Kuna mwana jf mmoja humu ana signature inasema "mitanzania ndivyo tulivyo" mimi nakubaliana nayo sana hii kwa sababu kila siku tumekuwa wa kudanganywa na sirikali hii hii na hatufanyi lolote kuonyesha tumekasirika!, ebu tazama suala la mafuta yameshushwa wauzaji wakagoma serikali ikatupiga changa la macho kuwa inachukua hatua kali, bajeti imepita bei imepanda kushinda ilivyokuwa awali. Mgao wa umeme ndio kama mnavyouelezea hapa, je si tunafanyiwa kwa sababu ndivyo tulivyo?!
Kitu kingine mnisaidieni jamani ule mchakato wa katiba mpya umefikia wapi?! 2015 iko mlangoni hivi itakamilika ili uchaguzi uwe huru na haki kweli?!
Sio siri naanza kuwa na wasiwasi na makamanda wetu mjengoni naona kama wamenunuliwa vile!! mbona mambo haya nao hawayapigii kelele wanakubali kupigwa changa la macho kama sisi tulioko nje ya mjengo?!!