Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Baada ya kuona sakata la baadhi ya wanaCCM kutaka kumeguka na kuanzisha chama kipya serikali imekuja na mbinu nyingine ya kutuliza hali ya hewa ndani ya chama tawala

Ina maana na 'mgombe' binafsi pia? Yumo kwenye Chama?

Hilo lawezekana lakini sioni ni vipi hasa
 
- Kumbe yule waziri was right, hakuna hiyo sheria ndio maana aliniambia hii kesi imechukua muda mrefu sana kusemwa ni kwa sababu majaji walijua wamechemsha!

Respect.

FMES!
 
Field Marshall ES,
Sikubaliani na wewe kuwa waziri Chikawe alipatia kwenye suala hili la wagombea huru kwani katiba yetu ndiyo inajichanganya kuhusu suala hili hasa baada ya ammendments iliyofanywa baada ya hukumu ya Jaji Lugakingira mwaka 1992 iliyoiumbua serikali kuu!

Ina maana majaji wote 4 walichemsha?kuanzia mwaka 1992 Jaji Lugakingira aliposema ni haki ya kila mtz kuamua kugombea bila kuwa na chama hadi majaji akina Manento mwaka 2005 waliposema hivyo hivyo?What coincidence was that jamani?

Ona mkanganyiko wa katiba yetu hapa chini mkuu FMES;unaompa haki kila mtz nafasi ya kupiga na kupigiwa kura bila kusema wazi kuwa anahitaji awe mwanachama wa chama cha siasa

(nanukuru toka JF)

"Vifungu hivyo ni namba 21(i) kinachosema kwamba bila kuathiri masharti ya Ibara ya 5, 39 na 67 ya katiba na sheria za nchi kuhusina na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi"

"Mtu huyo anaweza kushiriki moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao au kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria"

Sasa ona tena sehemu hii ya katiba iliyofanyiwa marekebisho na Bunge hasa baada ya hukumu ya jaji Lugakingira mwaka 1992

(Nanukuru toka JF)

"Pia kifungu namba 39 (1) kinachosema kwamba mtu hastahili kuchaguliwa kushika kiti cha rais wa Jamhuri ua Muungano isipokuwa ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa"

Kwa maoni yangu binafsi,kugombea bila kuhusicha chama ni haki ya msingi ya kila MTZ na hauhusiani hata kidogo na party affiliation na kwa maoni yangu serikali kukatia rufaa jambo kama hili ni kuchezea hela zetu walipa kodi.
 
kama kuna uwezekano hao majaji wasiwe watanzania!!!


Ukiondoa mahakama za chini ambako kuna rough za hapa na pale za kirushwa rushwa, kwa sheria za Africa, Mahakama kuu na ya Rufaa Tanzania ni moja ya vyombo sheria ambavyo viko free and fair kabisa. No doubts about it. Tusubiri na kitakachotoka ndicho hicho hicho.
 
Mahakama ya Rufaa itakubaliana na hoja za Mtikila na serikali itashindwa. Haina hoja.

Naomba niulize (ili kuonesha kwanini serikali itashindwa) = Je ni nani ana haki ya kupiga kura Tanzania?
 
Mahakama ya Rufaa itakubaliana na hoja za Mtikila na serikali itashindwa. Haina hoja.

Naomba niulize (ili kuonesha kwanini serikali itashindwa) = Je ni nani ana haki ya kupiga kura Tanzania?

Jibu kwa Mwanakijiji

Mtu yeyoye aliyethibitishwa kuwa ni mtz;mwenye akili timamu; aliyefikisha miaka 18 na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na siku ya uchaguzi awe uraiani(ukiwa jela au mahabusu hupigi kura)unaruhisiwa kuchagua kiongozi amtakaye kwenye chaguzi yeyote nchini tz.

Nyongeza yangu binafsi bila kuhusisha jibu la Mwanakijiji

Lkn sheria hiyohiyo ya uchaguzi inambagua mtz akitaka "apigiwe kura" na kumlazimisha lzm apitishwe na chama cha siasa ndipo eti apate nafasi ya kupigiwa kura

Kama tu ulivyokuwa uamuzi wa Jaji Lugakingira na akina majaji Manento;nami pia naungana na Mwanakijiji naliona anguko la JK na serikali yake kwenye kesi hiyo!
 
Malafyale,

Malafyale.. you got my point pretty good na sidhani kama itawachukua majaji muda mrefu kuweza kuona hilo.

a. Kama Mtanzania aliye raia, aliyeandikishwa katika kitabu cha kupiga kura na ana akili timamu ana haki ya kupiga kura kumchagua mtu yeyote yule bila ya kulazimishwa kuwa kwenye chama cha siasa, inakuwaje Mtanzania huyo huyo mwenye uwezo wa kumchagua mtu mwingine (hata kujipigia kura yeye mwenyewe) asiwe na haki ya kuchaguliwa bila kulazimishwa kuwa katika chama?

b. Kama kuwa katika Chama ndiyo sifa kuu (hivyo ndivyo inavyoonekana) ya mtu kuchaguliwa, kwanini basi hata wale wanaomchagua wasilazimishwe kuwa wanachama wa vyama vya kisiasa? Maana haingii akilini kuwa tunaamini mtu anaweza kuchagua kiongozi na tukakubali uamuzi wake huo bila kumlazimisha awe kwenye chama lakini wakati huo huo yeye mwenyewe akitaka kuchaguliwa tunamuambia huwezi hadi uwe kwenye chama!
 
Luteni,
Luteni kuna mwana jamii moja kabla ya Post yako ameelezea historia ya kesi hii na sababu ya katiba kubadilishwa ili iwe kama ulivyo quote.

Sasa ukijua historia hiyo utakuwa katika nafasi nzuri ya kuelewa kama kuna uhalali au hakuna. na Jambo hili zaidi ya hiyo hukumu ya Jaji lugakingira, kuna maoni ya tume ya Jaji Mkuu Nyalali wakati huo, sasa sijui binadamu mwenye akili zake timamu anataka nini ili kujua haki ya kuwepo Mgombea Binafsi. Ndio maana leo hii maamuzi ya kitaalamu yana amuliwa na wanasiasa.

inabidi tufike mahali tujue nini cha wanasiasa, nini cha wanataaluma, nini ni cha Bunge nk nk.
 
Malafyale,
Asante malafyale nimekiona hicho kifungu cha 21(i) kweli kinapingana na vifungu 5 39 na 67 nilivyovinukuu awali nafikiri hukumu ya jaji Lugakingira ili-base hapa basi Mtikila ana uwezekano mkubwa wa kushinda katika hukumu yeyote ikitokea katiba inajichanganya basi majaji wanao uwezo wa ku-favour upande wowote.
 
Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa Februari 8, mwaka huu na jopo la majaji saba wakiongozwa na Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani, Jaji Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathania Kimaro, Mbarouk Salim, Dk. Stephen Bwana na Benard Ruanda.
 
Luteni,
Mkuu Luteni rejea kesi ya kwanza ya Mtikila ya mwaka 1992. wakati anashinda hii kesi hivi vifungu ulivyovinukuu vilikuwepo? Na kama havikuwepo viliingizwa lini na kwa sababu gani? Huoni kama Serikali iliviongeza hivyo vifungu ili ijiandae kuja Kumbwaga Mtikila?

Na je kwa kuingizwa kwake huoni kunaifanya katiba yetu iwe inajikanganya yenyewe yaani full contradictory, bora liende tu
 
Hivi mnafikiri hii kitu itapita?hata akija jaji mahiri kuliko wote duniani,kama hakuna Political will hiii hoja haipti ng'o..let wait and see halafu tutaona...hili liinchi halina Demokrasia kabisa..demokrasia yetu ni ya kwenye maandishi tu...
 
Let take the argument a notch higher. Tanzania imetia sahihi na kutambua Azimio la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu (rejea hotuba ya Mwalimu kwenye Umoja wa Mataifa). Azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni msingi wa Haki za Msingi (Bill of Rights) za Katiba nyingi za nchi mbalimbali. Natambua kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye Azimio hilo yameanishwa kabla katika Katiba mbalimbali na Maandishi mbalimbali kabla yake.

Kwa ajili ya hoja zetu tuangalia Ibara ya 20 kwanza:

Inasema Msisitizo wangu.
Article 20.
  • (1) Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and association.
  • (2) No one may be compelled to belong to an association.
Katiba ya Tanzania inamlazimisha mtu kujiunga na jumuiya au chama fulani. Kwa kusema kwamba mtu hawezi kugombea nafasi ya uongozi isipokuwa awe mwanachama wa chama cha siasa (siyo ya dini, shirika n.k) Katiba yetu inavunja moja kwa moja ibara hiyo.

Nayo Ibara 21 sehemu yake inasema:

Article 21.
  • (1) Everyone has the right to take part in the government of his country, directly or through freely chosen representatives.
Kama "Kila mtu" anayo haki ya kushiriki katika utawala wa nchi yake moja kwa moja (kama kiongozi) au kuchagua kwa uhuru wawakilishi wake basi Katiba yetu inatunyima haki ya kuchagua kwa uhuru kwani tunaambiwa NI LAZIMA tuchague mtu aliye kwenye chama cha siasa.

Sasa inakuwaje kama yupo Mtanzania ambaye ana uwezo na ana nia ya kushiriki katika uongozi wa taifa lake (per article 20) na wananchi wanataka awaongoze (iwe udiwani, ubunge au Urais) lakini Katiba inasema hawezi kwa sababu japo ana sifa nyingine zote lakini hana ya uanachama je kwa hili siyo uvunjaji wa Azimio hilo kwa kuwanyima watu uhuru wa kumchagua?

Je, kama tunaambiwa mnaweza kuwachagua x,y, z, d, a lakini hamuwezi kumchagua m kwa sababu hajajiunga na kikundi cha siasa, je kama tunamtaka "m" kutuongoza (no pun intended here) si kwamba tumenyimwa uhuru huo kwa kuweka kipengele cha kulazimisha chama cha siasa? Mahakama zimeshaamua huko nyuma jibu ni ndiyo.

Lakini naweza pia kutoa hoja nyingine kutoka kwenye azimio hilo; nayo ni ajira.

Article 23.
  • (1) Everyone has the right to work, to free choice of employment, to just and favourable conditions of work and to protection against unemployment.
Kama mimi nataka kuwa diwani na kwamba hiyo ndiyo iwe kazi yangu ya kunipa ujira lakini sitaki kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kwa kunilazimisha nijiunge na chama hicho kunaninyima uhuru wa kuchagua ajira niitakayo?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mwanakijiji
Uko sahihi kabisa...tatizo ni Political will ya waliokamata nchi...hawataki kwa makusudi kuwa na Mgombea binafsi kwani tayari wanaona mbele...wanatambua kabisa kwamba kuna watu wanamajina makubawa ikitokea wakiruhusu hii watu hao watakuwa na fursa ya kusimama wenyewe na kushinda chaguzi mbalimbali halafu ndio mwanzo wa vyama vya siasa kuwa weak.

wanafahamu kabisa kwamba ndani ya vyama vya siasa kuna madudu mengi ambayo wengine wanatamani kutoka lakini kwakuwa wana vission za kisiasa hivyo inawalzimu kuendelea kuvitumiaki hivi vyama hata kama ni kwashingo upande.
 
GS, usiwe na shaka; mwaka huu wagombea binafsi wataruhusiwa. Tatizo langu ni kuwa watawala wanaweza kuchelea kulitekeleza hilo.
 
GS, usiwe na shaka; mwaka huu wagombea binafsi wataruhusiwa. Tatizo langu ni kuwa watawala wanaweza kuchelea kulitekeleza hilo.
mkuu huitaji kuwa kiona mbali kuliona hilo, huitaji nguvu za giza za shehe Yahya kuliona hilo, ni dhahiri.....
kama CCM bara walitaka kuingilia swala la ZNZ kuwa kura za maoni zipigwe baada ya uchaguzi mkuu wa kisiwa hicho na laiti Wazanzibar wasingewastukia wangefuata ushauri wao...ila bado nasikia kina makamba wanafight vilivyo kuhakikisha wanaingia kwenye uchaguzi mkuu bila kuwa na sheria itakayo ruhusu mseto katika utawala.

sasa CCM ni mabigwa wkuingilia mifumo ya mahakama kwa kutumia ushawishi wa rais mwenye mamlaka yakuwateua na kuvukuza kazi watendaji wakuu wa muhimili wa mahakama.
 
Back
Top Bottom