Mh. Membe atoa kauli nzito Bungeni kuhusu Malawi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Membe atoa kauli nzito Bungeni kuhusu Malawi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaKiiza, Aug 6, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Waziri Benard Membe ameweka wazi kuhusu mpaka wa Tanzania na kubainisha kuwa mpaka unapita katikati ya ziwa Nyasa!

  Na amebainisha kuwa mipaka hiyo iliwekwa kwakipindi hicho nyasa ikiitwa Nyasaland nahivyo wamalawi wamekuwa wakijua Nyasa ni yao na Tanzania inaishia pwani ya ziwa Nyasa!

  Na amesema tatizo ni la mda mrefu tangu miaka ya 1960... Na hili tatizo lilishindikana kutatuliwa kwakuwa Kiongozi wa Malawi Kamuzu Banda Kuwa na urafiki na makaburu.. Hivyo Tanzania kwakuwa ilikuwa inaendesha harakati za ukombozi mwa afrika kusini hivyo haikuwa rahisi kwa Tanzania kukaa kitikimoja na Malawi kwakuwa Malawi iliwakumbatia Makaburu.

  UPDATE:
  Serikali imetoa tamko rasimi kuanzia sasa kuondoka,kuanzia sasa na serikali haitaruhusu utafiti huu kuendele mpaka makubaliano yatakapokuwamepatiwa muafaka....Na serikali iko tayari kulinda mipaka kwa gharama yoyote ile na imeitahadharisha serikali ya malawi kuondoka mara moja na kusitisha shughuli zozote zile za utafiti ndani ya Ziwa Nyasa.

   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Amewataka Malawi kushehimu mazungumzo ya tarehe 27/12 na katika kipindi hiki, wasiruhusu mtu au kampuni au kikundi kufanya shughuli zozote kama za kutafuta mafuta na gesi.

  Hapa tunazungumzia mustakabali wa watu takribani 600 wanaotegemea ziwa kwa maisha yao

  Serikali imeyaonya makumpuni yote yanayofanya utafiti kwen ziwa nyasa eneo linalobishaniwa kuacha MARA MOJA. Serikali haitaruhusu utafiti kuendelea hadi makubaliano kuhusu mpaka yatakapopatikana

  Wananchi waendelee na shughuli zaoziwani na nchi kavu. Serikali ipo tayari kulinda mipaka ya nchi yetu kwa gharama yoyote .
   
 3. T

  Twigwe Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na kawaonya watafiti wote kutoendelea na utafiti wowote ndani ya ziwa,hivyo wasimame kabisa!!
   
 4. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  ametangaza vita rasmi...kama wakiendelea tutailinda mipaka kwa ghalama yeyote ile....
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwenye maelezo yako hakuna ufafanuzi wowote , bora hata thread za watu wengine humu ndani zina maelezo ya kutosha.
  Kama Waziri ndivyo alivyoeleza hivyo, basi hilo ziwa litachukuliwa na Wamalawi, na itabidi tubadili vitabu vyetu vya Jiografia haraka!
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mh. Membe tumekusikia tena umechelewa, hii kauli ingetoka wiki iliyopita. Laiti kama angeitoa AMIRIJESHI MKUU mwenyewe vijana tukaanza kupiga jaramba.
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Na ameonya tena watafiti hao wasisogee kabisa kuanzia leo jumatatu 06/08/2012 na wale wavuvi na wakulima waendelee na shughuli zao kama kawaida.

  Kwa hapo naikubali hii serikali SIKIVU kwa kusubiri siku muafaka waurekebishe mpaka huo km ule wa Chad, Seychelles na mingineyo.

  Ngoma ni lile PASU la chenji ya Chenge kwa nini Serikali imechukua fedha zote na zile zilizogawiwa ktk a/c ya New Jeasey hatuzioni HEBU MLIOKO MJENGONI ULIZENI SWALI HILO tupo huku nje kuwapigia like au makofi
   
 8. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Mh. Membe ametamka wazi. Na yeye ndiye mtu hasa kauli yake tumekuwa tukiisubiria. Ni tamko ambalo liko clear.
   
 9. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Tutaamini vipi kwamba serikali inailinda mipaka yetu kwa gharama yoyote ile wakati tunaushahidi kwamba ndege ya Jeshi la Qatar ilingia kwenye anga yetu, na kutua kwenye ardhi yetu, na kuchukua rasilimali zetu ambazo hazipaswi kuchukuliwa na kuondoka zake na mpaka leo hatujasikia kauli ya ukali kutoka kwa kiongozi yoyote yule wa serikali?

  Au, Mbona hatusikii kauli za ukali dhidi ya wazungu wanaoingiza ndege zao kwenye anga letu, na kutua kwenye ardhi yetu na kupakia michanga yenye madini yetu na kuondoka bila taasisi za serikali yetu zilizokasimiwa madaraka ya kusimamia uchimabaji wa madini yetu kuwa na taarifa yoyote ile?

  Au haya hayaonekani kuhatarisha amani na utulivu wetu? au haya sio matendo yenye ishara ya dharau dhidi Nchi yetu? au hii sio kuingilia mipaka yetu?

  Au serikali yetu iko wapi kuilinda mipaka ya nchi yetu dhidi ya watu wanaoingiza madawa ya kulevya ambayo yanatishia yanasababisha uharibu mkubwa sana kwa nguvu kazi ya nchi yetu, na kuvuruga mira na desturi za maisha baina yetu?

  Mpaka pale ntakapopata majibu ya maswali haya ndio nafsi yangu itakaporidhia serikali kutumia mapato yangu kwenda vitani dhidi ya malawi, sababu mimi mwenyewe siko tayari kushiriki vita hiyo.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  katamka wapi akimueleza nani???? leteni habari yote mbona mnabania taarifa muhimu kama hii???
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nimelisikiliza tamko la waziri inaonekana kama tuliwaachia sana Malawi wafanye watakalo baada ya kelele nyingi serekali inakuja na tamko la kututia upofu waTanzania kwamba serekali iko makini na inajua kichoendelea wakati kila mmoja wetu anajua imewachukua wiki nzima kuandaa tamko !!!!!!!!!!!!!!!!!!.
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  tangu jana wanajeshi wa Tanzania wanaelekea huko mpakani...
   
 13. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Mkuu alikuwa anawasilisha makadirio ya Wizara yake ya M/Nje na ushirikiano wa kimataifa!!Najua tuko wote mkuu!
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280

  bungeni
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Nani kasema ukiibiwa vitu ndani ya nyumba yako na majambazi unasusa na kuacha kununua chochote nyumbani kwako???

  makosa au kasoro zinazilalamikiwa kuwa serikali haijalinda vya kutosha raslimali zetu sio msingi wa kususa ziwa Nyasa na kwaachia wamalawi ni wendawazimu.
   
 16. Pangaea

  Pangaea JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa nini tumefika hapa? Miaka hamsini ya uhuru bado mipaka ya nchi hii ina utata! Kweli Watanzania tunahitaji maelezo toshelevu.Kwa bahati mbaya kama Wamalawi wameshaona dalili za uhakika za uwepo wa mafuta mzozo huu utakuwa mgumu zaidi kutatua.Lakini ninaamini pia Wamalawi wanatujua vizuri sana jinsi tulivya serious katika kulinda mipaka yetu, kama wamesahau wajikumbushe yaliyompata Idd Amin.Wakituchezea tutafika hapo Lilongwe na Blantire kuwasabahi na huyo dada Joyce hatakuwa tena rais.
   
 17. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,076
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo waziri anaweza kutoa tamka ila rais ndiye anaamrisha kazi kuanza!

  Haya Mzee Abdulaman Shimbo, tunakusubiri uwashikishe Wamalawi hawa adabu
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ulinzi, usalama na Mambo ya Nje inatoa maoni yake sasa. Inahangaika zaidi na utendaji wa Membe ingawa haimtaji kwa jina. Imeponda mambo mengi utadhani maoni haya yameandikwa na kambi rasmi ya upinzani!
   
 19. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Waziri Membe asiishie kutoa matamko tu bali wananchi tunataka kuona mipaka yetu iklilindwa.
  Tunalo jeshi la wananchi ambalo linalipwa vizuri sana na lenye mafunzo ya hali ya juu, kwahiyo hatukutarajia hata kusikia kwamba malawi wamethubutu kuvuka mpaka na kuingia eneo letu.
  Bila kuhakikisha kwamba kuna doria/ulinzi wa kueleweka katika ziwa nyassa, hao wamalawi watendelea kufanya utafiti ndani ya ziwa na kujiwekea mazingira ya uhalali wa kulimiliki ziwa lote.
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Good show!!!!

  Uchokozi wa Malawi nauona katika jambo moja tu hata kama ziwa Nyasa ni la kwao na sisi tunasema hapana tuna sehemu yetu ...... Hawana budu kuwa waungwana kumaliza mgogoro mezani hata ikibidi kuitumia jumuia ya kimataifa kuliko kupuuza mazungumzo na kuendeleza miradi ndani ya ziwa.............. Hizi ni dharau hata kwa Rais mnayemuita ni dhaifu hawezi kuvumilia ubinafasi huu.

  kama kweli malawi wana ushahidi kwa kutosha kwa nini hawakimbilii kusuluhishwa na jirani yao (Tanzania) wao wanakimbilia kuingiza makampuni ya utafiti wa mafuta ziwani?
   
Loading...