Mguu wangu masikini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mguu wangu masikini!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 17, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa mtumishi wa idara ya serikali mkoani Iringa kuanzia mwaka 1977 hadi 1983 nilipopata ajali ambapo ilibadili kabisa maisha yangu, kutoka yenye matarajio hadi maisha yaliyosheheni giza totoro. Nikiwa hapo Iringa, familia yangu ilizoeana na familia nyingine ya bwana mmoja ambaye alikuwa na maduka ya vyakula. Mke wa bwana huyo alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi. Mke wangu alikuwa ni mwalimu shule ambapo mwanamke huyu alikuwa akifundisha.

  Katika urafiki huo wa kifamilia, mimi niliingiliwa na ibilisi wa kumtamani yule mke wa mfanyabiashara, ambaye naweza kusema, alikuwa ni rafiki yangu, kwani kuzoeana kwetu kulikuwa kumepevuka kidogo . Mwanamke huyu naye kumbe alikuwa amevutiwa nami. Wakati huo nilikuwa bado kijana, ninayependeza. Tulianza uhusiano mwaka 1979, miaka miwili baada ya mimi kufika Iringa na kujuana na familia hii. Wakati huo ndoa yangu ilikuwa na miaka sita tu, maana nilikuwa nimeoa mwaka 1973. Tulianza kukutana kwa siri na mwanamke huyu, ambaye alikuwa mdogo ukilinganisha na mumewe, kwani mumewe alikuwa ni mtu mzima kidogo, akiwa kwenye umri wa mwanzoni mwa miaka 50. Yeye alikuwa na umri wa miaka kama 25.

  Uhusianao wetu na mke wa jamaa yangu ambaye hapa nitamwita Mfanyabiashara ulianza kwa kasi kubwa sana. Tulikuwa tumehemkwa kwa nguvu kubwa kiasi kwamba nilianza kuhofia. Nilijitahidi sana kuweka mipaka ili tusifikie mahali tukajisahau. Mwaka 1981 habari zilianza kuvuja kuhusu uhusiano wetu. Mke wangu ambaye alikuwa anafundisha na huyu hawara yangu shule moja, huku wakiitana marafiki, aliniambia kwamba, kuna jambo linanongónwa kwamba, nina uhusiano na huyu rafiki yake, mke wa mfanyabiashara, ambaye hapa mke huyo, nitamwita Waridi, ikiwa ni tafsiri ya kiswahili ya jina lake halisi.

  Niliposikia habari hiyo kutoka kwa mke wangu nilishtuka sana. Lakini nilimudu kujifaragua nakujitetea kiasi kwamba, ingekuwa ni mtu mwenye moyo mgumu sana ambaye asingeweza kulainika. "Watu hawapendi wakiona familia mbili kama zetu. Mimi bado kijana mdogo, nina kazi nzuri, na fedha na wewe una kazi, hawa wenzetu wana biashara nyingi hapa mjini, ni lazima utasikia mengi. Shemeji Waridi hawezi hata kufikiria kuhusu upuuzi huo na mimi wala sijawahi hata kuota, siyo kwa Waridi, bali kwa mwanamke yeyote." Nilimaliza kujitetea.

  Nilimwonya sana Waridi baada ya kukutana. Aliniambia naye mume wake alikuwa amemuuliza kuhusu madai anayopata ya uhusiano wetu. Niliogopa sana. Lakini alisema, alikuwa amemudu kumtuliza kabisa na wala hilo halikuwa suala tena. Nilipata moyo na mapenzi yetu yakapamba moto zaidi. Mwaka 1982, mke wangu alinisakama tena, safari hii akidai kwamba, ana vyanzo vya kuaminika kuhusu uhusiano wetu na Waridi. Nilimwambnia kwamba, sina haja ya kubishana naye, ila niko tayari kushika kitabu cha dini tuape kwa laana zote. Nilipomwambia hivyo alinywea. Nilimwambia hivyo kwa makusudi, nikijua kwamba, alikuwa ni mtu dini sana. Aliogopa akiamini kwamba, kusema kwangu vile, kulikuwa na maana ya uhakika kwamba sikuwa nashiriki jambo hilo.

  Alisema, hao watu wanaomwambia, wana sababu gani ya kudanganya. "Nimekwambia watu wana hila mke wangu. Dini inasema, kufumania ni kuona kwa macho na siyo mtu mmoja, bali wanne. Unadhani inasema hivyo bure tu, hapana , ni kwa sababu ya mambo kama hayo." Nilizidi kumfanya aniamini. Ilibidi sasa tubadili mikakati yetu na Waridi. Nilikuwa nachukua gari la kazini na tukawa tunaondoka wote hadi nje kabisa ya mji wa Iringa. Wakati mwingine tulikuwa tunaingiza gari porini na kufanyia mambo yetu garini na hii ilitupa raha zaidi. Tuliamua kufanya hivyo baada ya kubaini kwamba, kuingia gesti za pale mjini ilikuwa ni kujichongea bure.

  Ilisaidia kwani mwaka 1982 uliisha bila kero na 1983 ukafika hadi Juni, bila kusikia lolote. Lakini kama inavyosemwa, mkizini mtafumwa tu, hata iweje, ilitokea kwa aibu na fadhaa. Hiyo Juni, 1983 mume wa Waridi alipata safari ya kwenda Malawi kibiashara. Wiki hiyo mimi nilikuwa na safari ya kwenda Dar es Salaam. Tulikubaliana kwamba, tuondoke wote wakati mimi naenda Da es Salaam, tuje hadi Morogoro, tulale pale hadi kesho yake, mimi niendelee na safari naye arudi Iringa.

  Kwa bahati nzuri shule zilikuwa zimefungwa. Waridi alisema angemwambia mumewe akirudi kwamba, alikuwa ameenda Morogoro kumwona dada yake ambaye alikuwa ameumwa ghafla. Niliona ni wazo zuri. Ni kweli tuliondoka wote. Tulifika Morogoro na kupiga kambi. Waridi alikwenda kwa dada yake na kumwambia kwamba, amesikia kwamba anaumwa, hivyo amekuja kumwona. Ni kweli, alikuwa anaumwa kidogo wiki hiyo, lakini alikuwa na nafuu. Baada ya kuzungumza naye kwa muda wa saa mbili alimwaga kwamba anarudi Iringa.

  Alimsindikiza hadi stendi, ambapo mimi nilijitokeza na gari na kujifanya tunajuana na Waridi na kujifanya kwamba, natoka Dar es Salaam na ninaenda Iringa. Waridi alijifanya ananiomba lifti ambapo nilimkubalia. Dada yake alisema, "una bahati kweli, haki ya Mungu." Wenyewe tuliona tunafanya ujanja mkubwa sana. Tuliondoka hadi mzunguko wa Msamvu na kurudi mjini. Tulilalala Morogoro na asubuhi yake Waridi aligoma kurudi Iringa, akisema ni lazima afike na kulala Dar. Niliogopa kidogo, lakini nami wakati huo ilibilisi alikuwa amenikalia kichwani vibaya sana. Nilimkubalia. Tuliondoka Morogoro saa 1.45 asubuhi kuelekea Dar.

  Ilikuwa ni kama kilomita mbili tu kutoka Mlandizi, ndipo ilipotokea. Nilikuwa nimeshuka kilima kutokea mji wa Mlandizi na kupanda, halafu nikakanyaga mafuta hadi gari likawa linaenda kilomita 100 kwa saa. Nilisikia mlio mkubwa sana na gari iliyumba na nikanyangánywa usukani. Halafu niliona tukipaishwa na kutupwa kando ya njia kwenye mti wa mwembe.

  Upande alikuwa amekaa Waridi ukifikia kwenye shina la mwembe. Sikusikia tena kitu, wala kujua kilichotokea. Ni siku ya pili jioni niliposhtuka nikiwa Muhimbili. Nilimwona mke wangu akiwa kando ya kitanda changu pamoja na watumishi wa makao makuu ya idara niliyokuwa nafanyia. Nilihisi kama wepesi fulani huko chini. Nilipojikagua, niligundua kwamba, sikuwa na mguu wa kushoto. Nilihisi kama wepesi fulani huko chini. Nilipokaguia, niligundua kwamba, sikuwa na mguu wa kushoto. Ilinichukua muda kabla sijakumbuka kilichotokea. Polepole nilikumbuka kutoka Iringa, Morogoro bado Mlandizi. Sikukumbuka tena kitu. Ilinichukua muda kukumbuka ajali na kumkumbuka Waridi. Nisingeweza kumuuliza mke wangu au yeyote pale kuhusu Waridi, Lakini nilikuwa na uhakika kwamba , alikuwa amekufa.

  Nilianza kububujikwa na machozi. "Nilijaribu kusema, lakini sikuweza, ni midomo tu iliyokuwa ikicheza. Amekufa, amekufa, uso wangu sasa naupeleka wapi, nauweka wapi jamani..." Mke wangu alisema na kuangua kilio. Nilimwelewa. Wale watumishi wenzangu walimtuliza.`tuangalie na kujali hali ya mgonjwa kwanza,` walimwambia.

  Ni kweli, Waridi alikufa palepale kwenye tukio la ajali na mimi ni bahati tu kupona na kukatwa mguu mmoja badala ya miguu miwili na mikono. Nilikuwa na uhakika kwamba, makovu ya mwilini baada ya kupona yangekuwa yanatisha. Kila kitu kilifahamika baada ya siku ya tatu tu. Mume wa marehemu Waridi alirejea safarini na kusimuliwa kila kitu. Aliahidi mbele za watu kwamba, angenimaliza na mimi, iwe kwa mvua au jua. Nilipopata taarifa hizo nilicheka kwa sababu, niliona akifanya hivyo angekuwa amenitua mzigo mzito. Labda aliambiwa baadaye nilivyokuwa nasema, ndiyo maana hakunifanya lolote.

  Nilitoka hospitalini nikiwa na mguu mmoja baada ya miezi mitatu.Nilikuwa na nafuu kidogo. Mke wangu alishaanza uhusiano na yule mfanyabiashara na hakunificha. Ilibidi nifikie mahali niombe talaka. Talaka ilitolewa na kuwaacha waendelee. Hatimaye, mwaka 1985 walioana, ingawa ndoa yao ilivunjika mwaka 1990 kwa makeke na vurugu kubwa. Mimi nimepunguzwa kazi mwaka juzi na hivi sasa nina shughuli zangu. Nilikuja kuoa mwaka 1987, mke ambaye tunaelewana sana na amekuwa ndiye kiongozi wangu kwa mambo mengi. Tuna watoto wanne.

  ANGALIZO: Stori hii ni ya kweli, lakini hainihusu mimi Mtambuzi.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  ni stori nzuri inafaa kui edit na kuwauzia kina Kanumba,ila mpe pole huyo jamaa kwa yaliyomkuta.Nalog off
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Aisee!i una speed ya kusoma si mchezo! Duh!
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mtambuzi haya ndo mambo ulisema nifanyie kazi?? Ujue kua wanalifanyia kazi.... na nilifikisha ujumbe.


  B2T.... It's Great!!
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Natumia darubini mkuu,macho yenyeewe yashakufa.Nalog off
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana AshaDii. Kumbe ulikuwa hujanisahau? Kiherehere kimenifanya nianze na hii!
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Hakuna kilicho haribika lakini.... Usijali bana....lolz (I know how you love writting)
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nikashangazwa na speed yako.......lol. Vipi shangazi aliyemfananisha mkeo na bundi bado yupo au umemuhamishia hotelini?
   
 9. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hii story inasikitisha lakini ina mengi ya kujifunza maisha hayana formular moja ..........
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kumbe umeshanigundua eh!, hata sijui aliyeniroga ni nani....................!
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  story ni nzuri....japo inahuzunisha....lakini ni fundisho kwa wakware....
   
 12. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  duh,haiendelei tena jamani?
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  yaelekea ni nzuri ila ndefu sana..nimeshindwa kuimaliza..hebu mtu anisummarizie fasta fasta! nina hamu ya kujua contents
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Bonge ya movie, naomba hii iandaliwe movie iwe fundisho kwa watu kama sisi tunaopenda nyumba ndogo.
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Ni stori nzuri yenye maudhui ya ...Mla vya wenzake na vyake huliwa..........
   
 16. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Duh! Kweli mshahara wa dhambi ni kufa!
   
 17. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  kagoma kwenda hotelini,nimemuomba mke wangu aende akapumzike kwanza ili huyu shangazi atakapoondoka ndio nitamrudisha.Nalog off
   
 18. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  huu ni ukweli usiopingika.Nalog off
   
 19. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  nyumba ndogo ndio kila kitu.Nalog off
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mzee mwenzangu Rejao, unajua hii stori ilikuwa na kurasa nane! hapo nime-summarize sana
   
Loading...