja wetu anajua imewachukua wiki nzima kuandaa tamko !!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Mh. Membe tumekusikia tena umechelewa, hii kauli ingetoka wiki iliyopita. Laiti kama angeitoa AMIRIJESHI MKUU mwenyewe vijana tukaanza kupiga jaramba.
Ameyasemea ofisini au kwenye eneo la tukio.
Na wka kuongezea, wakati wa kutoa matamko , kwa suala hili, ulishapita. sasa kinachotakiwa ni vitendo. Hivi kama hayo makampuni yakigoma kuacha hizo shughuli zao, Membe ameonyesha ni jinsi gani tutakabiliana nayo?Nimelisikiliza tamko la waziri inaonekana kama tuliwaachia sana Malawi wafanye watakalo baada ya kelele nyingi serekali inakuja na tamko la kututia upofu waTanzania kwamba serekali iko makini na inajua kichoendelea wakati kila mmoja wetu anajua imewachukua wiki nzima kuandaa tamko !!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Usipende kukurupuka mbona Membe kaeleweka vizuri wewe unataka serikali ifuate mawazo yenu nyie Pro-Chadema msioitakia mema nchi yetu.
Wewe kwa akili yako unataka JWTZ waanze vita ili suala linaitaji mazungumzo mpaka hatua ya vita kufikia mpaka mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice-ICJ) washindwe.
Malawi wanapoteza muda wanaleta usumbufu tu mkutano wa mwaka 1884 uliofanyika Berlin lazima kila nchi iheshimu mipaka iliyowekwa na wakoloni.
Mh. Membe tumekusikia tena umechelewa, hii kauli ingetoka wiki iliyopita. Laiti kama angeitoa AMIRIJESHI MKUU mwenyewe vijana tukaanza kupiga jaramba.
Ah! Ina maana tuliwagwaya Makaburu! Na baada ya Kaburu kuondolewa serikali ilifanya nini. Jamani "Chelewa chelewa............"
inaonekana unapenda vita. Tanzania isingetoa tamko wakati mazunguzo yako mezani.
1. Mwalimu Nyerere na Kamuzu banda walikuwa paka na panya wasingeweza kukaa meza moja lakini kila mtu aliamua kulitumia ziwa baada ya kuona hakuna uwezekana na kuzungumza. Nyerere na Banda walikuwa wana ugomvi katika mambo matatu, mosi, mpaka wa ziwa nyasa, Kamuzu Banda (malawi) kuwa na uhusiano wa kibalozi na utawala wa kibaguzi wa Afrika kusini na Banda alimtuhumu Nyerere kwamba anawatumia wakimbizi wa Malawi waliokimbilia Tanzania kutaka kumpindua.
2. Mkapa na Muluzi ndio walioamsha upya mazungumzo baada ya kuonekana kwamba Bakili Muluzi anayo nia ya dhati ya kuzungumza. hadi Muluzi anaondoka madarakani mazungumzo yalikuwa hajaisha.
3. Kikwete ambaye pia alikuwa ni waziri wa mambo ya nje wakati huo alishiriki sana katika mazungumzo hayo na akajaribu kuyaendeleza lakini Rais mpya wa malawi Marehemu Bingu wa Mutahalika alikuwa hatoi ushirikiano wa kutosha kuna tetesi kwamba alikuwa muumini wa wanaoamini kwamba Ziwa Nyasa ni la Malawi.
4. Rais Joyce banda amekuwa madarakani kwa muda mfupi bado haijafahamika msimamo wake kwani makampuni ya kutafuta mafuta (Ya Uingereza) yaliyoko ziwa Nyasa yana chimbuko lake katika utawala wa Mutharika. hata hivyo, wanaojua msimamo wa huyu mama wanasema na yeye ni muumini wa wanaodai ziwa lote ni la Malawi.
Hivyo kauli ya Membe ni sawa kutoka sasa.