Mgomo utapita kama ilivyopita mingine, na huu sio wa kwanza wala wa mwisho.
Rafiki,
naona unashadadia as if ni kitu kizuri sanaaaaaa.
ni mambo matatu
1. kwa serikali
act faster kwa hicho mlichojipanga(stmt from Mh. Pinda)
ushauri
-tangaza nafasi za udaktari ndani na nje ya TZ.
-privatised medical sector
2. kwa madaktari
-rudini kazini
-kwa wale wanaogoma tu kwa shinikizo la wengine be careful ulisoma peke yako na ukakaribia na kua daktari kama ww
speak out then serikal ikusaidie si kwa njia ya kusababisha mauaji/hofu kwa wagonjwa
-ninyi ambao mna channels kwenye ma NGO halafu mnawachuza wenzenu M/Mungu atawalipizia humu humu dunian, kwan hata mkifukuzwa tayari mna kazi sehem nyingine
3. wananchi
-mgomo wa madaktar unaweza kua ni sahihi ila tutazame kwa kina jamaa wamekosea,maombi yao mengi ni nadhalia zaid kuliko uhalisia na iwapo wakitimiziwa haya next watakuja na complicated things na pia je kuna halufu ya kuchochowa!!!
JJK akipeana mkono na Dr. DUX, katikati karibu na Dux ndo Dr. Ulimboka kwa msiomjua.
Nyuma ya JK anayesmile ni Rais wa MAT Dr. Namala Mkopi
Ndugu yangu si kweli mgomo huu utapita bure, mgomo huu unapita na roho za watanzania maskini. Migomo mingine kweli ilipita, kwa kuwa kama shule zilifungwa kisha zikafunguliwa na watoto wakaendelea na masomo, vituo vya dala dala na vya treni vilifungwa kisha vilifunguliwa na abiria wakaendelea na safari zao. Lakini mtu aliyepatwa na mstuko wa moyo (Cardiac Arrest) na kukosa huduma ya daktari, hawezi kuamka tena na ndo maana leo Mhe. Rais amekutana na viongozi wa madaktari kuangalia jinsi gani ya kumaliza mgomo huu. Natumaini Mhe. Rais atatumia busara tena, kama kwenye Mswada wa Katiba mpya.
Mungu ibariki Tanzani.
JJK akipeana mkono na Dr. DUX, katikati karibu na Dux ndo Dr. Ulimboka kwa msiomjua.
Nyuma ya JK anayesmile ni Rais wa MAT Dr. Namala Mkopi
Acha wafe kabisa, na wafe kweli hata kama mie nikifa acha nife lakini najua kwa hili mtanzania atakuwa kaniua. Hakuna kuilaumu serikali wala ma-dr. Watanzania wenyewe mmeiweka serikali madarakani. Upumbavu wenu acha uwagharimu. Mtu anasema chagua ccm chagua chama cha nyerere. What a hel r u thnkng? Kufa, kufa kabisa. Na inflation acha ifike 100%. Unga, petrol na umeme vipande bei zaidi ili mjue kuwa mliweka madarakani matapishi yenu. Can u imagine, awamu ya 2 imechukua sukari tsh.450/= imetuachia sukari tsh.650/=. Awamu ya 3 imechukua tsh. 650/= miaka 6.5 sukari ni 2200+ bado 2015 hatujafka. Nyie mnailaumu serikali. JILAUMUNI WENYEWE NA UJINGA WENU WA KUFIKIRI km 2 ahead wenzenu wanafkiri km 1000 ahead.
Kama hutaki kurudi meza ya mazungumzo hadi waziri ajiuzulu, ina maana unataka mazungumzo bila waziri (common sense ni kwamba waziri hafanyi maamuzi binafsi, kuna kanuni, taratibu na maelezo mengine ambayo inabidi ayafuate wakati anafanya kazi- na hii inaaply kwa mfanyakazi mwingine yeyote). Kwa hiyo basi, Waziri akijiuzulu, au akaondolewa kwenye nafasi hiyo na Rais, basi lazima hiyo nafasi izibwe na waziri mwingine - ambaye atafanya kazi kwa kanuni, taratibu, sheria na maelekezo yale yale ambayo waziri msiyemtaka amekuwa akifanya kazi kwayo. Kumkataa waziri sio suluhisho la matatizo yeni, na hilo mnalijua fika.
Impliation ya madai ya kuondolewa waziri ili mkae meza ya mazungumzo ni kuwa hamtaki kuongozwa, mnataka mjiongoze ili mhakikishe mnapata vifaa, mazingira, posho, mishahara na stahiki zenu kadri mnavyopenda na mnavyoona inawasuit. Ingekuwa vinginevyo mngerudi meza ya mazungumzo (unless matakwa yenu mnayalazimisha kama vile sekta ya afya ndo muhimu kuliko sekta ya elimu, maji, kilimo nk ambao mnadhani wao hawana matakwa kama mliyonayo).
Wananchi malimbukeni kama mimi tunaona haina haja ya kuwa na madaktari wanaotaka kuua kwa maslahi yao binafsi badala ya kufa wao kwa ajili ya maslahi ya wengi. Mnastahili kuwajibishwa na nadhani mwenye mamlaka anachelewa sana kuwawajibisha.
Hoja zako hazina nguvu. Wanachi wamekwisha kutimizia wajibu wao kwa kukusomesha kupitia kodi zao. Bila wananchi kutimiza wajibu huo usingekuwa hapo ulipo. Unapaswa kushukuru kwa hilo kwanza. Kwa upande wa serikali, kama kuna mahali seikali yako haikukufanyia vizuri haikuhalalishii wewe kufanya kosa. Makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sahihi. Usijenge hoja kwa kuiga kosa la mtu mwingine.
Jambo muhimu kwa pande zote kujua kanuni za majadaliano ( negotiations) Majadiliano yaweza kuwa '' hardball'' ya ushindani au '' corperative' akushirikiana. Hardball hutumika kama watu wanaojadiliana hawatahusiana kwa mara nyingine na corperative kwa wale ambao mahusiano yao niendelevu
Uhusiano wa madaktari na Serikali ni endelevu hivyo majadilino yanayofaa ni ya kushirikina ili kutatua tatizo lililopo.
Jambo lingine muhimu ni matumizi ya nguvu (powers) ambazo pande zote zinazo na jinsi ya kuzitumia. Matumizi mabaya ya nguvu yanaweza kuchelewesha kufikia mwafaka au kuharibu kabisa mwenenendo mzima wa majadiliano. soma zaidi http://web.cba.neu.edu. Madaktari na serikali kwa wakti tofauti mmetumia vitisho jambo limetufikisha hapa.
Madai ya msingi ya madaktari ni halali kabisaa.
- Ukosefu wa vitendea kazi
- Mazingira magumu ya kazi (na ya kujifunza - kwa Ma-Interns)
- Mishahara/posho ndogo
Tatizo la madaktari waliopo mafunzoni kutolipwa posho zao lilikuwa uzembe wa watendaji wakuu wa wizara ya afya, ambao tayari wameshawajibishwa (Katibu Mkuu - Mama Blandina Nyoni na Mganga Mkuu - Dr Deo Mtasiwa). Baada ya hapo serikali ilikubali kuwa na mazungumzo na madaktari kuhusu matatizo mengine yaliyotolewa na madaktari; vikao kadhaa tayari vimefanyika na bado mazungumzo yalikuwa hayajasitishwa.
Suala la MAT kudai kuwa viongozi wa kisiasa wa wizara wafukuzwe au wajiuzulu, vinginevyo madaktari wataendelea na mgomo ni dhana ambayo haikufanyiwa "homework" vizuri.
- Wizara ya afya siyo kwa ajili ya madaktari tu (Kuna madaktari (MD), Manesi, Wafamasia, Wataalamu wa maabara, wataalamu wa mama cheza (physiotherapists), Optometrists na wengine wengi tu. Sijui kama madai ya kutaka Waziri na Naibu wake wafukuzwe ni madai yanayowakilisha taaluma nyingine za tiba!
- Waziri na Naibu wake ni viongozi wa kisiasa kwenye wizara; kwa maana nyingine ni wawakilishi wa Rais kwenye wizara, na jukumu lao kubwa ni kusimamia utekelezaji wa sera SIYO UTENDAJI. CEO wa wizara ni Katibu Mkuu.Kudai mawaziri hawa wafukuzwe ni kumwamuru Rais afanye mabadiliko ya Cabinet!
- MAT siyo chama cha kutetea "Labour related issues" za madaktari. MAT ni NGO kama ilivyoainishwa kwenye tovuti yao kuwa
- Hili suala la mawaziri mbona halikuwa kwenye madai ya mwanzo?
- Duniani kote kuna taratibu za kuitisha migomo, ikiwa ni pamoja na kutoa notice ya siku kadhaa (siyo siku 4) na kuhusisha "trade union" inayowakilisha wafanyakazi hao. Je, MAT walifanya hivyo?
Ombi langu kwa madaktari wanaogoma: Jamani mwogopeni Mungu; waoneeni huruma maskini wagonjwa. madai yenu ya msingi ni halali kabisaa, lakini hili la mawaziri liangalieni upya. Rejeeni kwenye mazungumzo na serikali.
Hajafanya hivo makusudi.Hivi JK anapotoa mkono kwa hawa madaktari wakati mkono wake uko mfukoni ana maana gani?? Pamoja na kwamba yeye ni Rais, hii kwa kiasi fulani ni dharau kwa mtu unayemsalimia.
Madaktari hawajamzuia profesheno yeyote kufanya analoliona kuwa ni sahihi,Wakuu hapo juu.......asanteni sana kwa mawazo mazuri.......
......madai ya madaktari kuhusu mazingira ya kazi ni ya msingi na yashughulikiwe tena nasema URGENTLY.....lakini madai ya eti Mawaziri wajiuzulu kwa kuwa wao ndio vikwazo.......narudia.....ni UKILAZA USIO NA KIFANI.......utafikri mijitu haifikirii au haijaenda shule.......
Yaani madaktari wanataka kutuchagulia Mawaziri..............halafu siku nyingine wahandisi wagome kwa kuwa Magufuli anakwamisha matakwa yao ya msingi..........halafu....wanasheria nao.......waje wagome wadai hawamtaki Celina.......halafu siku nyingine wanajeshi nao wagome waseme hawamtaki Dr. Hussein........THIS IS ABSOLUTE RIDICULOUS......
Nimekufuatilia sana hoja zako. Ni nzuri ila zina ukomo wa fikra. Ulivyomalizia angalau ungetoa ukweli wa 'kosa kuingiza, kuingia au kuingizwa kwenye siasa na kusahau wajibu wenu" kwa kutaja bayana mazingira yaliyosababisha tukio hilo.Mtawakomboaje watanzania kwa kutomtaka waziri? unadhani shida kubwa ya watanzania ni afya?
Assume waziri kajiuzulu na madai yenu yote mmetimiziwa kesho, je mnaweza tibu wagonjwa bila umeme, maji etc?
Mmefanya kosa kuingiza, kuingia au kuingizwa kwenye siasa na kusahau wajibu wenu.
Madaktari hawajamzuia profesheno yeyote kufanya analoliona kuwa ni sahihi,
kama ni hivo basi wahandisi na waige.
Kama hutaki kurudi meza ya mazungumzo hadi waziri ajiuzulu, ina maana unataka mazungumzo bila waziri (common sense ni kwamba waziri hafanyi maamuzi binafsi, kuna kanuni, taratibu na maelezo mengine ambayo inabidi ayafuate wakati anafanya kazi- na hii inaaply kwa mfanyakazi mwingine yeyote). Kwa hiyo basi, Waziri akijiuzulu, au akaondolewa kwenye nafasi hiyo na Rais, basi lazima hiyo nafasi izibwe na waziri mwingine - ambaye atafanya kazi kwa kanuni, taratibu, sheria na maelekezo yale yale ambayo waziri msiyemtaka amekuwa akifanya kazi kwayo. Kumkataa waziri sio suluhisho la matatizo yeni, na hilo mnalijua fika.
Impliation ya madai ya kuondolewa waziri ili mkae meza ya mazungumzo ni kuwa hamtaki kuongozwa, mnataka mjiongoze ili mhakikishe mnapata vifaa, mazingira, posho, mishahara na stahiki zenu kadri mnavyopenda na mnavyoona inawasuit. Ingekuwa vinginevyo mngerudi meza ya mazungumzo (unless matakwa yenu mnayalazimisha kama vile sekta ya afya ndo muhimu kuliko sekta ya elimu, maji, kilimo nk ambao mnadhani wao hawana matakwa kama mliyonayo).
Wananchi malimbukeni kama mimi tunaona haina haja ya kuwa na madaktari wanaotaka kuua kwa maslahi yao binafsi badala ya kufa wao kwa ajili ya maslahi ya wengi. Mnastahili kuwajibishwa na nadhani mwenye mamlaka anachelewa sana kuwawajibisha.