Hossam
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 3,538
- 2,155
Huu sio muda wa kampeni bali ni wasaa wa kukijenga chama, ama niseme huu ni wakati wa kueneza na kuhibiri elimu ya uraia ili kila mtanzania kwanza aelewe wajibu wake lakini pia mageuzi ya kisiasa yapatikane kwa amani.
Nimesikia kutoka kwa mtu wa karibu kabisa na Mh Mchange kuwa hivi sasa chama chake yaani Chadema kinamhujumu huko Kibaha mjini kwa kufanya mikutano ya siasa majukwaani bila kumhusisha na pia bila kumjulisha. Kwa ufupi hizi ni habari ambazo Mchange mwenyewe anatakiwa kuja hapa jamvini na ama kukanusha ama kukubaliana nazo, kama si hivyo Chadema itakuwa na sintofahamu kuu juu ya huyu mheshimiwa. Chadema hakiwezi kamwe kumtelekeza Mh Mchange kwa kuwa tunaamini huyu alishiriki kwa kiasi kikubwa kukijenga chama wakati wa kampeni za mwaka 2010. Chadema haiwezi kusahau mchango wake mkubwa wa hali na mali katika jimbo ambalo chama kilimuangukia asimame.
Suala la kulalamika kwa informer wa Mchange kwamba chama kinataka kumpiga zungu na kumuweka mmoja kati wa waadishi nguli wa habari za kila wiki hususan za rais wetu, hakuwezi kutoa tafsiri kwamba chadema imemtupa Mchange.
Lakini ifahamike kwamba kama Mchange hapatikani kwenye simu yake ya kiganjani hasa ile ya zain, halafu hatoi taarifa kama hatakupo Kibaha, unadhani chadema iliyo na ratiba tight ya mwaka mzima itaahirisha elimu ya uraia kwa watu wa Kibaha? Mchange ni lazima awe bega kwa bega na chama ili kujua nini kitafanyika ama kwake ama kwingineko Tanzania.
Sitaki kumsema sana Mchange, natambua mchango wake, ila ni lazima utaratibu wa chama uheshimiwe na ufuatwe.
Ni mimi,
Pangu Pakavu,
Nawasalimia.