Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Majaji wote 7 ni Watanzania wakiongozwa Jaji Mkuu mwenyewe. Wengine ni akina Mama Munuo, Stephen Bwana,....Hili ni suala linalogusa moja kwa moja KATIBA yetu. Hukumu yake itafungua mengi tu mabovu yaliyomo kwenye KATIBA hii ambayo kuiandika upya imeshindikana.

Hofu yangu ni moja. Wakiruhusu mgombea binafsi hata kwenye ngazi ya URAIS si ajabu akina RA, EL, Mtikila, Mengi, Butiku, Bakhresa, Raza, Juma Nature, Ben Kinyaiya, Dr Cheni, Zamoyoni Mogela, mimi,....tukachukua fomu ya kugombea!?
 
Asante malafyale nimekiona hicho kifungu cha 21(i) kweli kinapingana na vifungu 5 39 na 67 nilivyovinukuu awali nafikiri hukumu ya jaji Lugakingira ili-base hapa basi Mtikila ana uwezekano mkubwa wa kushinda katika hukumu yeyote ikitokea katiba inajichanganya basi majaji wanao uwezo wa ku-favour upande wowote.

Bunge la CCM tupu la mwaka 1992 lilikuwa ni bunge butu labda kupata kutokea ktk historia ya tz;badala ya kufuata sheria wao walivunja na kuamua kuishughulikia hukumu ya jaji Lugakingira bila kukata rufaa!

Vifungu hivi kama ili kupigiwa kura unahitaji udhamini wa chama cha Siasa uliingizwa baada ya hukumu hiyo,kabla ya hapo katiba mama ilisema tu wazi kuwa kila mtu anastahili kupiga na kupigiwa kura!na hata majaji kwenye kesi marudio ya mwaka 2005 walifata katiba mama ilisemaje kabla ya kuingizwa madudu kwa matakwa ya bunge la mwaka 1992

Msekwa,Malecela,Mrema,JK,Kingunge,Makweta,Mwinyi,Mkapa,Warioba,jaji Lubuva na wengine wengi wote waliasisi mpango huu ambao sasa baadhi yao kama akina Mrema na baadae Lumuli Kasyupa waliokuja upinzani wanaona hata aibu kusema lolote!
 
GS, usiwe na shaka; mwaka huu wagombea binafsi wataruhusiwa. Tatizo langu ni kuwa watawala wanaweza kuchelea kulitekeleza hilo.

Re: Majaji saba kuamua suala la mgombe binafsi

Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani, Jaji Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathania Kimaro, Mbarouk Salim, Dk. Stephen Bwana na Benard Ruanda.

......eeeerh... further postmortem is needed!
 
The Tanzanian constitution is unconstitutional.

Inatoa haki kwamkono mmoja na kuiiba kwa mkono wa pili.

We have to remove this inconsistency before a politically fueled constitutional crisis ensues.
 
The Tanzanian constitution is unconstitutional.

Inatoa haki kwamkono mmoja na kuiiba kwa mkono wa pili.

as a matter of fact.. ndiyo sababu ya Mahakama kukataa nyongeza yao ile. Hoja ya Mahakama ni kuwa huwezi kubadili vipengele vya Katiba vikapingana na Haki za Msingi (Bill of rights), ukifanya hivyo, Bill of Rights inasimama peke yake na nyongeza yako inavunjwa. Wenyewe wanasema kutumia Katiba kuipinga Katiba.
 
kama kuna uwezekano hao majaji wasiwe watanzania!!!

Mkuu unasahu kuwa moja ya sababu za kuifanya TAnzania iwe jamhuri ilikuwa ni kukwepa jambo hilo, ili haki ya individuals isijekupewa kipaumbele kwenye privy council. Kwa hiyo hilo katika halia ya kawaida haliwezekani. Unless tubadilishe katiba.
 
Hii kesi kama ingesikilizwa wakati Barnabas Samatta akiwa judge mkuu ningekuwa na imani lakini sasa hivi huyu kada wa CCM Augustine Ramadhani na majority ya majudge wakiwa wateule wa Jakaya naona kabisa kuwa CCM itatetewa na mgombea binafsi itakuwa ndoto!

Ingekuwa enzi ya majudge wenye msimamamo na uzalendo thabiti kama wakina Mwalusanya na Lugakingira pengine ningekuwa na matumaini!! Much as I would like to see private candidates contest the coming elections, I am pessimistic that they will not be allowed given the pro CCM composition of the constituted court!!
 
Hoja ni ya msingi....si lazima kila mtu awe mwanachama wa chama cha siasa. Kwa mantiki hiyo hiyo si lazima ili uwe mwanachama wa chama cha siasa ili uwe kiongozi. Kuna mkanganyiko katika katiba....Mtikila anaonyesha jinsi alivyobobea katika masuala ya sheria.
 
Hivi naomba kuuliza kwa washabiki wa hii proposal ya mgombea binafsi. In general mgombea binafsi atasaidia vipi katika jamii au hata fanya kitu gani ambao especially wabunge wa sasa hawafanyi? Na vile vile ni kitu gani kinachomfanya asigombee kupitia chama?.

Bila kujali atafanya nini, haki hii ipo kwenye katiba na haiwezi kuondolewa kienyeji tu. Haijalishi kama atasaidia au hatasaidia ni haki ipo lazima watanzania tuifaidi.

Kwa mfano haki ya kuishi ipo, lakini watanzania mamia wanaishi maisha ya tabu saaana una maana tuombe bunge liondoew haki ya kuishi simply because haki hiyo haisaidii kitu????

Suala ni principle so long as it is there it has to be exercised.
 
Mzee Mwanakijiji,
Excellent analysis.

Pamoja na kuwa wengi wanaosema kesi ni ngumu pia wako sahihi, lakini kikubwa kinachojodhihirisha katika kesi hii ni Katiba kujitatanisha yenyewe. Katika baadhi ya vifungu inatoa fursa na haki kuwa kila mtu anayostahili ya kuchaguliwa na kuchagua na vifungu vingine inaweka pingamizi la kuchaguliwa.

Kwa wakati huo huo, Katiba inaweka misingi yake kuwa binadamu wote ni sawa na wanastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wao. Kama kuwa kwenye chama kunamtambua binadamu zaidi ya kutokuwa kwenye chama, msingi huu ambao ni muhimu zaidi kwenye Katiba ya nchi una maana gani?

Ndio maana huwa nasema mara nyingi (kwa imani kabisa), kwamba Katiba yetu haiwezi kutusaidia kabisa kurekebisha hali ya kisiasa, kijamii na wala kutuhakikishia uongozi bora. Inahitajika Katiba ambayo inaainisha mambo yote bila kujifinyanga katika vifungu vingine.

Naelewa kuwa Katiba ilibadilishwa haraka haraka ili kuruhusu uwepo wa vyama vingi, na bila kujali nafasi ya vyama hivyo katika uongozi wa nchi. Kwa maana nyingine, watawala hawakutegemea kuwa vyama vya upinzani vitawahi kukuwa na kupata support kubwa kutoka kwa wananchi. Walidanganyika na 20% ya waliounga mkono mfumo wa vyama vingi. Wakidhani hali itabaki kama ilivyo.

Hakuna kinachoweza kuzuia mahitaji ya wananchi kupata viongozi wasiofungamana na vyama vya siasa. Tatizo ninaloliona ni kuwa, watakaotakiwa kupitisha mabadiliko ya vifungu hivyo vya Katiba, ni wawakilishi wa vyama ambao sina uhakika sana kama wako tayari kuwa na wapinzani huru ndani ya Bunge.
 
Mimi naona Srikali imeshashinda. Hata kama Mahakama ikitupilia mbali rufaa ya serikali, itabidi itungwe sheria ili kuruhusu mgombea binafsi na serikali itahakikisha sheria inachelwa mpaka uchaguzi 2010 upite. Kwa maana hiyo tutasubiri hadi 2015! Sijawahi kuona Chama kioga kama CCM!
 
MAHAKAMA ya Rufani Tanzania imetoa angalizo kwamba uamuzi wa Makamama Kuu uliotolewa kuhusu mgombea binafsi kusimama katika uchaguzi mkuu uko pale pale, ingawa umekatiwa rufaa.

Angalizo hilo lilitolewa jana na majaji saba wanaosikiliza rufani inayopinga uamuzi uliotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu; Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, ambao walikubaliana na ombi la Mchungaji Christopher Mtikila na kuruhusu kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi.

Majaji hao walitoa angalizo hilo baada ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kuomba mahakama iahirishe usikilizwaji wa rufani hiyo na impe miezi minne apitie jalada kwa kuwa hajajiandaa na pia mwanasheria mwenzake anauguliwa na baba yake, hivyo hajapata muda wa kutosha, ombi ambalo lilipingwa na walalamikiwa ambao ni mawakili wa Mtikila, wakidai wiki moja itatosha.

Masaju pia alihoji kuwapo majaji saba katika rufaa hiyo badala ya watatu kwa mujibu wa ibara ya 122 ya Katiba.

Hata hivyo, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, alihoji ni wakati gani jopo kama hilo huwa linakaa na kusema kama ni makosa, basi yalishafanyika tangu mwaka 1984 ambapo jopo la namna hiyo lililohusisha majaji watano lilitumika Zanzibar.

Alisema aliamua kuunda jopo hilo kulingana na unyeti wa suala lililoko mbele yao. Baada ya kutoa ufafanuzi huo, rufani hiyo iliahirishwa hadi Aprili 8 mwaka huu.

Rufaa hiyo iliyofunguliwa na Jamhuri namba 45 ya mwaka jana inasikilizwa na majaji wakiongozwa na Jaji Mkuu, Ramadhani. Wengine ni Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathania Kimaro, Mbarouk Salim, Bernard Luanda and Sauda Mjasiri.

Katika rufaa hiyo, Serikali imetoa sababu sita za kukata rufaa, mojawapo ikidai Mahakama Kuu ilikosea kujipa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, ilikosea kutengua vifungu vya Katiba ya nchi, na ilikosea kisheria kupunguza matakwa ya lazima ya Ibara 30 (5) na 13 (2) ya Katiba ya nchi.

Sababu nyingine, ni kujipachika mamlaka ya Bunge ya kutunga sheria, kukosea kisheria kwa kuiweka Katiba ya nchi katika vyombo vya kimataifa na kuitolea uamuzi kesi hiyo bila kuweka suala hilo bayana.

Hukumu ya Mahakama Kuu juu ya kesi iliyofunguliwa na Mtikila ilitolewa Mei 2006, ikiruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu Katiba ya nchi inatoa haki hiyo.

Mahakama Kuu ilibainisha kuwa Katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani.

Awali Mchungaji Mtikila alifungua kesi hiyo ya kikatiba mwaka 1993 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Jaji Kahwa Lugakingira (marehemu), alikubaliana na hoja za Mtikila na kuitaka serikali kuruhusu wagombea binafsi.

Baada ya serikali kuwasilisha rufani hiyo iliyotakiwa kuanza kusikilizwa jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, alisema msingi wa rufaa ya Serikali si kupinga mgombea binafsi, bali ni kuiuliza Mahakama ilikopata mamlaka ya kufuta vifungu vya Katiba ya nchi, kama ilivyofanywa na Mahakama Kuu katika uamuzi wa kuruhusu mgombea binafsi.

Alisema msingi wa serikali kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, unatokana na Ibara ya 98 ya Katiba ya nchi, ambayo imelipa Bunge peke yake mamlaka ya kubadili Katiba ya nchi na kwa kufuata mchakato maalumu na kwamba, ibara hiyo haitaji mahali popote mahakama kupewa uwezo huo.

Katika uamuzi wa Mahakama Kuu, iliamriwa kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ifanye marekebisho ya Sheria Namba 34 ya 1994 ambayo inapingana na kifungu cha 21 (1) cha Katiba ambacho kinampa haki ya mtu kugombea na kupiga kura.

Mahakama Kuu ilimpa Mwanasheria Mkuu kati ya Mei 5, 2006 hadi uchaguzi ujao, awe amewasilisha bungeni sheria inayotoa fursa ya kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi bila kutegemea chama chochote
 
hawa majaji ni fake tu.do you think wako independent?
wanakulala pesa ya uchaguzi tu na taxpayers.
hakuna mantiki hapa kama mtu anataka kugombea bila ya chama cha kifisadi ,ruksa.
 
mmakonde;kaandika
"hawa majaji ni fake tu.do you think wako independent?
wanakulala pesa ya uchaguzi tu na taxpayers.
hakuna mantiki hapa kama mtu anataka kugombea bila ya chama cha kifisadi ,ruksa."

Malafyale kaandika

Mmakond,hawa majaji sio fake na kwa kweli sijajua umetumia kigezo gani kusema hivyo,

Kwenye kesi ya misingi iliyosiklzwa jana majaji hawa 7 wameitosa serikali na kumpa ushindi wa muda Mtikila kwani wametamka wazi kuwa maamuzi ya mahakama ya kesi iliyopita yanabaki pale pale;kumbuka Mtikila alishinda kesi hiyo na kutangazwa rasmi kisheria kuwa wagombea binafsi ni ruxa!

Soma hapa chini kwa mujibu wa mwana JF Luten

"MAHAKAMA ya Rufani Tanzania imetoa angalizo kwamba uamuzi wa Makamama Kuu uliotolewa kuhusu mgombea binafsi kusimama katika uchaguzi mkuu uko pale pale, ingawa umekatiwa rufaa.

Angalizo hilo lilitolewa jana na majaji saba wanaosikiliza rufani inayopinga uamuzi uliotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu; Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, ambao walikubaliana na ombi la Mchungaji Christopher Mtikila na kuruhusu kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi"


Andiko la Malafyale

Kesi hii hadi sasa inatuendea vyema sisi wapenda mabadiliko na tuzidi "keep our fingers crossing"zaidi ili kwenye kesi ya msingi hiyo mwezi April maamuzi yawe kwa manufaa ya demorasia kama walivyoamua jana!

Yes we can,na likely mgombea binafsi TZ atapatikana na kupunguza nguvu ya Kamati Kuu ya vyama vya siasa ya hasa mizengwe ya kuteua wagombea maana sasa watajua kuwa ukikata jina la mgombea chaguo la wengi basi atakwenda kugombea kama mtu huru asiye na chama!
 
Malafyale,

Mkuu huko Bungeni nako kutakuwa na uhuru wa maoni zaidi. Sasa hivi wasomi na elimu zao wanafanya mambo ya ajabu sababu ya kuogopa rungu la chama.
 
JF,
Mimi si Mchumi wala Mwanasiasa, ila jana na leo nimesikia kwamba mgombea binafsi anaruhusiwa mpaka hapo rufaa waliyokata wenzetu wa serikali itakaposhinda katika mahakama kuu ya rufani.

Sipendi kuwahi kuleta kitu ambacho hakijaiva au kukatiwa shauri kabisa ila tunaweza kupanuana mawazo juu ya jambo hili ili likiwa tayari next few months basi na sisi tuwe tayari.

Sasa inavyoonekana kuna uwezekano mkubwa wagombea binafsi wakaruhusiwa sababu katiba ya Jamhuri yetu imeeleza wazi kwamba kila mwananchi wa taifa hili anaweza kugombea ngazi yoyote ya uongozi wa taifa letu ilimradi asivunje sheria.

Sasa swali la msingi wa wachambuzi wa mambo ya kijamii na kisiasa

Je hii itatusaidia kukuza demokrasia ya kweli katika nchi yetu, na kupunguza ufisadi? ni yapi mema basi tuyasubirie endapo shauri hili likipita rasmi na zoezi likafanyika katika uchaguzi ujao? 2010

Binafsi nalipokea kwa shauku sana - ili kama mtanzania mwenzetu anakubalika katika jamii na hayupo katika kundi lolote la chama cha siasa - basi naye awe na nafasi ya kuongoza taifa lake endapo wananchi watamchagua.
 
swala la mgombea binafsi lina pande mbili,
pande ya kwanza itatoa uhuru mkubwa kwa wananchi kwa ujumla na kuwapa haki yao ya msingi kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa, na pindi kiongozi anaposhinda uongozi kwa ugombea binafsi anakuwa hana kanunu zinazombana zaidi ya kanuni za chombo husika na sheria za nchi kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kukuza demokrasia.

pande ya pili ni kutokana na jamii kubwa ya kitanzania kuwa masikini basi kunaweza kutokea na mfumo wa kuajiriwa kwa maslahi ya mabwanyenye.

yani bwanyenye anaweza kumpa mwananchi wa kawaida fedha za kampeni ili tu akamwakilishe yeye, huu ni sawa na utumwa, na pia inaweza ikawa ni nafasi ya matajiri kuingia kwenye uongozi.

so ugombea binafsi unaweza kukuza demokrasia au kudumaza.
 
Back
Top Bottom