Mgala muueni haki yake mpeni, na tusisahau baniani mbaya kiatu chake dawa

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
Huu ndio muonekano wa Hospitali ya Uhuru iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma , Ujenzi wa hospitali ya Uhuru umegharimu kiasi cha Shilingi Billioni 3.9 (Milioni 3900).

Ujenzi wa hospital ya uhuru ni agizo la aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alilolitoa kwa kusema fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za Disemba 9, 2018 zitumike kujenga hospitali hiyo.

NOTE: Kama kila Kiongozi wa nchi hii angeokoa Fedha zinazoelekezwa kwenye MATUMBO ya Viongozi kwa mwavuli wa sherehe za kitaifa za Uhuru, Muungano na Mapinduzi Tanzania ingekuwa na hospitali kama hizi au zaidi ya hii si chini ya 100, tungekuwa na shule za kisasa za Kata, tungekuwa na viwanda vingi vya kuchakata mazao n.k.

Mgala muueni haki yake mpeni. Uongozi ni maono na moja ya eneo ambalo Magufuli alikuwa na maono chanya ilikuwa ni pamoja na eneo hili la sherehe za Uhuru na Muungano. Alidhubutu kupunguza gharama za sherehe hizo kwa asilimia kubwa. Hukuishia tu katika kupunguza gharama bali akaenda mbali katika kusherehekea sherehe hizo kwa njia ya tofauti kama kutumia fedha hizo kwa ajili ya miundombinu ya madaraja, barabara na hospitali. Hili kwangu naona ni bora sana.

Kuliko kuwakusanya Viongozi nchi nzima na kulipana mabilioni ya posho ni bora kutumia mabilioni hayo kuweka alama itakayodumu na kunufaisha Watanzania wengi kuliko kunufaisha MATUMBO ya wachache.

Hapa hata Mtanzania akiingia kutibiwa ukamwambia karibu matunda ya UHURU anakuelewa. Sherehe hazimsaidii Mwananchi wa kawaida bali huwanufaisha Viongozi na familia zao.

Hakika baniani mbaya lakini kiatu chake dawa.
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti

1626437799411.png

1626437929787.png
 
Hivi ni kwanini Tanzania hatutilii maanani mandhari ya nje majengo yetu? Dodoma tayari ni sehemu kame. Kwanini eneo kama hili lisipandwe bustani za maua na miti kila sehemu? BTW Hospital ni utaalaam na vifaa. Tutatoa pongezi iwapo patakuwa na madaktari wazuri na vifaa vya kutosha.
 
Inaonekana haijakamilika.
 
tofauti ya magufuli na Samia

magufuli: hakuna shereh za uhuru, pesa zichukuliwe zijenge hospitali pale dodoma, itasaidia watu

magufuli: pesa za sherehe za muungano zichukuliwe zijenge barabara kutoka morocco mpka mwenge

Samia: pesa za sherehe za muungano zigawanywe alafu mzitumie pale mnaona zinafaa.

my take; hela za shereh za muungano zilizopita hatujui zimetumikaje na wapi. Mafisadi washagawana. RIP JPM, you were a true leader
 
Hayupo hata ufanyaje
 
Ni ujinga kama si upumbavu kusifia kitu kilichojengwa kwa amri na mtu aliyedharau mifumo.

Maana kwa kufuata amri za mtu, mtu kafa na amri zake zimekufa.
 
tofauti ya magufuli na Samia

magufuli: hakuna shereh za uhuru, pesa zichukuliwe zijenge hospitali pale dodoma, itasaidia watu

magufuli: pesa za sherehe za muungano zichukuliwe zijenge barabara kutoka morocco mpka mwenge

Samia: pesa za sherehe za muungano zigawanywe alafu mzitumie pale mnaona zinafaa.

my take; hela za shereh za muungano zilizopita hatujui zimetumikaje na wapi. Mafisadi washagawana. RIP JPM, you were a true leader
hii alisema kweli?
 
Hivi ni kwanini Tanzania hatutilii maanani mandhari ya nje majengo yetu? Dodoma tayari ni sehemu kame. Kwanini eneo kama hili lisipandwe bustani za maua na miti kila sehemu? BTW Hospital ni utaalaam na vifaa. Tutatoa pongezi iwapo patakuwa na madaktari wazuri na vifaa vya kutosha.
Ni kweli wangepanda miti sambamba na ujenzi huenda ingekuwa sawa na hayo mjani mawili hapo
 
Back
Top Bottom