Mfumo Unapoingiza Nyoka: Swali katika Neno Lisemwalo

Mfumo Unapoingiza Nyoka: Swali katika Neno Lisemwalo

Jumba zuri: uteuzi wa Anne Kilango
Nyoka: Mapungufu ya Anne Kilango

Why so serious? Kateuliwa, alimeteua hajaridhika na utendaji wake, katengua uteuzi wake. Period. Finito. Nukta
Niliandika hili kabla ya habari za tengua hii na kwa hakika sikuwa namlenga Kilango.
 
12938251_10153518935351156_6483212126583419465_n.jpg
UKIKUTA NYOKA NDANI

Nawasalimu watani, wa mbali na wanyumbani,

Nina swali mawazoni, mnijibu asilani,

Yakikukuta jamani, utafanya jambo gani?

Ukikuta nyoka ndani, utaita seremala?


Wewe umepata nyumba, mtani ukahamia,

Si nyumba hiyo ni jumba, machoni linavutia,

Bustani zimepamba, ndege wazishangilia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita injinia?


Ulipoingia ndani, jumba ukafurahia,

Ukamuomba Manani, ulinzi kukujalia,

Jalali wetu Rabbani, kwake ukajiachia,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita polisi?


Ndipo ukakaa chini, mke na watoto pia,

Mmetulia sebuleni, na nne mmekunjia,

Kuangalia ukutani, kuna ufa wapitia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita daktari?


Kuangalia darini, kumbe dari linavuja!

Jikoni mpaka vyumbani, dalili haiko moja,

Furaha yako mtani, kumbe jumba ni kihoja,

Ukikuta nyoka ndani, utamtafuta nani?


Kuliinua zulia, kumbe sakafu ya vumbi!

Kichwa kinazungukia, kama mlewa ugimbi,

Hamaki imeingia, mpaka mawazo ya dhambi,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita wakwezi?


Kabla hujatulia, kelele unasikia,

Mama Chanya Analia, “kuna nyoka kaingia!”

Mbio ukakimbilia, kuokoa familia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya jambo gani?


Pale mlipohamia, nyoka alishahamia,

Mayai kajitagia, tena ni mayai mia,

Hivyo ni vinyoka mia, ni moja mia sikia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya nini kwanza?


Patashika imekua, pumzi inakutoka,

Hao nyoka utaua, au utachekacheka?

Uamuzi waujua, ni jasiri kuushika?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Utasema ni mfumo, nyoka ameutumia,

Nyoka kaingia humo, mfumo umeachia,

Utaanza toa somo, mfumo kuangalia?

Ukikuta nyoka ndani, utaziba nyufa kwanza?


Utaita seremala, waliangalie paa?

Ati nyoka wamelala, mzima una kichaa?

Utafanya masihala, ulale mzime taa?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza piga maombi?


Nyoka muondoe nyoka, kabla kugeuka joka,

Mkirembesha hakika, mtageuka mahoka,

Mazuri unayotaka, mpaka nyoka katoka,

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Beti zangu nazifunga, kusema nimeshasema,

Anayetaka kupinga, apinge hii hekima,

Kama hajui kutunga, mashairi si lazima,

Ukikuta nyoka ndani, wewe utafanya nini?


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Aprili 11, 2016
kwa mwendo huu wa jpm chadema R.I.P 2020
 
12938251_10153518935351156_6483212126583419465_n.jpg
UKIKUTA NYOKA NDANI

Nawasalimu watani, wa mbali na wanyumbani,

Nina swali mawazoni, mnijibu asilani,

Yakikukuta jamani, utafanya jambo gani?

Ukikuta nyoka ndani, utaita seremala?


Wewe umepata nyumba, mtani ukahamia,

Si nyumba hiyo ni jumba, machoni linavutia,

Bustani zimepamba, ndege wazishangilia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita injinia?


Ulipoingia ndani, jumba ukafurahia,

Ukamuomba Manani, ulinzi kukujalia,

Jalali wetu Rabbani, kwake ukajiachia,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita polisi?


Ndipo ukakaa chini, mke na watoto pia,

Mmetulia sebuleni, na nne mmekunjia,

Kuangalia ukutani, kuna ufa wapitia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita daktari?


Kuangalia darini, kumbe dari linavuja!

Jikoni mpaka vyumbani, dalili haiko moja,

Furaha yako mtani, kumbe jumba ni kihoja,

Ukikuta nyoka ndani, utamtafuta nani?


Kuliinua zulia, kumbe sakafu ya vumbi!

Kichwa kinazungukia, kama mlewa ugimbi,

Hamaki imeingia, mpaka mawazo ya dhambi,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita wakwezi?


Kabla hujatulia, kelele unasikia,

Mama Chanya Analia, “kuna nyoka kaingia!”

Mbio ukakimbilia, kuokoa familia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya jambo gani?


Pale mlipohamia, nyoka alishahamia,

Mayai kajitagia, tena ni mayai mia,

Hivyo ni vinyoka mia, ni moja mia sikia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya nini kwanza?


Patashika imekua, pumzi inakutoka,

Hao nyoka utaua, au utachekacheka?

Uamuzi waujua, ni jasiri kuushika?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Utasema ni mfumo, nyoka ameutumia,

Nyoka kaingia humo, mfumo umeachia,

Utaanza toa somo, mfumo kuangalia?

Ukikuta nyoka ndani, utaziba nyufa kwanza?


Utaita seremala, waliangalie paa?

Ati nyoka wamelala, mzima una kichaa?

Utafanya masihala, ulale mzime taa?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza piga maombi?


Nyoka muondoe nyoka, kabla kugeuka joka,

Mkirembesha hakika, mtageuka mahoka,

Mazuri unayotaka, mpaka nyoka katoka,

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Beti zangu nazifunga, kusema nimeshasema,

Anayetaka kupinga, apinge hii hekima,

Kama hajui kutunga, mashairi si lazima,

Ukikuta nyoka ndani, wewe utafanya nini?


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Aprili 11, 2016


Nyoka alihamia, kabla yakuhamia.
Nini unatarajia, nyoka kumfanyia.
Nyoka alizaa, hata kajijukulia
Nyoka mameenea.hadi kufika mia.

Waite wajenzi nyumba kuibomoa.

Nyoka wamejazana,wasije kukuua.
Nyoka watazaliana,mia mara mia.
Nyoka, tujiulize wapi waliingilia?
Nyoka walipenya nyufa zilizoachia.?

Waite wajenzi mfumo ulikosewa

Nyumba imejaa nyufa hadi dari pia
Nyumba inazulia vumbi limejaa
Nyumba ilikosewa haikusakafiwa.
Nyumba hukuigagua kabla kuhamia.

Waite wajenzi mfumo kuuondoa.
 
Mtumbu mtumbua, atumbu atumbuani?
Mtambu mtambua, atambu atambuani?
Agundu agundua, dira i mahali gani?
Mihemuko ya kuzua, mizuka ya ngomani?

Atamba atumbua, yeye atamtumbuani?
aibu kuziibua, zake atazisemani?
Mizungu keshaijua, lelele za siasani?
Mihemuko ya kuzua, mizuka ya ngomani?

Njia mmeshajua, twaenda mahali gani?
Safari si kitumbua, au kula biriani
Au tende na halua, au togwa harusini
Mihemuko ya kuzua, mizuka ya ngomani?

Almaaruf fufufu, almajnun fununu
wafu wawazike wafu, wanu wawazike wanu
Unyoofu si ukengefu, kucheza kimanumanu
Mihemuko ya kuzua, mizuka ya ngamani?
 
Kuna watu ni kama wameamua kusimama tu upande wa kupinga (si kuwa upinzani) ....wengine kila MM akiandika makala wanakimbilia kutoa comments za kupinga na kejeli juu bila hata wakati mwingine kusoma ujumbe wote zaidi ya heading. Kuna wengine tena na heshima zao humu utacheka wanachoandika ili kumpinga MM ....kama hujui watu wa humu hasa wakongwe na mtiririko wa hoja zao na jinsi walivyoamua kuhamisha magoli kihoja kufix malengo yao wanachekesha mno ....
Bila shaka wanatumia haki yao ya kutoa maoni
 
Mfumo uliingiza Chatu toka Chato, Ambaye anameza grass snake na kuua rattle snake. Boma lote lina aina zote za nyoka wenye sumu na waso na sumu, wenye makengeza na wenye vichwa saba.
 
Mtumbu mtumbua, atumbu atumbuani?
Mtambu mtambua, atambu atambuani?
Agundu agundua, dira i mahali gani?
Mihemuko ya kuzua, mizuka ya ngomani?

Limeulizwa swali, swali halijibu swali,
Unaenda wapi swali, vipi uulize wali?
Swali lahusu mahali, unaleta ya bakuli?
Swali lisipojibiwa, swali linabaki swali!

MMM
 
Nyoka alihamia, kabla yakuhamia.
Nini unatarajia, nyoka kumfanyia.
Nyoka alizaa, hata kajijukulia
Nyoka mameenea.hadi kufika mia.

Waite wajenzi nyumba kuibomoa.

Nyoka wamejazana,wasije kukuua.
Nyoka watazaliana,mia mara mia.
Nyoka, tujiulize wapi waliingilia?
Nyoka walipenya nyufa zilizoachia.?

Waite wajenzi mfumo ulikosewa

Nyumba imejaa nyufa hadi dari pia
Nyumba inazulia vumbi limejaa
Nyumba ilikosewa haikusakafiwa.
Nyumba hukuigagua kabla kuhamia.

Waite wajenzi mfumo kuuondoa.

Wajenzi Kuibomoa, Kubomoa kwa Ghalama.
Huu kweli ukichaa,Ukichaa wa kiyama
Utaja kuja kulia, Kushindwa hiyo ghalama
Pili pili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Ukiwa hujui Juzwa, Juzwa kisha uelewe
Nyoka apenda maziwa, Pilipili Yakera we
Wajenzi watauliwa,Hilo sasa uelewe
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Uchunguzi wachunguzwa, Huku nyoka kauawa
Mfumo mpya kuundwa,Si Nyumba Kubomolewa
Ziba nyufa sawa sawa, Taa mpya kuwekewa
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Joka lile Joka kubwa, Limefugwa kwa Jirani
Tena sasa Linatumwa, Kuja kuwatishieni
Sasa hivi la nyonyeshwa, Wewe unafanya nini?
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Tamati nimefikia, Karamu chini naweka
Najua umesikia, Ukifumba watacheka
Dawa umeshaijua, Siyo Nyumba kubomoka
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza
 
Hahahahahahaaaa, sicheki kwamba nacheka
Kicheko cha kushangaa, ukweli nimeudhika
Lijoka lilivyokaa, na mirija likaweka
Kuliua joka hilo kawaite zimamoto

Usiite daktari yeye kazi yake tiba
Majirani ni hatari, waweke pembeni baba
Joka lina mistari, limesheheni si haba
Kuliua joka hilo kawaite zimamoto

Na watoto wake shida, hujui yupi ni mwema,
Kila inompa shada, Mwizi wa Mali ya umma,
Labda zidisha ibada, joka kaharibu Boma
Kuliua joka hilo kawaite zimamoto

Wengine watakubeza, funga masikio wewe
Nyufa zote ukiziba, watajitaja wenyewe
Kazi utaimaliza, wameshapata kiwewe,
Na Zimamoto unalo, kwa nini uhangaike?
 
Fukunyua Fukunyua, Mayai kuyavunja
Tumbua tena Tumbua, Fundi wa nini Kungoja?
Pangua Panga Pangua,Mfumo Kuwa mmoja
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?

Nyani wataka Kuua, Uso watazamiani?
Utaja vuna mabua, Huruma weka pembeni
Tanzu na kuzitanzua,Huruma si Marekani
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?

Zenji huko uzenjini, Vijibweka vyavumako
Rungu unalo la nini? Gonga gongako kunako
Mirija mirijanini, Kukata na kukatako
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?

Posho zile Mjengoni, Posho ni za kiduwanzi
Una nini mkononi, Tumbua bila na ganzi
Ili wakija mwakani, Kura kuomba kwa kazi
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?

Joka lile la milia, Na vitoto vya mikia
Upupu baba tumia, Na sifongo kuulia
Wasema eti sheria, Hao wanatutania
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?

Sakamanya sakamanya, Manyanga watayabwaga
Mianya hii Mianya,Ni kuziba na kufunga
Tapanya wali Tapanya,Vitambi walivimbaga
Rungu umepewa baba, Subira ya nini tena?
 
Ukikuta nyoka ndani, utaita seremala?
Kwani Kuna nyoka seremala.Wote nyoka wanatofautiana ukubwa.Hujawahi kusikia big fish eating the small fish.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom