Mh.Makonda umejikwaa kidogo kumshambulia Pierre!

Mh.Makonda umejikwaa kidogo kumshambulia Pierre!

wa Tanzania wengi tunakwama katika hili suala la uliberalism.. yaani kuheshimu mawazo ya mtu hata kama hukubaliani nayo.. kwa mazamo wako unaona amekosea na pia hapo hapo wewe huenda ndio umekosea kwa mtazamo wako!
 
wa Tanzania wengi tunakwama katika hili suala la uliberalism.. yaani kuheshimu mawazo ya mtu hata kama hukubaliani nayo.. kwa mazamo wako unaona amekosea na pia hapo hapo wewe huenda ndio umekosea kwa mtazamo wako!
Dogo kajikwaa kwelikweli

Tena kajikoki kwa konki Master

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, vipi msimamo wako kama Rais mtarajiwa haungwi mkono hata baadhi ya mawaziri inaonekana wanahisia hasi na Rais wetu mtarajiwa?

Au TISS inatosha mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Escaper, kwani determinant ya nani anafaa kumpokea Magufuli ile 2025, iko determined na mawaziri kumuunga mkono?.
Soma tarehe ya bandiko hili, na uangalie ni kina nani wana determine nani ndie awe rais wetu, na wala sio TISS.

P
 
Mkuu Escaper, kwani determinant ya nani anafaa kumpokea Magufuli ile 2025, iko determined na mawaziri kumuunga mkono?.
Soma tarehe ya bandiko hili, na uangalie ni kina nani wana determine nani ndie awe rais wetu, na wala sio TISS.

P
Sawa mkuu acha nipitie bandiko ili niunge dots.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,ni dini gani inayokumbatia ulevi?
Makonda sio muumini mkubwa wa dini bali ni muhumini mkubwa wa kiki na wakati mwingine hutumia dini kwenye kiki zake.Hakuna muumini mkubwa wa dini yeyote anaye jikweza na kunyanyasa wengine kwa maslai binafsi.Hata ivyo muda wake unahesabika mwanzo wa ngoma ni lele anzidi kuzihirishia umma kuwa yeye ni zero yaani sufuri kwenye kilakitu hadi hizo kiki zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kibwengo Pierre is a talent-less, unfunny, fake, alcoholic midget full of nonsense. Huwezi kumlinganisha na marehemu Mzee Majuto, mfano. Hapawsi kabisa kupewa promo kwenye jamii sababu ni mpuuzi.
Remember he is an IMAGE of God as you are.
 
Sasa itakuwaje na tutafika wapi kama kila mara tutateremsha standards za maadili kuruhusu wapuuzi kama PIierre Liquidy na watu wa hulka yake kupewa rukhsa kueneza upuuzi wao kwenye jamii? Kama tutaruhusu watu kama hawa kupewa promo na kukubalika kwenye jamii basi itakuwa mwisho wetu. Tutafika mahali pabaya kama jamii. Itabidi kuruhusu kila mpumbaavu kufanya atakalo na zaidi ya yote kushangiliwa na kufaidika kipesa kwa upuuzi wao.
Ndjabu, habari...
Kwa maoni yangu naona unakosea kama alivyofanya RC. Hoja si kuwa huyo Liquid anafanya vizuri au watu wote wanafurahia ayafanyayo ktk ulevi. Hoja ni double standard. Kwa nini ashambuliwe kwa suala la maadili na wengine wanaokosea sana kuliko yeye kimaadili tena wapo karibu na RC wafanywe watakatifu? Isee you are missing a point on this issue.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Mh.Makonda @baba_keagan binafsi umejikwaa ,umeteleza kutamka maneno, wanafiki wanaokupigia makofi.

Wewe Mh.Makonda ni muumini mkubwa sana wa dini ya kikristo,unasoma biblia kutwa kucha ,najua unafahamu kuwa Riziki na neema kwa mtu hutolewa na Mungu,Mungu kwa wanadamu wake habagui hata kidogo,yeyote amuombaye humpa,humpa kwa namna tofauti haijalishi ni kupitia ulevi,au kupitia biashara,au kupitia usanii au kupitia uongozi vyote Mungu hujalia.

Ndio maana ukisoma Wakoritho2 9:8 inasema "Na Mungu anaweza kuwajaza kila neema kwa wingi,ili nanyi mkiwa na Riziki za kila namna siku zote ,impate kuzidisha sana katika kila tendo jema"

Kwa waislam kupitia Hadithi Qudsi Mungu anasema ,inasema (4.) Wewe hula riziki Yangu (kutoka Kwangu) na unaniasi, lakini unaponiomba Mimi hukuitikia.

Hivyo umejikwaa au kuteleza kumshambulia @officialpierre_liquid @officialpiere_liquid @pierre_konki_liquid ,Pierre amepaishwa na neema ya Mungu ,hao unaotaka wafahamike sio kwa matakwa yako au yao ni Mungu tuu. Mungu akitaka kukupaisha au kukuinua sio lazima vyombo vya habari.

vyombo vya habar hasa online bloggers wanafanya biashara wanatafuta viewers,Pierre sio mlevi namna hivyo ila ni mnywaji tuu akiambatanisha vituko,vichekesho na ucheshi watanzania wakatokea kumpenda hadi nje Kama Kenya,wakimuona wanacheka wanafurahi,media zinapata viewer,Wafanyabishara Kama @tullyswine wanamtumia kutangaza biashara,Mungu ana muinua ,Kuwa Brand Ambassador kila mtu anaweza kuwa ila hutegemea na potentiality yako kwa biashara hiyo,Pirre wana mtumia sababu ametokea kuwavutia umma.Watu wanapenda kumuona hivyo ni rahisi kupitia Pierre kuona kabisa na biashara anayoitangaza

Mfano,Dr.Shika walikuwa wanamtumia sababu watu hupenda kumuona anavyoongea hivyo kupitia hii watu wakawa wanamtumia ku brand biashara,waandishi katika kupata viewers,haya mambo ni uwezo wa Mungu,hao unaotaka wajulikane subiri hadi Mungu atakapo amua iwe hivyo,usilazimishi.Mbona ulitangaza nusu bei ya pombe?

@officialpierre_liquid usivunjike Moyo ,pambana kuna watu ni walevi wa kutupa ila ndio marafiki zetu ,mabosi zetu ,Ndugu zetu,viongozi wetu mbona hatuwasemi tumemuona Pierre tuu !
Piga kazi @officialpierre_liquid.Utabaki kuwa juuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mlevi ni mlevi tu na madhara ya ulevi ni mabaya sikuzote; hatuwezi kumsifu mlevi na kumuona ni shujaa. Tatizo wa Tz wengi hushabikia ujinga badala ya werevu
 
Mlevi ni mlevi tu na madhara ya ulevi ni mabaya sikuzote; hatuwezi kumsifu mlevi na kumuona ni shujaa. Tatizo wa Tz wengi hushabikia ujinga badala ya werevu
Inawezekana ikawa ni sahihi kabisa bila kupindisha . Lakini tambua ya kuwa huyo jamaa ni mtu kama watu wengnie, anaweza akawa baba, kaka, mjomba, mume.....wa mtu, anastahili heshima yake kama kawaida huwezi kumwita mtu wa hovyo mbele ya kadamnasi na yeye akiwemo humohumo sio busara ya kiongozi yoyote yule....uwepo wake ktk tukio hilo inaonesha kuna watu wamemthamini na ndio mana akaalikwa kumwita mtu wa hovyo maana yake umetukana watu wengi nyuma yake. By the way Bashite ajitathimini.....
 
Nchi hii ina wajinga wengi kuliko nilivyofikiria mwanzo...the Pure content ilikua "media ziache kufocus kwenye mambo ya kijinga"... Tunaweza msamehe Makonda kwa character assassination kwa Piere lakini tusisahau aliongea jambo la msingi.
 
Nchi hii ina wajinga wengi kuliko nilivyofikiria mwanzo...the Pure content ilikua "media ziache kufocus kwenye mambo ya kijinga"... Tunaweza msamehe Makonda kwa character assassination kwa Piere lakini tusisahau aliongea jambo la msingi.
Hayo mambo ya ujinga ndio chakula halisi cha vyombo vya habari!!

Habari za kijinga ndio hasa zinazopaswa kumulikwa ili vyombo vya habari vibaki kwenye chati. [usitake kujifanya mjuvi wa journalism hapa]

Ulitaka vyombo vya habari virekodi kwaya za katoliki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom