Mgawo wa Umeme wasitishwa, utafiti mpya umeona hauhitajiki kama awali

Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Stephen Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya utafiti huku wakiwa wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia kwamba mgao usiwe mkali kama ilivyotangazwa.

Kupungua kwa matumizi ya umeme, mvua zinazoendelea na kutumia mitambo ya TPDC kwenye gesi vimetajwa kama sababu ya kuuhairisha.

=========

Mbunge: Katakata ya umeme inayoendelea na mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa, mwanzo tulielezwa ni kwasababu ya matengenezo ambayo hayakufanyika kwa miaka mitano, maada ya muda mfupi tukaambiwa ni kwasababu ya mabwa kukauka wakati huo huo TANESCO wanasema hakuna mgao wa umeme baadae Tanesco wanatangaza mgao wa umeme.

Tuelezwe na Serikali kwasababu linaathiri sana watanzania. Taifa liko kwenye hali ngumu ya ukosefu wa umeme. Nini kinachosababisha hali hii ya katakata na mgao wa umeme?

Naibu Waziri(Nishati): Tanesco haikatikati umeme, hakuna mtu ambae ameajiriwa kwa ajili ya kukata umeme, mifumo ya umeme inarespond kutokana na mazingira iliyokuwa nayo na kikubwa kinachotokea, pale ambapo mitambo yetu inazidiwa na matumizi yenyewe automatically inakata umeme.

Tunachofanya ni kuhakikisha tunaongeza nguvu za mitambo.

Tulitarajia kwenye marekebisho ya mitambo yetu ya kufua gesi ambayo inazalisha sehemu kubwa zaidi, twende tukarekebishe kwenye mitambo ya gesi. Matarajio makubwa ya mgao ambayo tulidhani tutakuwa nayo hatutakuwa nayo.

Sababu tatu zilizopelekea kuahirishwa mgao mkali
  1. Kwa maelezo ya Rais, amesema mgao usiwe mkali, tukabaini tunaweza kuchepusha gesi baadhi ikapitia mitambo ya TPDC badala ya kampuni ya Paet
  2. Hali ya mabwawa imeanza kurejea katika hali nzuri
  3. Umeme ni supply and demand, kile ambacho tulitarajia kitahitajika sicho kinachohitajika, tutahakikisha watu wanaendelea kupata umeme.
Kwa maelezo hayo basi umeme kukatika huwa ni maslahi ya watu binafsi yanafanyika,, sasa kama rais amesema amesema mgao usiwepo na mmetii inamaana kumbe matengenezo yangefanyika bila kuwa na mgao ila nyie tanesco mlikua na mambo yenu binasfi!!! pumbafu sana hili shirika la hovyo sana.

Mpaka hapa nimejiridhisha 100% kwamba umeme ukikatwa huwa kuna mambo yao binafsi ya kishenz
 
Waziri na ile menejimenti yake yote ya wezi.
 
Huku Kinondoni north. Au north of dsm from mwenge to Mbweni hakuna umeme mpaka wakati huu. Nadhani wahusika wanafurahia sana haya matengenezo.

Kama wananchi hatuoni kama wakubwa hili la umeme linawauma wao wanatumbua ma bruch tu mixer kuku wa kupaka huku sisi tunaumia vibaya sana na mgao.

Sent from my Infinix X605 using JamiiForums mobile app
 
Toka nizaliwe cjawahi kuona mgao na matengenezo ya hadi saa sita usiku
 
Wewe ni robot? Watu walipolalamika kuhusu umeme wa mgao ulisema ni lazima uwepo ili maintenance ifanyike.
Leo imeletwa taarifa kuwa mama Samia kaingilia Kati, unapongeza na kuona hakuna haja ya mgao.

Ha ha ha mkuu hicho Nyerere alikiita ni kipaji..
 
Tatizo la kuamini watu wachache tu Ndio wenye haki ya kuongoza nchi ...

Mtanzania mmoja ailezee Wizara ya Nishati Na waziri wake kwa sentence moja tu pasipo kupata maumivu ya kichwa ...kama yupo
 
Bw. February kasemwa sana kiasi kwamba inabidi apunguze kasi ya kuwakumbatia wenye biashara zao
Yaani Mgao unapungua baada ya yeye kukalishwa kitako, Kwamba kama asingali kalishwa chini ungelikuwepo mgao. Na naibu nae anasema baada ya kukaa na Rais ndio wakaenda kukaa na wataalamu akimaanisha kwamba tangu swala linaonekana hadi mgao unapangwa hakukuwa na reaction ya kutizama ufanisi wa ku handle angali wataalamu walikuwepo. Bado natazam tu. Pengine ningepewa majibu ya maswali haya labda ningepata picha: Kipi Anafanya Makamb Kalemani Hakufanya au alikuwa hawezi kukifanya? na sina maana kwamba haikuwa na haja au hafai lahasha ila nawasiwasi kwamba kama tunakwangua nyeupe na kuweka nyeupe( tena iliyo fubaa) basi huenda tunapoteza muda katika mambo ambayo hayakustahili muda wetu.
 
Back
Top Bottom