Mgomo mkubwa kuhusu pensheni waathiri usafiri Ufaransa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Ufaransa imeathiriwa na mgomo mkubwa ambao unafanyika leo wa wafanyakazi katika sekta ya usafiri wa umma. Treni nyingi hazifanyi kazi, shule zimefungwa na wasimamizi wa mnara wa Eiffel wametoa onyo kwa wageni kutozuru eneo hilo; kufuatia maandamano na mgomo dhidi ya mpango wa serikali kuufanyia mageuzi mfumo wa kustaafu na malipo ya pensheni.

Maafisa wa polisi 6,000 wamepelekwa katika maeneo mbalimbali kushika doria, kukabili kile kinachotizamiwa kuwa yatakuwa maandamano makubwa katika mji mkuu Paris, huku vituo viNgi vya treni vikiwa vimefungwa. Wafanya kazi wa umma wanahofia kuwa mpango wa mageuzi hayo ya Rais Emmanuel Macron, utawalazimisha kufanya kazi kwa saa nyingi na kupunguza pensheni zao.

Waziri wa uchukuzi amesema atakutana na vyama vya wafanyakazi leo kujaribu kuondoa wasiwasi. Mamlaka inayosimamia usafiri wa treni SNCF imesema safari za takriban treni 9 kati ya 10 za mwendo kasi zimesitishwa. Aidha asilimia 30 ya safari za ndege za ndani nchini humo pia zimesitishwa kufuatia mgomo huo.
 
Back
Top Bottom