Mgawo wa Umeme wasitishwa, utafiti mpya umeona hauhitajiki kama awali

Kwa sababu Kalemani alilimaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme naamini January Makamba baada ya haya matengenezo anayoyafanya kwa siku 10 siyo tu mgai utakuwa historia bali hata kiwango cha umeme unaozalishwa kitaongezeka.

Kadhalika kwa sababu sasa umeme utakuwa haupotei baada ya miundombinu kukarabatiwa ni wazi bei ya umeme mitashuka.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
Miaka 60 ya uhuru bado kuna mgao
 
Ifanyiwe maintenance au isifanyiwe, hiyo siyo sababu ya kusababisha migao.

Ndo maana nimeshahoji kuwa, huko kwingine mitambo yao huwa haifanyiwi maintenance?

Maana katu sijawahi sikia hata kwa lisaa limoja tu kuwa kutakuwepo na mgao wa umeme wa siku 10 kwa sababu mitambo inafanyiwa maintenance.

Hawa Tanesco wetu hawana uwezo wa kufanya maintenance kwenye mitambo yao bila kusitisha huduma? Haiwezekani kabisa kufanya hivyo?
Mbona nilikujibu Mkuu Nyani? Inawezekana kufanya maintenance ya kawaida bila kusitisha huduma. Tanesco hawawezi kufanya hivyo kwa sababu inaendeshwa kisiasa na sio kitaaluma. Uamuzi wa lini wafanye maintenance sio wao ni wa wanasiasa.
Wao na binamu zao ATCL wako chungu kimoja. Ndege hazikununuliwa kwa sababu za kibiashara bali kutuliza ego ya wanasiasa.

Amandla...
 
Back
Top Bottom