Naomba haya yaliotajwa hapo juu yaelezwe kwa undani
Yanayowahusu wanayajua, ushauri ni kama hayakuhusu waachie wenyewe yanayowahusu! . Usizungumzie yasiyokuhusu ili usiwakere yanayowahusu! .
Mfano mdogo ni huu, kuna watu wana imani ya kuamini kuwa Yesu ni Mungu! .
Wengine Yesu ni Mwana wa Mungu hivyo ni Mungu! .
Imani nyingine hakuna Mungu isipokuwa Allah Subhanahu wa ta'ala na Muhammed (SAW ) ni Mtume wao, hivyo kwao Yesu sii Mungu wala Mungu hana mwana! . Kitendo tu cha kusema Yesu sii Mungu, ni machukizo kwa waumini wa Yesu ni Mungu! ,hivyo kwa ushauri wa jf, kama Yesu hakuhusu awe ni Mungu au Sii Mungu, waachie wenyewe! .
Vivyo hivyo kwa wale wanaoamini kuwa Allah si Mungu bali ni shetani fulani na huyo mtume wake ni mtume wa shetani fulani, maadam hakuhusu, waachie wenyewe, huna sababu ya kutoa taarifa zitakazo kwaza imani za watu humu! .
Kila mtu awe huru kuamini anacho amini mfano mimi ni muumini wa dini yetu ya asili, hatuna mwisho wa idadi ya wanawake wa kuoa, sipaswi kubezwa katika hili na wala nisiitwe mpagani au dini yangu kubezwa kuwa ni dini ya kishenzi! , naweza kumloga mtu zile sehemu zake za. .. zihamie usoni, ya kiume ikae puani ya kike ikae mdomoni, ujione utaiweka wapi sura yako! ,msicheze na imani za watu! .
Pasco