Marufuku zilizowekwa na Serikali ya awamu ya tano tangu Rais Magufuli aingie madarakani, Novemba 2015

Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,343
3,280
Wakuu salam kwenu!

Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa Rais na Kuunad Serikali yake ya awamu hii ya tano mengi yametokea na mengi yanatarajiwa kutokea

Hapa nataka tukumbushane MARUFUKU zilizowekwa na serikali yake.

Marufuku hizo zimejikita katika nyanja mbili, Kiuchumi na Kijamii; Kwenye uchumi ni jinsi anavyochukua hatua kukabiliana na rushwa. Kwenye mambo ya kijamii hapa serikali inaonyesha kukanyaga haki za watu kwasababu ya kinachoitwa "maslahi ya taifa".

Sasa tujikumbushe marufuku "ban" zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano tangu kuundwa kwake:


1. Mikutano ya siasa na maandamano
Rais Magufuli alinukuliwa akisema shughuli za siasa ikiwa ni pamoja na maandamano na mikutano ya hadhara isimame hadi uchaguzi ujao mwaka 2020

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Juni 25, 2016 alipopokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.

Akiwa mkoani Singida Julai 29, 2016 Rais Magufuli alisisitiza amri aliyoitoa mwishoni mwa Juni mwaka huu ya kupiga marufuku shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, akisema wabunge na madiwani ndio wanaopaswa kufanya mikutano na shughuli nyingine kwenye maeneo yao walimopigiwa kura huku yeye akizunguka nchi nzima kwa sababu ndiyo jimbo lake


2. Marufuku ya siasa kwa Wanafunzi wa vyuo wakiwa vyuoni
Rais Magufuli amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kufanya siasa wanapokuwa chuoni bali watumie muda mwingi kusoma na kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Tanzania

Amesema hayo leo Mei 07, 2018 wakati wa ziara katika chuo cha kilimo (SUA) Mkoani Mororgoro ambapo amesema kuwa serikali inatoa fedha nyingi sana kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu na kuongeza kuwa hatasita kuchukua hatua

3. Marufuku ya ziara za nje kwa Maafisa wa Serikali
Katika siku yake ya tatu akiwa Rais tangu aapishwe Alhamisi Novemba 05, 2015 Rais Magufuli aliagiza ziara zote za wafanyakazi wa umma nje ya nchi kupigwa marufuku

Alitangaza marufuku hayo Mnamo Novemba 08, 2015 katika mkutano na Makatibu wa Wizara, Manaibu wao, Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Profes Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kukusanya Ushuru ya Tanzania (TRA), Bw Rished Bade, katika Ikulu ya Dar es Salaam

4. Marufuku Michango shule za msingi na sekondari
January 17 2017 Rais John Pombe Magufuli alitangaza kupiga marufuku aina zote za michango kwenye Shule za msingi na Sekondari za Serikali na kuwaagiza Mawaziri Ndalichako na Jafo kusimamia agizo hilo

Aliyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako

5. Wanafunzi Wasichana wenye ujauzito kutoendelea na masomo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni

Rais Magufuli aliyasema hayo mnamo Juni 22, 2017 alipokuwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kwenye mji wa Chalinze mkoani Pwani wakati akihitisha ziara yake mkoani humo.

6. Marufuku matumizi ya shisha
Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alipiga marufuku uvutaji wa shisha na kusema uvutaji shisha umekuwa ukichangia katika kudorora kwa maadili miongoni mwa vijana, na kuwapunguzia uwezo wa kiakili na kimwili wa kufanya kazi.

Bw Majaliwa, akiongea katika futari iliyoandaliwa kwenye msikiti wa Khoja Shia Ithnaasheri, Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam mnamo Julai 04, 2016, amesema watakaokaidi agizo hilo pamoja na wauzaji wa vilevi hivyo, wataadhibiwa vikali.

7. Marufuku ya matumizi ya 'Viroba'
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi Mosi, 2017 Serikali itapiga marufuku matumizi ya pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

Ametoa kauli hiyo Mnamo Februari 17, 2017 wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

8. Marufuku ya kusafirisha mchanga wa madini nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini nje ya nchi na ametaka mchanga wote ufanyiwe uyeyushaji hapa hapa nchini.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo Mnamo Machi 02, 2017 wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Kampuni ya Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

9. Marufuku kusema vyuma vimekaza
Mnamo Desemba 20, 2017 Rais Magufuli alisema kuwa watu ambao wanasema vyuma vimekaza na wale ambao wamekuwa wakisambaza takwimu mbalimbali za kupikwa kukamatwa na kuwekwa ndani na baadaye kupelekwa mahakamani

Aliyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma

Aidha, Alhamisi Desemba 14,2017 alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dodoma, Rais John Magufuli alisema vyuma vikikaza vinatakiwa kuwekwa grisi vilainike, vinginevyo vitavunjika kabisa.

10. Marufuku ya Matumizi ya fedha za kigeni ikiwemo Dola
Serikali ilipiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni ikiwamo ‘dola’ kuanzia Januari 1 mwaka 2018, na kueleza bei zote za huduma na bidhaa zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa kutoa agizo hilo mnamo Desemba 29, 2017 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango alisema matumizi ya fedha za kigeni sambamba na Shilingi ya Tanzania wakati wa kufanya miamala mbalimbali yanaweza kuwa na athari kiuchumi ikiwa pamoja na kudhoofisha thamani ya shilingi.

Alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18

11. Marufuku uuzaji wa Mazao yakiwa shambani
Serikali imewapiga marufuku wafanyabiashara, walanguzi na wakulima kuuza mazao yakiwa bado shambani na kusema pindi atakaebainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo yamebainishwa Mei 07, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa

12. Marufuku Mwanafunzi kujiunga shule ya Bweni bila kupima Kifua Kikuu(TB)
Serikali imesema ni marufuku mwanafunzi yeyote kujiunga na shule ya bweni bila kupimwa maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo Jumanne Machi 20, 2018 wakati akizindua dawa maalumu ya kutibu TB ya watoto

Aidha, Waziri Ummy amemuagiza Mganga Mkuu wa Serikali kuhakikisha anasimamia suala hilo na kuwapa maelekezo waganga wakuu wa wilaya na mikoa

13. Marufuku kusafirisha mizigo au bahasha kwa kutumia magari ya abiria
Serikali imepiga marufuku kusafirisha mizigo, vifurushi na bahasha kwenye magari ya abiria, mpaka kuwe na kibali maalum kutoka Mamlaka ya mawailiano nchini (TCRA)

Marufuku hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mnamo Machi 5, 2019 alipokuwa akizungumza na watumishi wa taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania, mjini Musoma

14. Marufuku Walimu wa kuingia na viboko darasani
Serikali imepiga marufuku walimu wanaofundisha madarasa ya kuanzia elimu ya awali hadi darasa la tatu kuingia na viboko darasani.

Kauli hiyo imetolewa Julai 29, 2019 mjini Mwanza na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Tixon Nzunda wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuandaa vipindi vya redio kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE-Tanzania).

Nzunda alisema kuwa vitendo hivyo vinasababisha wanafunzi wa madarasa hayo kuogopa na kutokuwa wasikivu wakati wanapofundishwa

15. Marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa Wanafunzi bili kibali maalum
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha imepiga marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi bila kibali maalum

Pia amepiga marufuku Walimu kutembea na viboko, Ole Nasha ametoa agizo hilo leo Novemba 13, 2018 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM Rose Tweve aliyetaka kujua kauli ya Serikali kwa Walimu wanaokiuka sheria za adhabu kwa Wanafunzi.

16. Marufuku Wananchi kununua nguzo za umeme
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema wananchi hawapaswi kulipia nguzo wanapotaka kuunganishiwa umeme kwa kuwa hilo ni jukumu la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza mnamo Julai 28, 2019 akiwa ziarani katika Wilaya ya Babati na Mbulu mkoani Manyara, Waziri alitoa onyo kwa mtumishi yeyote wa TANESCO atakayebainika kutomuunganishia umeme mteja aliyelipia huduma hiyo kwa kisingizio cha kutokuwepo nguzo au kumtaka alipie

17. Marufuku usafiri wa Bodaboda Visiwani Zanzibar
Kutokana na kuongezeka kwa ajali za barabarani zinazotokana na uendeshaji wa Pikipiki maarufu Bodaboda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia bodi ya usafiri barabarani imepiga marufuku usafiri huo maarufu bodaboda kutumika kama chombo cha biashara visiwani Zanzibar.

Marufuku hiyo ya bodaboda imeanza leo Septemba 21, 2018 kama ilivyoelezwa na katibu wa bodi ya usafiri barabarani Mohammed Simba Hassani

18. Marufuku kusafirisha Wanyama hai nje ya nchi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi KIgwangalla amesema Serikali ya Tanzania haitaruhusu usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi. Kauli hiyo imefuta agizo la Wizara hiyo ambayo iliweka zuio la miaka mitatu na Mei, 2019 ilikuwa ndiyo mwisho wa zuio hilo

Kigwangalla ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Februari 8, 2019 wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Muheza (CCM), Balozi Adadi Rajabu.

19. Marufuku Wagonjwa kuangalia tamthilia wakiwa hospitali
Serikali kupitia Wizara ya Afya, imepiga marufuku runinga zote za hospitali za serikali kuonesha wagonjwa vipindi vya kawaida kama tamthiliya badala yake waonyeshe vyenye kutoa elimu ya afya.

Marufuku hiyo, imetolewa Januari 14, 2019 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kufanya ziara hospitalini hapo

20. Marufuku usafirishwaji wa Kaboni kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine
Serikali kupitia Wizara ya Madini imepiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kwa ajili ya kuchenjulia madini ya dhahabu kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na kusisitiza kuwa haitasita kumchukulia hatua za kisheria mchimbaji wa madini atakayekiuka agizo hilo.

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 18 Oktoba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Saza kilichopo wilayani Songwe mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

21. Marufuku upigaji ramli nchini
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jana tarehe 13/01/2015 imetangaza kupiga marufuku upigaji wa RAMLI na kuanza kwa oparesheni ya nchi nzima ya kuwabaini na kuwakamata watu wanaojihusisha na upigaji ramli ikiwa ni mkakati wa kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)

22. Marufuku ugawaji viwanja 'Pandikizi'
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amepiga marufuku ugawaji viwanja ambavyo tayari vimemilikishwa huku mmiliki wake wa awali akitafutiwa eneo lingine.

Hatua hiyo inafuatia kushamiri kwa tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri nchini kugawa maeneo ambayo tayari yana wamiliki wake wa awali na kuwapa watu wengine wenye uwezo kifedha huku wamiliki halali kuahidiwa kupatiwa kiwanja kingine

23. Marufuku kutengeneza, kuuza, kuingiza na kutumia mifuko ya plastiki
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuanzia Juni Mosi, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuuza, kuingiza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.

Alisema katika kuchukua hatua hizo kuna bidhaa lazima zifungashiwe kwa mifuko ya plastiki, “vifungashio kwa bidhaa hizo havitapigwa marufuku kwa sasa




 
Yani serikali ipige marufuki vitu vyote

Lakini sio kuzuia wasichana kuvaa nguo fupi,
Wengine hapa ndio tunachagua vizuri sasa utauziwaje nguo kwenye gunia
Lakini wakiwa na vinguo vyao vifupi wanavutia
 
Marufuku kupandisha mishahara na marupurupu ya wafanyakazi mpaka nchi inyookeee....

Marufuku kusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha magogoni.......
 
7. Marufuku Viroba
8. Marufuku kusema vyuma vimekaza
9. Marufuku Michango mashuleni
10. Marufuku kusafiri nje ya Nchi Watumishi wa umma
 
7. Marufuku Viroba
8. Marufuku kusema vyuma vimekaza
9. Marufuku Michango mashuleni
10. Marufuku kusafiri nje ya Nchi Watumishi wa umma
Nakumbuka hii marufuku ya viroba kuna mfanyabiashara aliripotiwa kufariki baada ya stock yake ya viroba kutoisha ndani ya muda uliowekwa kabla ya ban.

Sikumbuki ilikiwa mkoa gani.
 
Marufuku kupandisha mishahara na marupurupu ya wafanyakazi mpaka nchi inyookeee....

Marufuku kusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha magogoni.......
Hii marufuku kutosafiri bila muhuri wa ikulu kwawafanyakazi wa uma naona ilikuwa sawa kiasi fulani. Magu aliona dawa ya hawa jamaa waliozoea kwenda nje ya nchi kuliko wavyoenda kusalimia kwao ni muhuri wa ikulu tu.

Well, sifahamu hadi sasa ni kiasi gani kimeokolewa. Je una data tujuzane?
 
Wakuu salam kwenu


Toka Rais Magufuli ameunda serikali yake miaka miwili sasa imepita. Katika hii miaka miwili mambo mengi yametokea.


Hapa nataka tukumbushane MARUFUKU zilizowekwa na serikali yake.

Hizi "ban" zimejikita sehemu mbili. Uchumi na jamii. Kwenye uchumi ni jinsi anavyochukua hatua kukabiliana na rushwa. Kwenye mambo ya kijamii hapa serikali inaonyesha kukanyaga haki za watu kwasababu ya kinachoitwa "maslahi ya taifa".

Na inaonekana serikali imejiandaa kubeba risk kuhusu kutojali haki za binadamu.

Lakini pamoja na hatua JPM anazochukua hakuna guarantee serikali yake itawaletea maendeleo wananchi.

Sasa tujikumbushe marufuku "ban" toka serikali iundwe.


1. Usajili wa meli za kigeni


Last week serikali ilitoa temporary ban kusajili meli zote za kigeni. Sababu ilikuwa kukamatwa meli iliyopeperusha bendera ya Tz huku ikiwa na dawa za kulevya.


2. Marufuku ya kusafirisha madini nje


Last year serikali iliweka marufuku kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Haikuishia hapo serikali ikaitaka kampuni ya Barrick Gold kulipa $190bn kama taxes, interests and fines. Baada ya mzungumzo ikakubaliwa walipe $300m


3. Wasichana wenye ujauzito kutoendelea na masomo


Akiwa kwenye rally Magu alitoa hii marufuku. Ilileta sitofahamu kwenye jamii. Watu wa haki za binadamu na watoto walipinga sana hili.


4. Mikutano ya siasa na maandamano


Hii ilianza kukatwa kwa bunge live. Ikafuata marufuku mikutano ya siasa na maandamano. Iwe ya amani au vinginevyo.


5. Kufungiwa kwa magazeti na radio


Kwa kipindi hiki cha miaka miwili magazeti manne yamefumgiwa ikiwemo Wawio na Mwanahalisi. Pia mwaka juzi Radio 5 na Magic Fm walikumbwa na dhahama.


Lakini pia mtandao wetu JF nao ulipata misukosuko. Wote tunakumbuka dola ilivyokuwa inautaka uongozi wa JF kutoa identity za watumiaji.


6. Shisha


Hii marufuku alitoa prime minister Majaliwa. Hahaaa nakumbuka Makonda akamtuhumu Siro enzi hizo mkuu polisi kanda ya Dsm eti alipelekewa fedha na wafanyabiashara ya shisha.


Nimekumbuka haya. Je unakumbuka marufuku nyingine ya serikali ya uncle Magu?
Usinijalibu sijakuona ohooo
ce37689d83b6048885448db9b5eaae94.jpg
 
Nakumbuka hii marufuku ya viroba kuna mfanyabiashara aliripotiwa kufariki baada ya stock yake ya viroba kutoisha ndani ya muda uliowekwa kabla ya ban.

Sikumbuki ilikiwa mkoa gani.
Aisee huyu jamaa alijipiga risasi baada ya stock yake yenye thaman ya zaidi ya one bilion ilipofungiwa stoo na Kamanda Mambosasa wakati huo akiwa Dodoma, Anaitwa Mr. Olomi ni jirani yangu kule moshi alikua tajiri haswa mkuu, pale kijijin Umbwe kajenga hekalu haswa, baada ya kujiua tu miez kama miwili na ushee hivi baba yake mzazi nae alifariki maana alikua anauguziwa pale Dodoma kwa huyu jamaa
 
Aisee huyu jamaa alijipiga risasi baada ya stock yake yenye thaman ya zaidi ya one bilion ilipofungiwa stoo na Kamanda Mambosasa wakati huo akiwa Dodoma, Anaitwa Mr. Olomi ni jirani yangu kule moshi alikua tajiri haswa mkuu, pale kijijin Umbwe kajenga hekalu haswa, baada ya kujiua tu miez kama miwili na ushee hivi baba yake mzazi nae alifariki maana alikua anauguziwa pale Dodoma kwa huyu jamaa
Duh pole mkuu. Kumbe jamaa alijipiga chuma.

Aisee kwenye hii ban ya viroba serikali kama ilikurupuka flani hivi.

Muda kabla ya ban ulikiwa mfupi. Pia haikujali wafanyabiashara waliokuwa na stock kubwa.
 
Duh pole mkuu. Kumbe jamaa alijipiga chuma.

Aisee kwenye hii ban ya viroba serikali kama ilikurupuka flani hivi.

Muda kabla ya ban ulikiwa mfupi. Pia haikujali wafanyabiashara waliokuwa na stock kubwa.
Huyu jamaa alikua anailisha dom aisee na kwa maisha yake nlijua kua kiroba ilikua napesa maana alikua don flan hivi sema ilee akaona bora asepe tu
 
Back
Top Bottom