Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

Jeshi lililo makini lingeweza kuchukulia serious hi taarifa za Tendwa, tusisibiri mpaka mauaji yatokee ndiyo wachukue hatua, na hii ndio udhaifu wa jeshi la polisi wanashughulikia reaction. Mwiteni Tendwa aeleze ni wazee gani hao na wao waitwe kwa mahojiano na karipio kali

Nadhani kamanda aende mbali zaidi akachukue maelezo kwa Tendwa
 
kama ndio hivyo basi,huyu tendwa alishaitwa japo kuhojiwa tu?au ndo kila mtawala anawajibu wa kuropoka tu kutokana na nafasi yake
 
kama ndio hivyo basi,huyu tendwa alishaitwa japo kuhojiwa tu?au ndo kila mtawala anawajibu wa kuropoka tu kutokana na nafasi yake

Kwa kweli inabidi utawala wa sheria ufanye kazi hapa
 
Huyu Tendwa ni kibaraka mkuu wa CCM,ila nayeye siku zake zinahesabika!
 
haitoshi hiyo kamanda Andengenye.. kamata huyu jamaa awataje na wenzie.. uwafungulie jalada la kutishia kuua..
 
Washiri CHADEMA sasa wajipanga kukiumbua CCM juu ya Kamanda Lema kule Arumeru.
 
Siku zinahesabika za chama cha majambazi CCM! Ukombozi umefika,majambazi CCM yanatafuta njia za kulikimbia Taifa.
 
Huyu Tendwa ni kibaraka mkuu wa CCM,ila nayeye siku zake zinahesabika!

MWAKA 2010 MH. Dr.WPS ALIWAONYA CCM WAACHE KULALAMIKA KUHUSU UDINI BALI BALI WANATAKIWA WAMKAMATE NA KUMPELEKA MAHAKAMANI YEYOTE ANAYEHUSIKA NA UDINI ILI SHERIA IFUATE MKONDO WAKE. LEO HILI LA UKABILA LIMEKUJA PATAMU MAANA WASHIHIRI NA TENDWA WANATAKIWA WAPELEKWE MAHAKAMANI KUJIBU MASHTAKA YA KUENDEKEZA UKABILA HAPA NCHINI MAANA CDM NAAMINI HUWA HAWAPENDI KULALAMIKA.
 
Mh lema tupo pamoja na wewe katika kupigania haki na utu wa mwanadamu,udhalimu wa CCM dhidi ya watanzania hauwezi kuvumiliwa tena,mapambano muda wote,kila saa na kila muda! Viva Mh lema.
 
Lema akitishia kuu kosa akitishiwa sio kosa hao ;hapa lazima kieleweke hao wazee na msemaji wao twenda wachukuliwe hatua
 
Nawasalimu

Leo asubuhi nimesikia habari za uzushi na majungu kutoka katika gazeti la Chama Cha Mapinduzi Uhuru pamoja na gazeti la serikali la Habari leo .

Hivyo basi kilichosemwa na magezeti ya Uhuru na Habari leo ya leo tarehe 23/2/2012 ni uzushi na propaganda , Magazeti haya ya CCM yatatumika sana kipindi hiki kama yalivyotumika kule Igunga yalipojaribu kutaka kuwatenganisha watu hata kwa dini zao lakini baadae ukweli ulijulikana na ikawa aibu kwao .

Kwa zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wa Taifa letu kutoka kwa mkoloni bado Watanzania wa Arumeru sio huru na Watanzania wote kwa ujumla bado wanaishi maisha magumu kama wakimbizi nje ya Nchi yao.

Ninafahamu wajibu wangu katika kupigania demokrasia safi ya Nchi yangu na wakati huu jimbo la Arumeru Mashariki litakuwa mfano wa mapambano hayo na nitakuwa mstari wa mbele bila hofu wala kumuogopa mtu yeyote na wa cheo chochote katika kupigania ukweli na haki.

Wajibu wangu na wa chama changu kwa sasa ni kutoa matumaini kwa watu wote wa Taifa letu , na tunazo sababu za msingi za kwenda kushinda jimbo la Arumeru na ni wito wangu kwa kila kijana wa Arumeru anayeishi mjini kuona fursa hii ni kwa ajili ya ukombozi wa Nchi yetu na sio Arumeru peke yake na hivyo kwenda kutoa elimu vijijini tulikoacha wazee wetu.

Jana nilikuwa Meru , wazee na vijana wamekataa kuburuzwa na siasa za CCM ambazo kwa miaka hamsini ya uhuru wa Nchi hii zimeshindwa kutatua matatizo yao bali kufikiri rushwa ya pesa kipindi hiki cha Kampeni ndio mahitaji yao ya Msingi.

Nimesikia Tendwa msajili wa vyama vya siasa naye ameanza kusaidia CCM kufanya propaganda chafu labda ni vyema akatambua wajibu wake na sio kuanza kufanya kazi za siasa za CCM ni vyema akajua kuwa yeyote anayeitetea uovu leo itakuwa hasara kwake au kwa familia yake kesho .

Mwisho .

Ninajua macho ya Watanzania yako Arumeru mashariki , Ninawatia moyo wale mlioko mbali lakini mnapenda mabadiliko , sisi tulioko huku tutapambana kwa niaba yenu kufa na kupona kuhakikisha haki, usawa, na demokrasia vinapata thamani halisi bila uhuni wowote kufanikiwa.

Msiogope pengine huwezi kabisa kufika Arumeru kusaidia ukombozi basi wewe huko uliko tuombee kwa Mwenyezi Mungu , hakika hatutakubali uhuni ,udhalimu , na Nguvu ya rushwa iwachagulie ndugu zetu wa Arumeru Mbunge , kama Mbunge mmoja wa CCM Mwigulu Nchemba alivyotamba jana pale katika Hotel ya Mount Meru kuwa pesa bado hazijaanza kumwagwa kwani ndio kwanza ziko njiani zinakuja.

Hata hivyo Msiogope Udhalimu utashidwa Arumeru "" Ni Afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu .

Godbless J Lema (Mb)
 
kama ndio hivyo basi,huyu tendwa alishaitwa japo kuhojiwa tu?au ndo kila mtawala anawajibu wa kuropoka tu kutokana na nafasi yake

tendwa ni mzigo tena ni gunia la misumari ukilibeba lazima likutoboetoboe sijajua kwanini jk anamkumbatia.
 
Lema aende campaign kokote ila nae akae akijua Arusha kumedorora. Akae atulie, atulize vurugu kwa wafuasi wake afanye shughuli za maendeleo. Wabunge wenzake wa CDM tunaona wanayoyafanya yeye yako wapi? Ajue 2015 iko mlangoni inabisha hodi.......................... Hakuchagyuliwa kwenda mahakani kujibu kesi bli kuhamasisha maendeleo plz
 
Kumtumia mtu ujumbe wa kukusudia kumuua ni Kosa kisheria, na mtu yeyote anayefanya hivyo anapaswa afikishwe mahakamani. Washiiri ni Watuhumiwa na Tendwa ni Shahidi. CDM mshiache kututendea haki kwa kutokuwafikisha Washiiri mahakamani pamoja na Tendwa kama shahidi namba moja. Hapa ndipo Tendwa atatia akili ya kukataa kutumika next time.
 
Tendwa ni jaji mstaafu hivyo natarajia kabobea kwenye sheria. Cha kushangazza ni kitendo chake cha kukaa na hao wazee wa Meru (nafikiri anawasingizia) wakamweleza mipango yao ya kumuua Mheshimiwa Lema! Tendwa hastuki kwamba hapa kuna mauaji yanapangwa.
Badala ya kutoa taarifa hii polisi anakimbilia kumtahadharisha Lema kupitia vyombo vya habari, huu ni ******. Au ndo style ya CCM ya kutisha waatu?
 
Pamoja kamanda wa majeshi ya ardhini kikosi cha CDM2012ARUMERU. Pamoja Tutashinda!
 
Back
Top Bottom