Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzuzu, May 16, 2008.

 1. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2008
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mahakama yasisitiza wagombea binafsi

  na Happiness Katabazi
  Tanzania Daima


  MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania, imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na serikali, ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi za Tanzania.

  Uamuzi huo ulisomwa jana na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Ferdinand Wambali, kwa niaba ya jopo la majaji watatu, ambao ni John Mroso, Edward Rutakangwa na Engela Kileo.

  Akisoa uamuzi huo, Wambali alisema jopo hilo limekubali pingamizi la upande wa mawakili wa mdaiwa, Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki, ambao waliiomba mahakama kutupilia mbali rufaa hiyo.

  Katika pingamizi hilo, Rweyongeza aliieleza mahakama ombi la rufaa la serikali limejaa dosari za kisheria, likiwemo kosa la kuandika tarehe tofauti ya tarehe ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.

  Wambali alisema wamefuta kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana baada ya kubaini mawakili wa serikali, Mwaimu na Ndunguru waliwasilisha hoja dhaifu, ambazo zimeshindwa kulishawishi jopo hilo kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

  “Kwa sababu hiyo, jopo hili linakubaliana na pingamizi la upande wa mdaiwa, na linatupilia mbali ombi la mrufani, na linaamuru upande wa mrufani kumlipa mdaiwa gharama za uendeshaji wa kesi,” alisema naibu msajili huyo.

  Hata hivyo, alisema serikali inaweza kuwasilisha tena rufaa yake mahakamani kwa kufuata sheria kama itaona kuna haja ya kufanya hivyo.

  Machi mwaka jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliwasilisha rufaa iliyopewa namba 20/2007 akiomba Mahakama ya Rufaa itupilie mbali uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuruhusu mgombea binafsi, kwa kuwa umeonekana kuwa na dosari za kisheria.

  Mei 5 mwaka 2006, Mahakama Kuu chini ya jopo la majaji watatu walioongozwa na Jaji Kiongozi mstaafu, Amir Manento, waliruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika chaguzi kwa sababu katiba ya nchi inatoa haki hiyo. Majaji wengine walioshiriki kutoa uamuzi huo ni Jaji Kiongozi wa sasa, Salum Massati na Thomas Mihayo.

  Jopo hilo lilibainisha kuwa, katiba inatamka wazi kuwa kila mwananchi anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mwananchi kujiunga na chama fulani cha siasa.

  Katika hati ya rufaa ya serikali, Mwanasheria Mkuu wa serikali anadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria katika kutafsri Ibara ya 21 (1) ( c ), 39 (1) (c ) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mwaka 1993, mbele ya Jaji Khawa Lugakingira (sasa marehemu), Christopher Mtikilia alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Hata hivyo, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi katika chaguzi zilizofuata, na ndipo Mtikila alipoamua kufungua tena kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kushinda.

  Mtikila alifungua kesi hizo akiomba mahakama itamke kwamba mabadiliko ya ibara ya 39 na 67 chini ya marekebisho ya 11 ya katiba ya nchi kuwa ni batili na kwamba itamke kuwa ibara ya 21(1) inampa haki ya kikatiba ya kuwa mgombea binafsi katika nafasi ya urais na ubunge.

  Katika madai yake, Mtikila alieleza mabadiliko hayo ya katiba yanavunja haki za binadamu ambazo zimeainishwa wazi kwenye ibara 9(a) na (f), 13(2), 20(4) na 23(1) ndani ya katiba kama ilivyoainishwa kwenye tamko la haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.
   
 2. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wind of changes is blowing everywhere!
  This is a good start to our Judges,While the king is seated at his table, the spices has send out their perfum to people.
  Bravo
   
 3. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa CCM waka chonjo maana wagombe binafsi watatokea hukohuko CCM baada ya kuachwa kwenye kura za maoni. inawezekana utabiri wa mwalimu unakaribia kukamilika kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapo katikati niliwahi kusema kwamba JK alikuwa hapati usingizi kwa neno mgombea binafsi.I hope sasa kwamba ameridhika kwamba maamuzi ni sahihi na Lunyungu nitasimama Kibaha maana nimekaa sana hapa .CCM naamini wameumia na hawana namna sasa .Wale wote wanao kimbilia Vyama sasa wameanguka chaliiiiiiiiiii.Vurugu zote za vyuoni na CCM kwisha kabisa .Hongera Majaji .
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Mahakama sasa imeendelea kushinikiza uwepo wa wagombea binasfi!

  Kwa wale waelewa wa siasa..Tunaweza kusema kuwa ugombea binafsi ni jambo la kidemokrasia!

  Lakini kwa upande mwingine..Haki hii ya ugombea binafsi imekuwa ikikinufaisha iether chama kimoja cha kisiasa ama kingine!

  Kwamba mara nyingi si wagombea binafsi ambao wananufaika binafsi bali vyama vilivyoko kwenye kinyang'anyiro!

  Tumeshaona mifano halisi kama vile Ralph Nader ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kwa Al Gore kwenye uchaguzi wa USA 2000!

  Swali sasa linakuja kwenye siasa zetu Tanzania...

  Je kuna chama kitakachonufaika na uamuzi huu wa mahakama hapo baadae?
   
 6. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  pamoja na kushindwa kwa Al gore mwaka 2000, hii haiondoi umuhimu wa mgombea binafsi, inapotokea vyama vikawa na mizengwe ni rahisi kwa mtu mwenye uwezo kusimama kuomba kura za wananchi akiwa kama mgombea binafsi.

  pili hii itasaidia kuvipa vyama discipline, badala ya ukiritimba wa kimaamuzi wa baadhi ya vigogo katika vyama kuwawekea vikwazo washindani wao kisiasa ndani ya vyama hivyo, itabidi wajiulize mara mbili mbili kwa sababu ukimkwaza mtu anakwenda zake kusimama kama mgombea binafsi.

  tatu hii inapanua demokrasia katika jamii, haiwezekani mtu asiyekuwa na chama aweze kupiga kura kuchagua wenye vyama halafu eti na yeye akose haki ya kuchaguliwa.hii ilikuwa hai make sense.
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ni suala zuri na kupanuka kwa demokrasia.


  hata mkjj anaweza kugombea bila ya chama maana mbowe hatokubali kumwachia kiti
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa as long as sheria mpya haijatungwa sheria iliyopo bado inatumika.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe lakini kuna watakaoitumia kwa nia mbaya ya ku divide kura ili kumfanya mwingine ashinde!
  Lakini si ndio demkrasia hiyo?
  Hapa bottom line itategemea na uelewa wa wananchi kwenye suala husika.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii ni habari njema na ni habari yenye uzito mkubwa sana katika Tanzania yetu.

  Naona upande wa serikali expectedly, umepewa rukhusa ya kuweza kukata rufaa... nevertheless, the fact that wanasheria wa serikali walichemka katika procedure basic kama hizo walipowasilisha kesi, ni jambo ambalo linaonesha ukurupukeni wa serikali kupitia mawakili wake na si kinginecho...

  SteveD.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wengi sana wenye uwezo wa kuiongoza nchi yetu lakini wamechoshwa na siasa za CCM na Upinzani na labda wana haki ya kuwa wagombea binafsi!
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Na pia kwanini wanaopinga wawe na wasiwasi kiasi hicho?
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Ooh okay..Imeunganishwa!
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Kama mambo yasipobadilika kama wananchi wanavyoambiwa wasubiri yatabadilika..Kama vile kuwatia nguvuni mafisadi..Then usishangae wengi wetu wakimu endorse mgombea binafsi atakaye fuata matakwa ya wananchi!
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  stage ya pili tunataka mawaziri wasiwe wabunge.
  manake mtu mmoja, mfano waziri kutoka ccm, yeye ni waziri, yeye ni member wa nec, yeye ni mbunge, yeye ni mkurugenzi wa makampuni na mashirika ya umma kadhaa, yeye ni kiongozi wa familia. ..........
  demokrasia inapanuka, na ipanuke katika mengi
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye highlight naweza kukubaliana na wewe kwasababu moja kubwa..

  Wabunge wanapopewa uwaziri mara nyingi tumekuwa na frikra kuwa sasa kwasababu katokea jimbo flani..Basi atafanya majukumu yake kwa kubase zaidi kwenye jimbo lake na ndio maana tuna tabia ya kuwafagilia hata kama ni mafisadi!

  Juzi tu hata Pinda alipoteuliwa kwenye nafasi ya uwaziri mkuu..Maneno yakaanza kuwa eti sasa RUKWA ITAKUMBUKWA!

  Yani Rukwa ilisahauliwa kwasababu eti haikuwahi kutoa waziri mkuu?
  Hizi ni issue za kuzitupia macho!
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Na hapo ndio umemaliza mchezo mkuu Gaijin!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,056
  Trophy Points: 280
  High Court has no powers to rule on independent candidates, says minister

  ALVAR MWAKYUSA
  THIS DAY
  Dar es Salaam ​

  THE government has explained why it is intending to appeal against a High Court ruling in favour of private candidates.

  The Minister for Justice and Constitutional Affairs, Mathias Chikawe, told THISDAY in Dar es Salaam earlier this week that the intention to appeal is based on the belief that the High Court over-stepped its authority in giving the ruling.

  ’’We will be appealing against the powers of the court in this matter. We are questioning whether the High Court has the mandate to alter sections of the national constitution,’’ Chikawe said.

  ’’If this trend is left to continue, the court could alter the whole of the constitution,’’ the minister asserted, while at the same time striving to emphasize that the government is not against independent candidates.

  According to Chikawe, courts of law are supposed to interpret the laws of the land in resolving cases � but not to alter the laws.

  The High Court recently ruled in favour of the removal of restrictions preventing people not affiliated with any political parties from running for the presidency or parliamentary seats during general elections.

  The court directed the Attorney General’s Chambers to put in place a legislative mechanism to regulate the activities of non-party candidates in next year’s elections.

  Efforts to get a comment from Attorney General Johnson Mwanyika were not successful as he was said to have travelled out of the country, while his deputy was said to be in Zanzibar on official business.

  In its ruling, the High Court declared as unconstitutional the 1994 Election Law stipulating that anyone wanting to contest political posts must be members of a registered political party.

  The court said some articles in that law were unnecessary and unreasonable, only serving to restrict the fundamental rights of the citizenry to vie for elective political posts either as party members or as private candidates.

  It was the second time the High Court has ruled in favour of independent candidates. In 1994, the late Justice Rugakingira declared that it should be lawful for independent candidates, along with candidates sponsored by political parties, to contest presidential, parliamentary and local council elections held in the country.
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Uchuro wa watendaji serikali ya Tanzania.

  Kazi ya kutafsiri mikataba na kutafsiri sheria kwa vitendo ni ya Mahakama.
  Hakuna chombo kingine chochote klicho na uwezo wa kutafsiri sheria zaidi ya Mahakama.
  Bunge lina uwezo wa kutunga sheria na kwa kiwango fulani kidogo kutafsiri sheria hizo kupitia kamati zake. Kwa sababu bunge limejaa watu wenye agenda za kisiasa Bunge si mahali penye usahihi wa 100% wa kutafsiri sheria.

  Majaji hawapigiwi kura, majaji hawana agenda za kisiasa wala hawaogopi matokeo ya maamuzi yao ya kisheria. Jaji ni jaji mpaka astaafu au afe. Nguvu ya Jaji iko ndani ya sheria na kazi yake ya ujaji na si katika chombo fulani au kundi fulani la watu au Wahuni ndani ya serikali
  Nguvu ya mbunge iko kwenye siasa na si kazi aifanyayo ya kutunga sheria. Nguvu ya Mbunge ina ukomo wa Muda wa miaka 5. Mbele ya sheria mbunge ni mtu anayejichanganya kimaslahi. Siku zote mbunge atachagua siasa kuliko kuchagua kutunga sheria aua kuimarisha sheria kwa manufaa ya taifa.

  Mahakama ni chombo pekee kisicho cha kisiasia chenye uwezo na mamlaka yakutafsiri sheria bila kuwa kujikanganya kimaslahi kama Bunge.

  Taarifa ya serikali imejaa siasa na ulevi wa madaraka kama siyo ununda na umbumbu wa katika nyanja za haki za kikatiba kwa kila mwananchi.

  Mtu binafsi kugombea nafasi ya uongozi havunji katiba ya Tanzania kwa sababu katiba inasema kila mtu ana haki ya kushiriki katika siasa kama mtu.

  Kwa hiyo vifungu vingine vinavyo mlazimisha Mtanzania kushiriki katika siasa kupitia makundi ya kichama ni vifungu vinavyo kwenda kinyume kabisa na haki ya kisiasa aliyonayo Raia Mwema.

  Safari hii serikali wamekuja na Gia kwamba Mahakama haina uwezo wa kutafsiri na kuamuru sheria fulani ndani ya katiba ibadirishwe kwa sababu inapingana na sheria mama ya haki ya Mtanzania katika kushiriki siasa.

  Ni serikali hii hii imekiri wazi kwamba haina uwezo wa kuandika mikataba ya maana kati yake na Wachimba Madini Wafua Umeme na wafanyi biashara wengi kutoka nje na ndani kiasi cha kusababisha upotevu wa Mabilioni ya Dola huku watendaji haohao wakitajirika Overnight kwa kujijazia vijisenti kwenye account za nje.

  Kwa nini leo hiii wanakuja na Gia kubwa kwamba wana uwezo wa kujua kwamba Mahakama haina nguvu za kuingilia kati vifungu vyenye utata ndani ya katiba?
  Hivi Jopo la majaji na wanasiasa hawa wasio na uwezo wa kuandika mikataba yenye kunufaisha taifa nani ana jua sheria zaidi??

  Watendaji wengi wa serikali wanajificha nyuma ya serikali kuendeleza sheria za kikandamizaji ili kundi lao la Mharamia ndani ya CCM liendelee kuongoza kwa nguvu ya Rushwa ndani ya vikao vya ndani vya CCM vilivyo jaa manyang'au wenye hamu na kiu kuharibu bila faida kwao wala kwa vizazi vyao.

  Mjumbe wa Kikao ndani ya CCM ukipewa Tshs 75,000.00, ukalipiwa Guest house kwa siku 7, ukapewa Ulabu na Huduma ya MaChangu Doa au Vijust ili umchague Fisi kuwa mbunge, wewe unapata nini? Mkeo au Mumeoanapata nini? Binti yako ana pata nini?
  Ukichukua hiyo 75,000/(365X5) kila siku ni sawa na kulipwa Ths 4.10 na wasi wasi wa kukwaa miwaya?????

  Hivi watanzania ndani ya CCM bei yenu kwa siku ni ndogo naman hiyo?
  Shs 4 mpaka 1000 kwa siku zina kufaa nini?

  Hata hiyo Fisi akiwapeni Rushwa ya Tshs 1,825,000.00 ni swa na kujipatia 1000 kwa siku kwa muda wa miaka 5. fedha hiyo ni ndogo sana ukilinganisha na vurumai na dharau kubwa tupewao na Wabunge wahuni na wanyonge waliojaa ndani ya Bunge la Tanzania.

  Serikali yetu imejaa wasomi walioacha elimu yao yote mashuleni na kuondoka na kiburi cha shule tu.
  Wengine kama yule naibu waziri wa ulinzi mtani wangu mngoni ni Ma Dr Vihiyo wa kununua vyeti.
  Serikali yetu imejaa watu waliokua vimbelembele wa kutaka na kulilia umonita darasani na kung'ang'ania kugawa msosi kila siku ili wajijazie bondo la kutosha kwenye shani zao.

  Serikali yetu imejaa wasomi vipanga na manunda wa kutaka ujiko kwenye kila kitu.

  Labda safari hii watashinda hasa ukizangatia mahela mengi waliyoiba na wanayoendelea kuiba.
  Ukiwa na fedha siunapata uwezo kumnunua kila mtu???.

  Labda safari hii wanunue majaji wote kwenye jopo, kinyume cha hapo ushindi wa kesi hii muhimu bado ni Mtikilia.

  Mh Chilawe bado una kazi ya kutekeleza hukumu hii.

  Unataka au huna taka.
   
  Last edited: May 31, 2009
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama ni kwa hoja serikali imeshshindwa kwa sababu hata bwana waziri hapa anachoonyesha ni kuwa tatizo lao si hoja ya mgombea binafsi, bali uwezo wa mahakama kutoa amri kuhusiana na hoja hiyo. Namshukuru sana bwana waziri kwa kuonyesha kuwa hoja hii imeshinda, sasa wanataka kuipinga kwa vioja. Tusonge mbele
   
Loading...