Mgawo wa Umeme wasitishwa, utafiti mpya umeona hauhitajiki kama awali

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,816
Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Stephen Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya utafiti huku wakiwa wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia kwamba mgao usiwe mkali kama ilivyotangazwa.

Kupungua kwa matumizi ya umeme, mvua zinazoendelea na kutumia mitambo ya TPDC kwenye gesi vimetajwa kama sababu ya kuuhairisha.

=========

Mbunge(Luhaga Mpina): Katakata ya umeme inayoendelea na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa, mwanzo tulielezwa ni kwasababu ya matengenezo ambayo hayakufanyika kwa miaka mitano, maada ya muda mfupi tukaambiwa ni kwasababu ya mabwa kukauka wakati huo huo TANESCO wanasema hakuna mgao wa umeme baadae Tanesco wanatangaza mgao wa umeme.

Tuelezwe na Serikali kwasababu linaathiri sana watanzania. Taifa liko kwenye hali ngumu ya ukosefu wa umeme. Nini kinachosababisha hali hii ya katakata na mgao wa umeme?

Naibu Waziri(Nishati): Tanesco haikatikati umeme, hakuna mtu ambae ameajiriwa kwa ajili ya kukata umeme, mifumo ya umeme inarespond kutokana na mazingira iliyokuwa nayo na kikubwa kinachotokea, pale ambapo mitambo yetu inazidiwa na matumizi yenyewe automatically inakata umeme.

Tunachofanya ni kuhakikisha tunaongeza nguvu za mitambo.

Tulitarajia kwenye marekebisho ya mitambo yetu ya kufua gesi ambayo inazalisha sehemu kubwa zaidi, twende tukarekebishe kwenye mitambo ya gesi. Matarajio makubwa ya mgao ambayo tulidhani tutakuwa nayo hatutakuwa nayo.

Sababu tatu zilizopelekea kuahirishwa mgao mkali
  1. Kwa maelezo ya Rais, amesema mgao usiwe mkali, tukabaini tunaweza kuchepusha gesi baadhi ikapitia mitambo ya TPDC badala ya kampuni ya Paet
  2. Hali ya mabwawa imeanza kurejea katika hali nzuri
  3. Umeme ni supply and demand, kile ambacho tulitarajia kitahitajika sicho kinachohitajika, tutahakikisha watu wanaendelea kupata umeme.
Stephen Byabato.jpg
 
Kama maelezo hayo ndio kilichosemwa nimejiridhisha pasipo shaka kuwa KUKATA UMEME ni hujuma. Ndio maana awamu ile iliwazuia na haukukatika ovyo.

Yaani Rais amesema HAWAJAKATA ina maana uwezakano ulikuwepo tangu mwanzo. Top menejimenti kuanzia Waziri yatunzwe majina yao kwa matumizi ya baadae
 
Mbezi ya Kimara tangu j3 wanakata saa mbili asubuhi wanarudisha saa 6 usiku, huu utafiti wameufanya saa ngapi? Kwa maana hata leo pia wamekata kuanzia saa 2 asubuhi
 
Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya utafiti huku wakiwa wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia kwamba mgao usiwe mkali kama ilivyotangazwa...
Uongo mbona huku maeneo wilaya ya kibindoni hatuna umeme tangu asubuhi
 
Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya utafiti huku wakiwa wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia kwamba mgao usiwe mkali kama ilivyotangazwa...
Nipo mgahawa mmoja jirani na stand kuu Tabora, nasikia muungurumo wa generator, na harufu ya petrol kwa mbali. Hakuna umeme wa grid.
 
Back
Top Bottom