Mwisho wa siku najiuliza sana kama kuna haja ya kuwa proffessional inapokuja mambo ya starehe? Mfano mimi ni mpenzi mkubwa wa clouds. It is the only radio ninayoisikiliza. Lakini ni mpenzi wa jide dam dam. Natamani kuzisikia nyimbo zake wakati wa vipindi. Sasa personal interest zao na ubabe wa kutopiga nyimbo zake si ninaonewa mimi? Kwa nini nalazimishwa kumchagua mmoja?
Suala la radio station kutopiga nyimbo za msanii fulani au DJ fulani katika radio station fulani kutopiga nyimbo za msanii fulani si jambo geni hata kidogo.
Chris Brown alipomdunda Rihanna ile 2009 kuna baadhi ya radio stations kwenye majimbo kadhaa ziliacha kucheza nyimbo zake licha ya Chris Brown kuwa ni msanii anayependwa.
Hata R. Kelly kipindi anakabiliana na tuhuma za statutory rape kuna vipindi na radio stations zilizoacha kupiga nyimbo zake. Yes, the grammy-award winning R. Kelly. Kipindi cha asubuhi cha Tom Joyner ambacho ni syndicated kiliacha kabisa kupiga nyimbo zake hadi pale alipopatikana hana hatia ndiyo wakaanza tena kuzipiga. Na huo uamuzi ulikuwa ni wa Tom Joyner mwenyewe.
Hivi majuzi tu Rick Ross na Lil Wayne nao wametishiwa nyimbo zao kutokupigwa na baadhi na radio stations kisa maneno kwenye wimbo yanayounga mkono ubakaji
"Put Molly all up in her champagne, she ain't even know it, I took her home and I enjoyed that, she ain't even know it," kwenye wimbo wa UOENO na kuhusisha jina la Emmett Till kwenye hii line ya Weezy
"beat that pussy up like Emmett Till" kwenye wimbo wa Karate Chop wa Future.Ingawa sijasikia kama kuna station yoyote iliyoacha kupiga nyimbo za hao mabwana makampuni ya Reebok na Pepsi ambayo walikuwa wanatangaza bidhaa zake yamewaachisha kufanya hivyo.
Sasa leo/jana Ruge kaelezea hiyo ya nyimbo za Jide kutopigwa Clouds. Kasema kwamba siku ambayo Jide alipoanza kumwaga lawama zake kwamba nyimbo zake hazipigwi hapo Clouds, ile nyimbo yake mpya ya Joto Hasira ilikuwa tayari imeshapigwa mara 46. Hivyo Jide aliongopa. Na Ruge kasema ushahidi wote wanao wa lini nyimbo zinapigwa kwa sababu kila kitu kiko digitized na records zipo. Sasa yeye Jide habari za kwamba nyimbo zake au hiyo ya huo wimbo wake mpya kutopigwa Clouds alizitoa wapi?
And guess what? Hata mimi naweza ku vouch anachosema Ruge kwa sababu ile ile siku Jide katoa hiyo shutuma niliusikia huo wimbo ukipigwa mara mbili Clouds - kwenye kipindi cha XXL na Jahazi.
Huyo mdada hakuwa hata na decency ya kuomba radhi achilia mbali hata kukiri tu kwamba kwenye hilo alichemka. Sasa mtu mnapiga nyimbo zake lakini yeye bado anang'ang'ania kwamba hamzipigi na anaendelea kuwapaka matope huko kwenye blogosphere, what do you do?
Tupa pembeni huko. I'm pretty sure Clouds can live without her.
Kuna watu huwa wanapigwa marufuku kuingia club, restaurant, madukani, sokoni, na kadhalika, kwa sababu mbalimbali. Na kwa mujibu wa Ruge, hata Diamond, Ray C, Ali Kiba, n.k nao nyimbo zao zimeshawahi kuacha kupigwa kwenye vituo vingine vya redio hapo Dar.
So it's nothing new - it happens at many places.
Having said all that, kwa nini yeye Jide na wapenzi pamoja na maadui wa Clouds wasi join forces na kuiangushia mbali tu hiyo redio pamoja kampuni mama yake?
Coz the way people are acting it's like there is nothing else they can do without Clouds. If the place is that bad just call for a boycott and go for the jugular - i.e. go after the companies that buy commercial time. Call for a boycott of their products.
There are 80 plus radio stations in the country and from the way people are making it sound you would think there is only one. Good grief.