Mgao umeanza tena?

Mgao umeanza tena?

<br />
<br />
mmh!kwani mgao uliisha bandugu?huku mikoani maumivi palepale!

Na mie wa Arusha nilitaka kuuliza hivyo hivyo.....Huku maumivu ni makali balaa...Kama ni mgonjwa,basi yuko ICU
 
Nauliza kama mgao umeanza upya..manake toka jana kijitonyama tanesco wanachukua umeme wao saa kumi na mbili asubuhi na kurudisha kumi na mbili jioni...hii imekaaje?

siku moja kabla ya kusomwa kwa mara ya pili kwa bajeti ya waziri-porojo ngeleja, tukaoneshwa kwenye runinga tukio la kuwasili kwa mitambo ya megawatiwa 100. wiki moja kabla tu tulipumbazwa eti bei ya mafuta imeshuka, mara bp imefungiwa, sijui nini. puf. wehu mtupu.

baada ya bajeti............

jumatatu umeme unakatwa tangu asubuhi na wanarudisha wanapojisikia.

hatujakaa sawa tukaambiwa bei za mafuta zimepanda tena.

hapa ndipo ninapodiriki kusema, kikwete na timu yake yote inayounda serikali, ukiondoa Prof. Tibaijuka ni takataka.

wanatuona sisi mafala - hamnazo.

mimi nimeamka, wewe je?

piga vita ccm na ufisadi wake mwanzo mwisho, usirudi nyuma.
 
Hapa makuburi ndiyo umerud muda c mrefu..toka saa tatu asubuhi
 
Bajeti si imepitishwa..sasa wewe unategemea nini.
 
Serikali inaongozwa na Raisi muongo,waziri mkuu muongo ,mawaziri na watendaji wengine wa serikali waongo watupu serikali ya ovyo kabisa wanachezea akili zetu ni kama vile wanatulambisha pipi ya kijiti,yaani kila mtu kwa nafasi yake awe anajitayarisha kuwawajibisha ,wamechoka hawafai
 
Mgao uliisha lini jamani? Arusha mgao bado uko tena toka alhamisi ya last week ndo wameanza wa masaa 24..kama sio 26.. Tabu tupu huku kwetu!
 
Kama mnapata mgao mshukuruni Mungu.
Kwetu mgao ulishaisha(YANI HATA UMEME WA KUGAIWA HAUPO).
Ni giza tupu.
 
Mgao upo c bajeti imeshapita......Arusha-njiro we didnt have umeme for 3 days umekuja Leo
 
Nauliza kama mgao umeanza upya..manake toka jana kijitonyama tanesco wanachukua umeme wao saa kumi na mbili asubuhi na kurudisha kumi na mbili jioni...hii imekaaje?

Kwani ni lini uliambiwa kuwa mgao umeisha? mimi nilimsikia Waziri wa nishati akisema mgao utakwisha December, sasa wewe ulikuwa na kauli mbadala dhidi ya aliyoitoa waziri?
 
sio huko tu huku kwetu wanachukua saa kumi na mbili asubuhi na kurudisha saa tano usiku
 
Kwani ni lini uliambiwa kuwa mgao umeisha? mimi nilimsikia Waziri wa nishati akisema mgao utakwisha December, sasa wewe ulikuwa na kauli mbadala dhidi ya aliyoitoa waziri?
swala ni kwamba waziri alisema makali ya mgao yamepungua lakini baada ya bajeti makali yameongezeka hiyo ndo issue hapa.
 
Mh!nitarudi umeme ukishawaka. Tafakari chukua hatua.
 
swala ni kwamba waziri alisema makali ya mgao yamepungua lakini baada ya bajeti makali yameongezeka hiyo ndo issue hapa.

Kumbuka kuwa inafungwa mitambo mipya na ni lazima kutokee usumbufu mpaka itakapo kamilika kufungwa. Kama unabisha muite hata fundi umeme nyumbani tu, kabla hajakuwekea nyaya mpya atakutaka mzime umeme kama unawaka seuse mitambo mikubwa.
 
Nauliza kama mgao umeanza upya..manake toka jana kijitonyama tanesco wanachukua umeme wao saa kumi na mbili asubuhi na kurudisha kumi na mbili jioni...hii imekaaje?
<br />
<br />
kama sisi tu huku temeke,bajeti tayari.
 
mgao uko bado tena wiki hii kuna sehemu umekua worse, kama Ar ni siku tatu sasa umeme ukija haukai zaidi ya lisaa kwa siku,
 
Huku Mkoa wa Mwanza na wilaya zote yaani Sengerema, Geita, Magu, Kwimba n.k kote hakuna umeme leo ni siku ya TANO. Meneja wa mkoa wa Tanesco amesema waulizeni Serikali, megawati zimebaki 4 tu toka 46 zilizokuwa zinahitajika, hivyo ameona bora azigawe kwenye Hosptali ya Bugando na Seketoure.
 
Aisee! Poleni sana... Kazi kwelikweli...tusubiri tuone mwisho wake..
 
Back
Top Bottom