Mfumuko wa bei nchini Marekani waathiri vibaya uchumi wa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111398785608.jpg


Ili kutatua changamoto ya mfumuko wa bei nchini Marekani, Benki Kuu ya nchi hiyo inayofahamika kama “Federal Reserve” imeongeza viwango vya riba mara sita tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo madhara yake kwa nje yameathiri vibaya uchumi wa nchi zinazoendelea hasa za Afrika, na gharama za maisha ya watu wa nchi hizo zimepanda kwa kasi.

Lewis Endishu, mchambuzi wa Taasisi ya Sera ya Afrika nchini Kenya amesema athari za serikali ya Marekani kuongeza viwango vya riba kwa mfululizo kwa Afrika zinaweza kuwa mbaya zaidi kuliko athari kwa sehemu nyingi za dunia, akikitaja kitendo hicho kuwa “cha kutowajibika”.

Tunajua kuwa nchi nyingi za Afrika zinategemea sana uagizaji wa vyakula na mafuta ghafi kutoka nje. Marekani kuongeza viwango vya riba kunaweza kuongeza thamani ya dola, kisha thamani za fedha za nchi nyingine zikashuka, jambo ambalo huongeza gharama za kuagiza vitu vinavyohitajika kutoka nje.

Kulingana na takwimu mpya zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya, mfumuko wa bei nchini humo ulifikia 9.6% mwezi Septemba, kiwango cha juu zaidi katika miaka mitano iliyopita. Mbali na Kenya, nchi nyingine za Afrika pia zinashuhudia mfumuko mkubwa wa bei.

Ili kupunguza mfumuko wa bei, nchi hizo hazina budi kuongeza viwango vya riba vilevile, na hivyo kusababisha mzunguko mbaya wa fedha sokoni na mwisho kasi ya ukuaji wa uchumi inaweza kupungua. Benki ya Maendeleo ya Afrika hapo awali ilitoa "Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Afrika wa mwaka 2022", ikikadiria kuwa wastani wa mfumuko wa bei barani Afrika utafikia 13.5% mwaka huu; kasi ya ukuaji wa uchumi wa Afrika mwaka 2022 inaweza kufikia 4.1%, chini ya 6.9% mwaka 2021.

Hali halisi ni kuwa mfumuko mkubwa wa bei unaotokea leo nchini Marekani ni matokeo mabaya ya sera mfululizo za ndani na nje za serikali ya Marekani katika miaka ya hivi karibuni. Mwanzoni mwa mwaka 2020, ili kukabiliana na athari za janga la COVID-19 na mtikisiko katika soko la kifedha, serikali ya Marekani ilitoa hatua mbalimbali za kuchochea uchumi na kuchapisha pesa nyingi bila kujali wasiwasi wa pande zote.

Hatua hii ilisababisha mzunguko mkubwa wa fedha katika soko la Marekani, na utoaji wa bidha ulizidi mahitaji, hali ambayo ilisababisha kupanda kwa bei ya bidhaa na mfumuko wa bei ukapanda juu. Lakini hii sio sababu pekee ya mfumuko wa bei wa Marekani kuendelea kuongezeka.

Katika miaka ya hivi karibuni, sera mfululizo za kupinga utandawazi, ikiwa ni pamoja na vita vya kibiashara, zilizopitishwa na Marekani zimeharibu kwa kiasi Fulani mnyororo wa utoaji bidhaa wa kimataifa, na pia kupandisha kiwango cha bei za bidhaa nchini Marekani.

Mashirika kadhaa ya washauri bingwa na taasisi za utafiti nchini Marekani zimekadiria kuwa iwapo Marekani itaondoa ushuru wote wa nyongeza uliowekewa kwa bidhaa za China, kiwango cha mfumuko wa bei nchini Marekani kitashuka kwa takriban asilimia moja. Wakati huo huo, serikali ya Marekani iliendelea kufanya uchochezi na kusababisha kuibuka kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine mwaka huu.

Baada ya hapo, Marekani pia iliiwekea Russia vikwazo, na kuathiri soko la nishati na vyakula duniani, na kusababisha kupanda kwa kasi kwa bei za nishati, vyakula na bidhaa nyingine duniani, na hatimaye kuzidisha shinikizo la mfumuko wa bei nchini Marekani.

Ndiyo maana, tunaona kuwa jaribio la serikali ya Marekani la kuhamasisha watu kuweka fedha benkini na kupunguza kiasi cha fedha sokoni sio tu kwamba haliwezi kutatua tatizo la mfumuko mkubwa wa bei wa ndani ya nchi hiyo, bali pia linaburuza nchi duniani kote. Kwa hiyo, kwa muda mrefu, wito wa "kuondoa matumizi ya dola" umekuwa wa juu, na wanasiasa na wachumi zaidi na zaidi wameanza kujadili hatua zinazowezekana.

Tukiangalia historia, mwishoni mwa miaka ya 1970, serikali ya Marekani iliwahi kuongeza viwango vya riba kwa kiasi kikubwa ili kukabiliana na mfumuko wa bei wa ndani ya nchi, na kusababisha mdororo mkubwa wa kiuchumi katika nchi zinazoendelea, na Afrika na Amerika ya Kusini zote zilishuhudia "muongo uliopotea". Sasa, Marekani inaunda mgogoro mwingine wa madeni unaoweza kutokea duniani. Ni wazi kuwa ubinafsi na ubabe ni rangi ya ndani Marekani isiyobadilika.

Mara inapokuwa katika matatizo, Marekani haizingatii madhara ya kitendo chake kwa nje hata kidogo. Hata hivyo, katika mchakato wa utandawazi wa leo, inaaminika kuwa madhara yataiendea Marekani yenyewe ndani ya muda mfupi. Wakala wa Kimataifa wa Ukadiriaji wa Mikopo Fitch hivi majuzi ilipunguza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa Marekani kwa mwaka 2023, kutoka 1.5% iliyotarajiwa Juni hadi 0.5%.

Fitch ilionya kwamba mfumuko wa bei uliokithiri na ongezeko kubwa la viwango vya riba vitaweka uchumi wa Marekani katika mdororo kuanzia msimu wa kuchipua wa mwaka 2023.
 
So what's the way forward and what about the Tanzanian economy, will it survive in the wake of the deteriorating global economy?
 
Back
Top Bottom