Mfumo wa elimu ubadilishwe

Rosemary Stephen

New Member
Oct 22, 2019
3
5
Moja ya jambo ambalo linatakiwa kutiliwa mkazo kwa sasa ni namma ambavyo mfumo wetu wa utoaji elimu unavyoathiri vizazi vyetu hasa vijana.

Ni mfumo ambao unalenga sana kuwaandaa wanafunzi kuwa tegemezi na kuwa wavivu wa kujituma na kupambania ndoto zao.

Wanafunzi wanafundishwa tu wakazane na masomo ili wapate kazi nzuri ili walipwe mishahara na kuwa na pesa ya kujikimu na maisha. Hii imesababisha jopo kubwa la wahitimu wengi waliomaliza shule na vyuo kurandaranda mtaaani kwa kisingizio cha kusubiria ajira.

Vipaji na ndoto za vijana wetu wengi zimekufa kwa sababu ya mbegu mbaya waliyopandikizwa shuleni.Elimu yetu imejikita zaidi katika nadharia na sio vitendo, darasani tunafundishwa ujasiriamali lakini kiuhalisia hatuwezi hata kugundua fursa zilizotuzunguka na bado tunasubiria ajira. Unaangalia unawaza kwanini sasa tumesoma ujasiriamali na bado hatuna ajira?

Serikali inabidi ijipange kisawasawa ili kuboresha mfumo wa utoaji elimu kwa wanafunzi. Hii itapunguza matatizo mengi Sana kwenye jamii yetu pamoja na imani za kishirikina, uhalifu, biashara za mwili , ubakaji nk.
 
Back
Top Bottom