Mh. Membe atoa kauli nzito Bungeni kuhusu Malawi!

Kama mnajua kulinda mipaka ya nchi hii kweli kweli, tunaomba mtuhakikishie kwamba mko tayari na kwa gharama yoyote ile kuhakikisha kwamba Muungano wa Tanzania Bara, Tanganyika or what ever na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hautavunjika na mtoe tamko kali kwa wale wanaotishia kuvuruga mipaka ya Jamhuri yetu. Kama hamuwezi hili, siko tayari mimi binafsi, mke wangu wala watoto wangu si tu kuchangia, bali hata kumtia moyo wala kumshawishi mtu yoyote yule kushiriki vita ya aina yoyote ile dhidi ya Malawi.

Mkuu suala hili ni la kitaifa sio suala la kumfuraisha mtu serikali hawafanyi kazi kwa kuifurahisha familia yako.
 
Mkuu suala hili ni la kitaifa sio suala la kumfuraisha mtu serikali hawafanyi kazi kwa kuifurahisha familia yako.

Hakuna mantiki yoyote ya utaifa mnayoisimamia zaidi ya kututupia zigo lingine la kutuweka busy. wala utaifa hauonekani wakati wa vita tu. sana sana mnachokionyesha ni kunogowa na mauaji baada ya kuanza kuua raia wenu wenyewe
 
Naomba isitokee vita kama ya Kagera tukarudi kule kule kufulia nguo kwa majani ya mipapai. Tuliokuwepo baada ya kumalizika vita vya Idd amini tuliteseka sana na wengi wetu tulidumaa kwa kukosa lishe stahiki kutokana na mporomoko mkubwa wa uchumi haswa tuliokuwa tunaishi vijijini enzi hizo.
 
Hawa wamalawi wahuni sana,sasa kama ziwa nyasa lote ni lao mbona kile kipande kilichoingia Mozambique hawaking'ang'anii?Hizi ndiyo athari za ushoga wanaouendekeza,Na Hilary Clinton yupo alikuwepo huko kuwaunga mkono na mwitikio wao juu ya ushoga!
 
Nyoka wa Mdimu...sasa nipo huru kabisa na ninajiamini kuwa Ziwa Nyasa ni 50/50. Sasa nasubiria kuona Mama wa Upande wa pili itakuwaje? Atatumia njia gani kumlainisha dhaifu....atampa rushwa ya ********, liwalo na liwe ..... tuje baadaye tuambiwe mpaka ni ufukweni!
 
Ukiangalia military rank kati ya Malawi na Tanzania kwa mwaka 2012,kadri ya CIA report Malawi ni ya 112 na Tanzania ni ya 169!!
 
kwa hiyo waziri anaweza kutoa tamka ila rais ndiye anaamrisha kazi kuanza!

Haya Mzee Abdulaman Shimbo, tunakusubiri uwashikishe Wamalawi hawa adabu
.......Mzee yupo kwenye mfungo mtakatifu, ngoja kwanza idd ipite atawashughulikia tu, kwani ana haraka gani mbona wameshafanya utafiti wamebaki kuaza kuchimba tu?
 
Naomba isitokee vita kama ya Kagera tukarudi kule kule kufulia nguo kwa majani ya mipapai. Tuliokuwepo baada ya kumalizika vita vya Idd amini tuliteseka sana na wengi wetu tulidumaa kwa kukosa lishe stahiki kutokana na mporomoko mkubwa wa uchumi haswa tuliokuwa tunaishi vijijini enzi hizo.
Lakini TANZANIA ikabaki na mipaka yake ileile. Watoto hawakukalia mawe au kukaa sakafu ya vumbi kwenye madarasa mabovu kama ilivyo sasa. Madawa kwenye zahanati na hospitali zetu yalikuwepo. Mali na rasilmali za nchi yetu zilibaki salama.
Tukipigana vita sasa hivi, vita hiyo itatugharimu sana. Sio siri kwamba mafisadi nao watanufaika sana na vita hii maana wapo hadi ndani ya majeshi yetu na vyombo vingine vya usalama. Tuombe vita isiwepo sio tu na Malawi bali na nchi nyingine yoyote.
 
Tumetenga dola bilioni ngapi kwa ajili ya vita?what will be our exit plan?siyo tuanze kulia njaa baada ya wiki 2,begginning a military campaign is not like going to a picnic,tuko tayari kukatwa salary zetu by half ili kuwezesha jeshi?Kenya waliingia Somalia wakaanza kulia njaa baada ya wiki chache
 
Mi naona Malawi i-claim possesion ya the whole Tanzania,
tubadilishe jina la nchi,
iitwe Malawi.
maybe nchi itamove
 
ha ha haaaaa! kati ya vitu ambavyo sasa hivi vinanifirahisha ni huu mgogoro hasa nikisoma post za watanzania na comment zake na post za wamalawi na comment zake nacheka sana,

MMALAWI:

96b4ca3300d43eb8494130c9c58e49dd
To hell with these so called Tanzanians.If they dont understand that Anglo-treaty let them understand the language of WAR.
Like
1_14_up.png
0
Reply

MTANZANIA:

da466c9778e518fa564f2734b130d521
your very stupid malawian you thinks you can own all the lake in one country and others not shame on stupid fool why that lake in other part is dived equaly by mozambiq the tanzanian they will kick ur as..
Like
1_14_up.png
0
Reply

hizo tambo na matusi zinanifanya nicheke sana bila na mi kuwa na comment zangu
 
Tutaamini vipi kwamba serikali inailinda mipaka yetu kwa gharama yoyote ile wakati tunaushahidi kwamba ndege ya Jeshi la Qatar ilingia kwenye anga yetu, na kutua kwenye ardhi yetu, na kuchukua rasilimali zetu ambazo hazipaswi kuchukuliwa na kuondoka zake na mpaka leo hatujasikia kauli ya ukali kutoka kwa kiongozi yoyote yule wa serikali?

Au, Mbona hatusikii kauli za ukali dhidi ya wazungu wanaoingiza ndege zao kwenye anga letu, na kutua kwenye ardhi yetu na kupakia michanga yenye madini yetu na kuondoka bila taasisi za serikali yetu zilizokasimiwa madaraka ya kusimamia uchimabaji wa madini yetu kuwa na taarifa yoyote ile?

Au haya hayaonekani kuhatarisha amani na utulivu wetu? au haya sio matendo yenye ishara ya dharau dhidi Nchi yetu? au hii sio kuingilia mipaka yetu?

Au serikali yetu iko wapi kuilinda mipaka ya nchi yetu dhidi ya watu wanaoingiza madawa ya kulevya ambayo yanatishia yanasababisha uharibu mkubwa sana kwa nguvu kazi ya nchi yetu, na kuvuruga mira na desturi za maisha baina yetu?

Mpaka pale ntakapopata majibu ya maswali haya ndio nafsi yangu itakaporidhia serikali kutumia mapato yangu kwenda vitani dhidi ya malawi, sababu mimi mwenyewe siko tayari kushiriki vita hiyo.

Kwa hoja mbofumbofu hivi punde utauliza inawezekanaje kuilinda mipaka yetu wakati vibaka pale Kwa-Mtogole wanaendelea kukwapua sim za watu? Ule wizi wa wanyama si uvamizi wa mipaka. Ni kazi iliyofanywa na serikali kwa makusudi. Ambaye hakujua ni wewe na mimi lakini wahusika wakuu katika tasnia hiyo walikuwa wanajua fika nini kinaendelea! Ukijitweza mwenyewe hakuna atakaekuinua!
 
Ukiangalia military rank kati ya Malawi na Tanzania kwa mwaka 2012,kadri ya CIA report Malawi ni ya 112 na Tanzania ni ya 169!!

Siyo kweli mkuu,unachosema wewe ni matumizi ya fedha yanayotengwa kwaajili ya jeshi kulingana na bajeti yote ya nchi husika!!
 
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ulinzi, usalama na Mambo ya Nje inatoa maoni yake sasa. Inahangaika zaidi na utendaji wa Membe ingawa haimtaji kwa jina. Imeponda mambo mengi utadhani maoni haya yameandikwa na kambi rasmi ya upinzani!
.......mwenyekiti wa kamati ameshaoteshwa tayari, anamsubiri Membe aoteshwe, sasa atamrembea nn
 
sisi vijaaaaaaaaaanaaaa,vijanaaa vijana tayariiiii

kulitumikiaaaaaaaaaa

taifaaa taifaaa taifaaa

kulitumikiaaaaa taifaaa taifaaa tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Tumetenga dola bilioni ngapi kwa ajili ya vita?what will be our exit plan?siyo tuanze kulia njaa baada ya wiki 2,begginning a military campaign is not like going to a picnic,tuko tayari kukatwa salary zetu by half ili kuwezesha jeshi?Kenya waliingia Somalia wakaanza kulia njaa baada ya wiki chache
Wengine wanadhani VITA ni lelemama tena kwenye mazingira ya kifisadi kama tulimo sasa. Tunayo vita kali humu ndani ambayo inaelekea kutushinda kabisa.
 
nia tunayo,sababu tunayo,uwezo tunao wa kuilinda mipaka ya tanzania na watu wake.

hatupo tayari kuchomwa chomwa jicho halafu tuendelee kumchekea adui.nasema hatuko tayari hata kidogo.malawi acheni chokochoko nawaambia.
 
sisi vijaaaaaaaaaanaaaa,vijanaaa vijana tayariiiii

kulitumikiaaaaaaaaaa

taifaaa taifaaa taifaaa

kulitumikiaaaaa taifaaa taifaaa tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

ha ha ha ha ha
 
Back
Top Bottom