Huo ni wajibu wake na ni lazima atekeleze kwa kuwa anakusanya kodi.Kama si ufisadi barabara hii ilitakiwa ikamilike muda mrefu.
.......
Duh umekomaa kwa propaganda.nimefurahi ujasiri wako wa kutumia makosa ya mwenzako kujiimarisha kisiasa
Ninachokiona hapa unacheza siasa na wanasiasa vijana wenye misimamo mikali kama ya kwako ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu.type ya akina Tundu Lissu na Sheikh Ponda
Ninachojua ni kwamba unahiandaa kugombea Rombo ndiyo maana uko vitani na nimeona jinsi ulivyokomaaa na hili kwenye mitandao na hasa page yako ya facebook na twitter.hoja ulizojenga ni kweli lakini kumbuka mtu huwa anakosea na hata wewe utakapokua mbunge utafanya makosa
Misimamo mikali kama hii itazidi kutuletea machafuko tu mkuu.Watu wa Rombo jihadharini na wanasiasa wa aina hii.Selasini anapiga kazi na hakuna wa kumtoa na Chadema tukifanya makosa huyu kumpitisha huyu Saanane basi yatatokea ya Tarime endapo atajiunga na CCM na kugombea tena huko
Hivi wewe ulipokuwa unafaulu Darasani mbona Wazazi wako hawakuita kukupongeza kwa sababu eti ni wajibu wako kusoma na kufaulu? Hizi ni akili za kitoto tu unastahili kusamehewa kwa vile hujui hata usemalo.
hongera mheshimiwa joseph selasin, mbunge wa rombo kwa kuwa muwazi kuhusiana na utendaji murua wa rais jk kwa kuwezesha ujenzi wa barabara jimboni mwake.
Amediriki kutamka mbele ya rais jk kuwa "ingekuwa amri yake barabara husika ingeitwa jakaya kikwete road"
source: Taarifa ya habari tbc, saa 2 usiku, october 30, 2012
Chadema wataona 2015.Nilimuona Ben Saanane akiponda uchaguzi wa vijana CCM kwamba ni Mnada huku akisahau uchaguzi wa BAVICHA ambao alikua mgombea walienguliwa kwa Rushwa
Nilimwambia hawawezi kupambana na UVCCM siku walipokua wakirushiana maneno makali na Beno Malisa pale Rose Garden.Pia yeye ni sehemu ya waliohusuka kupandikiza mamluki Uvccm wakishirikiana na akina Sango kasera na Makondo ambao walikua wagombea makamu mwenyekiti kwa lengo la kuidhoofisha UVCCM ili asipate changamoto andapo atashinda uchaguzi wa BAVICHA.Aachane na CCM
hivi ritz hunaga likizo.....mbona wafanyakazi wengine wanapewa likizo na nape?....au kanuni ni double standard?
Duh umekomaa kwa propaganda.nimefurahi ujasiri wako wa kutumia makosa ya mwenzako kujiimarisha kisiasa
Ninachokiona hapa unacheza siasa na wanasiasa vijana wenye misimamo mikali kama ya kwako ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu.
Type ya akina Tundu Lissu na Sheikh Ponda ninachojua ni kwamba unahiandaa kugombea Rombo ndiyo maana uko vitani na nimeona jinsi ulivyokomaaa na hili kwenye mitandao na hasa page yako ya facebook na twitter.
Hoja ulizojenga ni kweli lakini kumbuka mtu huwa anakosea na hata wewe utakapokua mbunge utafanya makosa.
Misimamo mikali kama hii itazidi kutuletea machafuko tu mkuu.Watu wa Rombo jihadharini na wanasiasa wa aina hii.
Selasini anapiga kazi na hakuna wa kumtoa na Chadema tukifanya makosa huyu kumpitisha huyu Saanane basi yatatokea ya Tarime endapo atajiunga na CCM na kugombea tena huko.
Jk hajashtuka sifa alizopewa..........hahaaaa siasa bana.........
Niliisha sema kwa JK lazima CDM waisome namba , na hapo bado kila mbunge wa cdm atapiga goti kwake kutoa shukrani
Kwani CDM wao na hoja zao za mabadiliko watakuwa hawakusanyi kodi? Maendeleo yatakuja kwa kutumia mishahara yao ya mifukoni? kazi kweli kweli. Subirini 2015 mtakavyokung'utwa na wananchi kwa vile sasa wameshajua kuwa CCM iko kikazi zaidi tofauti na ninyi mnaokesha kutaka kuingia ikulukwa majungu kama haya na kubeza yaliyofanywa na serikali.
Hongera Selasini kwa kutambua mchango wa rais Kikwete.
Vijana hizo roho za kwa nini mpaka lini? Mh Selasini amesema ukweli wake wewe unapata shida gani? Kama serikali ya Mh Kikwete imefanya jambo jema waache wasifiwe, tatizo nini vijana mnapenda kulaumu tu?
Mbona hizo barabara alizojenga Mh Kikwete ndizo mnazitumia kufanyia maandamano yenu? Au mtaanza kuandamana pembeni ya barabara?
Mimi nasema hivi mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni - kama hutaki jitundike. Liwalo na liwe (Mh. Pinda)
Wewe ndo yule mzazi ambaye akileta nyama anawasimangia wanawe eti shukuruni sana mmezaliwa kwangu la sivyo hizi finyango mngezisikilizia mbali. Kazi ya ujenzi wa nchi siyo ombi na siyo jambo la kuliona ajabu ni wajibu wenu kulitekeleza.
Kinachowafanya mkurupuke na kujenga ni nini na huo uwezo mmeupata wapi wakati kila siku mnailaani nchi kuitamkia umaskini?
Huyu Selasini ni sawa tu na Masumbuko Lamwai matapeli zandiki ndumilakuwili.
Safi kada wa cdm kwa kuwa mkweli na kukubali ukweli mana kina slaa wanapinga kila kitu hata penye ukweli
mchango wake umeonekana, hiv alitumia pesa zake Tshs ngapi?