Mh. Membe atoa kauli nzito Bungeni kuhusu Malawi!

Minaskia tu wanajeshi wameelekea uko. Leteni picha tuone basi kama kweli!
 
unataka serikali ifuate mawazo yenu nyie Pro-Chadema msioitakia mema nchi yetu. .
acha kuleta maswala ya vyama hapa,Chuki zako na chadema ziishie hukohuko,hili ni swala la kitaifa na linawahusu Watanzania wote bila kujali dini,kabila wala itikadi zao,hivyo ujaribu kutumia akili wakati mwingine
 
Hakuna haja ya kupiga Jaramba kwa sababu ya hisia, swala la kwamba Ziwa Nyasa kuna mafuta ndio linalowatoa viongozi wetu mapovu, kama kweli viongozi wetu wako makini katika kuhakikisha interest za Tanzania hazichezewi, waanze kutuonyesha kwa vitendo kwa kuhakikisha kwamba tunapata a reasonable share kwenye mapato ya madini, waanze kutuonyesha kwa vitendo kwamba viongozi wazembe, wala rushwa na mafisadi wanachukuliwa hatua.

Watanzania tusiwe tayari kutengenezewa maadui wengine wakati serikali hii hii imeshindwa kudhibiti Maralia kwenye makazi yetu badala yake inasubiri misaada kutoka nje.

Kama unataka kupiga Jaramba, anza kupiga Jaramba sasa kama meseji kwa CCM kwamba comes 2015 wasipokuwa tayari kuachia madaraka kwa mujibu wa matakwa ya UMA wa Tanzania basi wajiandae kwa lolote.

Acheni kusumbuana na Poor Malawi, kwanza wanamatatizo yao mengi tu ndio maana wao kupewa hadithi ya mafuta wameona kama vile uchimbaji umeanza. sisi hatuhitaji exploration, it is confirmed kwamba dhahabu, uranium,Tanzanite, Diamond etc zimejaa chini ya ardhi yetu. Kama vipi tupige Jaramba kuyalinda haya kwanza.

Mkuu yaelekea CCM imekukaa sana akilini, huwezi fanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya taifa bila kuitaja CCM.

CCM imekumaliza akili hadi huna fikra mpya....... huna wazo jipya ama kweli CHADEMA ina watu. Mnaleta mambo ya Simba na yanga kwenye mpaka wa nchi.?????
 
Usipende kukurupuka mbona Membe kaeleweka vizuri wewe unataka serikali ifuate mawazo yenu nyie Pro-Chadema msioitakia mema nchi yetu.

Wewe kwa akili yako unataka JWTZ waanze vita ili suala linaitaji mazungumzo mpaka hatua ya vita kufikia mpaka mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice-ICJ) washindwe.

Malawi wanapoteza muda wanaleta usumbufu tu mkutano wa mwaka 1884 uliofanyika Berlin lazima kila nchi iheshimu mipaka iliyowekwa na wakoloni.

Kama mnajua kulinda mipaka ya nchi hii kweli kweli, tunaomba mtuhakikishie kwamba mko tayari na kwa gharama yoyote ile kuhakikisha kwamba Muungano wa Tanzania Bara, Tanganyika or what ever na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hautavunjika na mtoe tamko kali kwa wale wanaotishia kuvuruga mipaka ya Jamhuri yetu. Kama hamuwezi hili, siko tayari mimi binafsi, mke wangu wala watoto wangu si tu kuchangia, bali hata kumtia moyo wala kumshawishi mtu yoyote yule kushiriki vita ya aina yoyote ile dhidi ya Malawi.
 
Hapa ndo tunaona na kushudia ukiukwaji wa sheria za kimataifa na upofu wa viongozi waew wa Tanzania au Malawi. Naona wachangiaji wengi mnapenda zipigwe lakini hayo yote yana negative impacts kwa nchi hizi mbili. Je Tanzania ikitokea ikadeclare vita dhidi ya Malawi wakati Malawi haijafanya hivyo hamuoni kuwa Tanzania itabeba lawama kati damage,destruction and injuries to the people of Malawi? Na ili ni swala linalo katazwa kwamjibu wa sheria za kimataifa.
Ushauri wangu kama mtanzania nadhani ingekuwa vizuri Tanzania kuishitaki kwa Malawi kama wamekataa dialogue na sisi watanzania.Tunaweza kuepuka ugonvi huu kwa kuitumia vizuri African Union au United Nations au SADC.

well said.

Mzalendo wa kweli wakati wote hapendi vita.
 
Kwa nini tumefika hapa? Miaka hamsini ya uhuru bado mipaka ya nchi hii ina utata! Kweli Watanzania tunahitaji maelezo toshelevu.Kwa bahati mbaya kama Wamalawi wameshaona dalili za uhakika za uwepo wa mafuta mzozo huu utakuwa mgumu zaidi kutatua.Lakini ninaamini pia Wamalawi wanatujua vizuri sana jinsi tulivya serious katika kulinda mipaka yetu, kama wamesahau wajikumbushe yaliyompata Idd Amin.Wakituchezea tutafika hapo Lilongwe na Blantire kuwasabahi na huyo dada Joyce hatakuwa tena rais.
Kuipiga Malawi hakuna hata kuiambia dunia kuwa tuna vita na wamalawi.
 
MAMA POROJO sipendi vita ila inaonekana serekali yetu imekuwa na uvumilivu wa kupitiliza inakuwaje ndege zinaruka katika anga la Tanzania zaidi ya mara tano tunaziachia zimefika hadi kutua pwani ya ziwa Nyasa bado tunaangalia ?.Kwanini tusitungue walau ndege moja kuonyesha tuko serious hatuna masikhara linapokuja suala la mipaka ya nchi yetu.Unadhani Malawi wakigundua mafuta au gesi watataka tena mazungumzo Mama POROJO ungekuwa mke wangu pengine ungeeelwa namaanisha nini nakwambia akitokea kidume akakukonyeza vita vinaanzia hapo hapo hakuna cha mazungumzo wala mahakama na suala la ziwa Nyasa nisingekuwa na mazunguzo na malawi kitendo cha kuvuka mpaka kingekuwa sababu tosha ya kuwafunza adabu.

Mkuu Ngongo haya majibu ya MAMA POROJO hayatofautiani na maelezo ya waziri membe.
Na ukiangalia namna serikali yetu inavyolishughulikia swala hili la mpaka wetu na malawi unagundua kwamba wamalawi wametambua udhaifu wa raisi wetu, udhaifu wa amiri jeshi mkuu wetu, pia wametambua udhaifu wa mwenyekiti wa chama tawala ccm.
 
Mkuu yaelekea CCM imekukaa sana akilini, huwezi fanya jambo lolote la maana kwa maslahi ya taifa bila kuitaja CCM.

CCM imekumaliza akili hadi huna fikra mpya....... huna wazo jipya ama kweli CHADEMA ina watu. Mnaleta mambo ya Simba na yanga kwenye mpaka wa nchi.?????
wewe ndio unafikra Mgando, na Inaonekana wewe ndio CHADEMA inakuwewesesha.
Mimi natoa msimamo binafsi, kama unataka kujua msimamo wa CHADEMA kamuulize John John Mnyika, achilia mbali kwamba sina mahusiano ya aina yoyote ile na CHADEMA.

Kama umeguswa na maoni yangu jielekeze moja kwa moja kukabiliana nayo, haitokusaidia kitu kuanza kuyaclassify kama ni ya kisiasa au si ya kizalendo.

Naomba niongezee kwamba, Akili zangu zinanituma kujipanua na kuyafurahia maisha popote pale duniani, ilimradi Mwenyezi Mungu ameweka mazingira stahiki kwa mimi kuwepo apo bila kuhatarisha uhai wangu. sifungwi na mipaka wala fikra zozote za kibinaadamu, na siko tayari kurudishwa nyuma na kufikia state ya ubinafsi kama ile iliyowajaa wote wanaoshabikia ulinzi wa mipaka na mapigano dhidi ya Majirani au binaadamu wengi wengine kokote pale walipo.

Tumeshindwa kushughulikia matatizo yetu ya msingi tumebaki kuwa kama ng'ombe kipofu, tunapapasa papasa hovyo ili tupate kitu cha kutuweka bize.
 
Hapa ndo tunaona na kushudia ukiukwaji wa sheria za kimataifa na upofu wa viongozi waew wa Tanzania au Malawi. Naona wachangiaji wengi mnapenda zipigwe lakini hayo yote yana negative impacts kwa nchi hizi mbili. Je Tanzania ikitokea ikadeclare vita dhidi ya Malawi wakati Malawi haijafanya hivyo hamuoni kuwa Tanzania itabeba lawama kati damage,destruction and injuries to the people of Malawi? Na ili ni swala linalo katazwa kwamjibu wa sheria za kimataifa.
Ushauri wangu kama mtanzania nadhani ingekuwa vizuri Tanzania kuishitaki kwa Malawi kama wamekataa dialogue na sisi watanzania.Tunaweza kuepuka ugonvi huu kwa kuitumia vizuri African Union au United Nations au SADC.

Kinachotakiwa hapa na ambacho watu wengi wanakipigia debe ni jeshi letu la JWTZ kulinda mipaka yetu. Kwakuwa malawi wameweza kuthubutu kuingia ndani ya mipaka yetu, hatua ya kwanza ambayo haingehitaji muda wa kuitafakari ilikuwa ni kuhakikisha kwamba si watafiti wa mafuta na gesi ama wanajeshi wa malawi ama ndege yao inayoingia ndani ya mipaka yetu.

Hilo la kutangaza vita halipo na hatuwezi kuishaurti serikali kutangaza vita, tunachoihimiza hapa ni kulinda mipaka yetu. Ukiweza kuiona hiyo toafauti basi utakuwa umeelwa msimamo wa wengi wetu katika hili.
 
Haka kanchi ni kabaya kwa mambo ya kiuchumi lakini siyo kwenye mambo kugombea mipaka. Kama wamalawi hawakajui, basi waendelee na chokochoko zao. Watafumuliwa na mama yao atakimbilia Afrika Kusini awaache wanalia peke yao.
 
Usipende kukurupuka mbona Membe kaeleweka vizuri wewe unataka serikali ifuate mawazo yenu nyie Pro-Chadema msioitakia mema nchi yetu.

Wewe kwa akili yako unataka JWTZ waanze vita ili suala linaitaji mazungumzo mpaka hatua ya vita kufikia mpaka mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice-ICJ) washindwe.

Malawi wanapoteza muda wanaleta usumbufu tu mkutano wa mwaka 1884 uliofanyika Berlin lazima kila nchi iheshimu mipaka iliyowekwa na wakoloni.

Kutoelewa kwake usihusishe na Pro CDM mkuu,ni yeye kama yeye. Hata hivo mipaka iliyoiwekwa na wakoloni c ndo hiyo inaonyesha ziwa lote lao?kwamba mpaka unapita kwenye shore ya lake Nyasa far east? au nieleweshwe vzuri hapa
 
tangu jana wanajeshi wa tanzania wanaelekea huko mpakani...
Jana nilikuwa Mlandizi, nimeshuhudia mabasi ya jeshi yasiyopungua 30 na malori yamejaa masoja tena yalikuwa yanaongozwa na gari la ma-mp likipiga king'ora. Magari hayo yalikuwa yanaelekea Dar. Akili yangu ilinambia kuwa walitokea ngerengere na walikuwa wanaelekea Dar kuchukua flight kuelekea eneo la tukio!

Tamko lazima litolewe baada ya maandalizi yote kukamilika!
 
acha kuleta maswala ya vyama hapa,Chuki zako na chadema ziishie hukohuko,hili ni swala la kitaifa na linawahusu Watanzania wote bila kujali dini,kabila wala itikadi zao,hivyo ujaribu kutumia akili wakati mwingine
Angel Msoffe, umeguisia jambo la KIUTU ambalo linahusu UTU WA TAIFA kwa ujumla wake.

When it comes to National bonders ALL BECOMES ONE ...

Udini, kando. Itikadi za vyama Kando. Ukanda Kando. Ukabila Kando. Jinsia Kando.

Wote tunaunganishwa na UTU WETU! Utu wetu ndio unakuwa common factor .... Na Common factor hiyo ndio kwa jina lingine inaitwa UTANZANIA!!

Ndani ya nguvu ya Utanzania kuna ushindi! Kwa Watanzania hili sio jambo geni ...lilishakuwepo kwa Nguvu kubwa huko nyuma sasa ni KULI UPDATE TU!!

Ni Utanaznia wetu ulio Utu wetu unafanya Utu wa taifa letu ambao ndio UZALENDO ULIOMCHAKAZA ID AMNIN DADA ...
Sasa akija Dada wa ukweli ..Dada Joyce ... Atatuamsha tuliko lala na kukumbukia enzi na tutamfanyia ...
 
Last edited by a moderator:
Nina wasi wasi na uwezo wa nchi yetu na jeshi letu kwa ujumla!
Maana naona blah blah nyingi je kama bado wanaendelea na utafiti mtafanyaje?maana ata speed boat za kusua sua
 
Back
Top Bottom