Mh Kassim Majaliwa, baada ya tar 1/3/2017 stock iliyobaki ya viroba ipelekwe wapi?

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa alitangaza kuwa kuanza March Mosi ni mwisho wa matumizi ya pombe kali ktk viroba.

Sasa wazalishaji,wauzaji na wasambazi wenye stock kubwa ya pombe hizo ktk viroba wazipeleke wapi?

Na kama walitumia biashara zao kama dhamana ktk Kuchukua mikopo Benki kisheria watalipaje mikopo yao?

Wadau hii imekaaje kisheria kwa wale walioendesha biashara hii kihalali baada ya tangazo hili maana huwezi kulazimisha stock kuishi store kama ulikuwa nayo kubwa?
 
Muda wa kusitisha uzalishaji ulitolewa kitambo almost a year. Hakuna kiwanda cha vileo kita seize production for a year na bado kukawa na circulation ya products kwa muda huo. Kama walifyatua viroba vingi wakitegemea kinga ya mwavuli wa kulialia itakuwa imekula kwao na ikumbukwe kuwa faini kwa mlevi ni miaka3 au sh50,000 au vyote! ukivisambaza kinyemera hakutakuwa na mnunuzi/mlaji.
Viroba vimechangia kwa asilimia kubwa watoto wadogo kuingia kwenye ulevi, uvuta bangi, ubwiaji ugoro na madawa mengine ya kulevya. Vimechangia kwa kiasi kikubwa sana vijana kuchuia kufanya kazi na kupenda starehe, vimechangia kushusha ufahamu na uwezo wa kufikiria.
Pia vifungashio vya viroba vinaleta athari kwenye mazingira.
Serikali piga marufuku viroba tuokoe nguvukazi ya Taifa.
 
Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa alitangaza kuwa kuanza March Mosi ni mwisho wa matumizi ya pombe kali ktk viroba.

Sasa wazalishaji,wauzaji na wasambazi wenye stock kubwa ya pombe hizo ktk viroba wazipeleke wapi?

Na kama walitumia biashara zao kama dhamana ktk Kuchukua mikopo Benki kisheria watalipaje mikopo yao?

Wadau hii imekaaje kisheria kwa wale walioendesha biashara hii kihalali baada ya tangazo hili maana huwezi kulazimisha stock kuishi store kama ulikuwa nayo kubwa?
Kiroba kilipigwa marufuku mwaka mzima uliopita.kama walidhani muda utaongezwa ndio basi tena
 
Viroba ndo hatua za awali za uvutaji bangi, unga na Inatokea (aghalabu) kutoa washeli
 
Siasa ni upuuzi wa kutaka sifa. Kilicho ndani ya kiroba ni pombe ambayo haijkatazwa. Iki uuze hiyo pombe yafaa iwekwe kwenye chombo kuendana na saizi. Wewe unapiga marufuku ujazo au karatasi? Kama ni ujazo basi watauziwa bila karatasi ya nailoni inayoitwa kiroba. watauza kama denge lua au mbege au gongo. Huhijtaji kasatasi. Mteja akitaka kuondoka nayo ataweka anakojua yeye .
Chupa za maji zatakuwa adimu kweli kweli. Vifunagadhio viko vingi tu.
 
haya hili nalo litapingwa kisa mimi ukawa!!!!watanzania jamani ebu jitambueni kwanza
 
Back
Top Bottom