Si kila kitu cha kuamini hapa JF. Nimejifunza jambo hili, kuna ID Zikitupia thread nasoma kwa uhakika bila ya shaka yoyote. Lakini kuamini kuwa upo uwezekano wa mtu kutamka maneno kama haya hadharani, tena kwenye kampeni. Tusifikie huko, ushabiki wa mambo ya kisiasa usifike hapa. Wakati wa kampeni ni kweli huwa kuna vijembe vingi tu. Lakini kwa matusi aliyoweka huyu bwana hapa, anataka kutufanya akili zetu punguani. Tuachane na aina hii ya ushabiki. Uchaguzi utapita, wanachama wa CHADEMA, CCM na vyama vingine pamoja na sie tusio na vyama. Wote tunaishi katika jamii moja, tunachangia misikiti, makanisa, mahosptali nk. Propaganda za aina hii zitupishie mbali.