Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke lifanyie kazi hili

Abuhunna

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
405
228
Jana tarehe 23, majira ya saa tatu usiku nilifika hospitali ya Malawi - Yombo, (yenye hadhi ya kiwilaya - ni referral hospital katika ukanda wa temeke) nikiwa na kijana wangu mdogo ambae alikuwa na homa, huduma zikawa zimesimama kwa kinachoelezwa umeme hauko sawa katika majengo ya mapokezi pomoja na vyumba vya madaktari, wakati huo maeneo yote yanayo zunguka eneo la hospitali umeme upo na hata katika baadhi ya majengo ya hospitali pia umeme upo. Nilisubiri huduma kwa zaidi ya dakika arobaini mpaka nilipoamua kuondoka kwenda kutafuta huduma sehem nyingine.

Kilichonisikitisha, waliingia wagonjwa wa wadharura ambao wenyekuhitaji msaada wa haraka, mmoja ni mama mjamzito ambae alikuwa na changamoto ya upumuaji, na mwingine ni mvulana aliekuwa anatapatapa kupigania uhai wake. Madaktari wala manesi hawakuwepo katika maeneo yao, ni walinzi pamoja muhudumu mmoja asiyekuwa na sare wala beji ya utambulisho ndio alikuwa anatoa maelekezo kuwa wagonjwa hao wakimbizwe hospitali ya temeke, ndugu wakaanza kuhangaika kutafuta usafiri na kuwa kimbiza hospitali ya temeke, sijiu huko wakoliko wana hali gani.

Tunajua kuwa hospitali zetu kwa sasa zinafanya kazi kwa mifumo ya kompyuta, hivyo changamoto yoyote ya umeme lazima itakuwa na madhara katika uendeshaji. SASA JE HATA KWA MGONJWA WA DHARULA ndio ashindwe kusaidiwa kwa huduma za awali kisa umeme hakuna tena katika hospitali ya wilaya. Niliumia sana sijui kama wale ndugu wawili wako salama.
 
Pole kamanda ,huyu daktari anayesikia kuwa wenza na michepuko itaongezewa posho,mishahara unahisi atajali haya madhira!!!
 
Wanafanya kazi kubwa posha hakuna mshahara kiduchu wanasiasi wanawaingilia kwenye majukum yao hivyo bàsi kila mtu apambane na Hari yake kifupi watumishi wa afya wamevunjika moyo
 
Back
Top Bottom