Mgomo wa madereva leo tarehe 29/09/2026.

Mgomo wa madereva leo tarehe 29/09/2026.

Sasa kwanini wanawaumiza abiria wasio na kosa kwa sababu ya makosa ya traffic?

Au ndio kila mnyonge na mnyonge wake!
Waathirika zaidi ni abiria na wanalalamika sana kuhusu kucheleweshwa.

Majibu wanayopewa wanaambiwa wasubilie tu hadi maafikiano yatakapofikiwa ndo safari ianze.

Inauma lakini hakuna namna ya kufanya, nchi hii ina mambo mengi ya ajabu kwa sasa
 
Wanapitia manyanyaso sana na usumbufu usio na umuhimu barabarani dhidi ya trafiki

nilijua tu,

mtanzagiza ukimtaka afwate na kutii sheria atakwambia unamnyanyasa, hata ukisema kila mtu afike kazini muda kamili wa kuanza kazi uliowekwa kimkataba wa kazi watasema unawanyanyasa, yaani mambo ambayo jamii nyingine ni kawaida tanzagiza wanaita ni manyanyaso, wanatala waishi wanavyotaka wao.

bottomline: ni nadra sana trafiki akaaonea dereva br. tanzagiza ...
 
Sasa kwanini wanawaumiza abiria wasio na kosa kwa sababu ya makosa ya traffic?

Au ndio kila mnyonge na mnyonge wake!
Wape mbinu ili wasigome. Hadi wanafikia hatua hii ujue hatua zingine za ndani zimeshindikana na huenda madai yao yalipuuzwa kama ilivyo kawaida.

Hii huwa njia ya mwisho kufikisha ujumbe kwa haraka. Ukisema uwajali abiria wakati wewe unaumia ndiyo uzalendo?
 
Wape mbinu ili wasigome. Hadi wanafikia hatua hii ujue hatua zingine za ndani zimeshindikana na huenda madai yao yalipuuzwa kama ilivyo kawaida.

Hii huwa njia ya mwisho kufikisha ujumbe kwa haraka. Ukisema uwajali abiria wakati wewe unaumia ndiyo uzalendo?
Sasa kama dawa ni kumuumiza wa chini yako, siku abiria nao wakiamua kugoma kupanda magari yao ndio watapata akili.

Bajaji, boda, na private cars zinaweza kuwanyoosha hao madereva wajuaji.
 
Hii niliona, gari ni mali ya tajiri, dereva hana mkataba, unamkamata kwamba tire zimeisha, huku dereva alishamwambia tajiri lakini hakuna kilichofanyika, fine anapigwa dereva, point zinakatwa kwenye leseni ya dereva na sio leseni ya gari, hata kama ni mimi nagoma. Mfumo wa point kwa Tanzania tumekurupuka, mfumo wa point unafaa nchi ambazo compliance ipo juu mfano tajiri anajua na kuelewa gari haipaswi kutoka ikiwa mbovu lakini pia, pasipo na rushwa, uonevu na matabaka tunayoyaona barabarani jinsi watu wenye mamlaka wanapojieka juu ya sheria yani kwamba wao wenyewe wanajua hivi vitu kutekelezeka ni mgogoro.
 
nilijua tu, mtanzagiza ukimwambia afwate sheria atakwambia unamnyanyasa, hata ukisema kila mtu afike kzini muda wa kazi kamili watasem unawanyanyasa, yaani mambo ambayo jamii zilioendelea ni kawaida tanzagiza wanaita ni manyanyaso, wanatala waishi wanvyotaka wao.

bottomline: ni nadra sana trafiki anaonea derve tanzagiza ...
Umeona hapo kwenye manyanyaso tu akili ikagomea hapo?

Hujaona usumbufu ysio wa lazima barabarani mfano dereva kulazimika kusimama muda mrefu ili tu atoe rushwa hata kama gari haina kosa?

Ungekuwa japo hata na Bajaj tu ungejua kwanini madereva wanafikia hatua ya kugoma.

Usumbufu ni mwingi mno ili mradi tu utoe kitu kidogo. Anasimamisha gari halafu haendi kuikagua anasubiri dereva amfuate ili wamalizane.
 
Back
Top Bottom