Mfumo Unapoingiza Nyoka: Swali katika Neno Lisemwalo

Mfumo Unapoingiza Nyoka: Swali katika Neno Lisemwalo

Kwani Kuna nyoka seremala.Wote nyoka wanatofautiana ukubwa.Hujawahi kusikia big fish eating the small fish.
Nina swali mawazoni, mnijibu asilani,

Yakikukuta jamani, utafanya jambo gani?

Ukikuta nyoka ndani, utaita seremala?
 
Kosa kubwa alilolifanya bwana mkubwa na ambalo litaendelea kukitafuna hata kizazi cha pili cha utawala wake ni kuendeleza ndoa za mitara za iliyokuwa ndoa ya mtangulizi wake...Yes! Kulikuwa na sababu gani basi kuendeleza mfumo wa kubebana ikiwa naye alikuwa kwenye cabin ile ile na aliwajua kwa majina na utendaji wao?

Nionavyo tayari wateule wake wameshakuwa wapiga zumari na probably wanachofanya ni kupiga wimbo aupendao aliyewapa kazi ya kupiga zumari,hata kama wanajua fika kwamba rhythm ya wimbo husika haiendani na mazingira halisi ya sasa!
 
Kuna watu ni kama wameamua kusimama tu upande wa kupinga (si kuwa upinzani) ....wengine kila MM akiandika makala wanakimbilia kutoa comments za kupinga na kejeli juu bila hata wakati mwingine kusoma ujumbe wote zaidi ya heading. Kuna wengine tena na heshima zao humu utacheka wanachoandika ili kumpinga MM ....kama hujui watu wa humu hasa wakongwe na mtiririko wa hoja zao na jinsi walivyoamua kuhamisha magoli kihoja kufix malengo yao wanachekesha mno ....

You have a point!

Akiandika kiswahili cha kawaida hawaelewi. Sasa MM kaja na fasihi imekuwa majanga. Tatizo watu wa FB wengi sana humu ndani.

Wapumbnavu siku zote hawaoni hoja. Wanaangalia nani kaandika. Hoja ile ile ingeandikwa na rafiki zao ungeona likes kibao au kuunga mkono.

Binafsi, nina watu huwa tunapishana sana kwenye hoja. Lakini nikiona mantiki kwenye postings nyingine sioni tabu kuunga mkono au kushadidia.

Tujikite kwenye hoja, sio nani kaandika!
 
Kwani Kuna nyoka seremala.Wote nyoka wanatofautiana ukubwa.Hujawahi kusikia big fish eating the small fish.

Emusisi unataka, Ushoga unautaka?
Jitegemea wataka, Misaada pia wataka
Wewe hivi mburucheka, unashindwa eleweka
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua

Aliye nacho anacho, Asiye nacho si kitu
Hata ukitoa macho, Sikitu huwa sikitu
Kile we ulicho nacho, Bepari kitu ni kitu
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua

Seremala wamtaka, Wakati joka li ndani
Hapa umeshachemka, Seremala ni wa nini?
Mwaga sumu ya majoka,Acha utani Jirani
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua

kijiji hiki ni chetu, Kwanini wafuga joka?
Jirani huyu ni chatu, Na uache kushoboka
Huyu anameza watu, Joka asiye fugika
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua

Anatabia za Swila, Kugonga gonga gizani
Anajfanya anamila, Kumbe joka li kazini
Kanisani kwenye sala, Pia na msikitini
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua

Ulisema huyu nyoka, Kwa nini unamfuga?
Au kitu ulitaka, Watu sisi kuvuruga
Achananao utata, Kijiji chetu kujenga
Mtoto wa nyoka nyoka, Dawa yake ni kuua
 
12938251_10153518935351156_6483212126583419465_n.jpg
UKIKUTA NYOKA NDANI

Nawasalimu watani, wa mbali na wanyumbani,

Nina swali mawazoni, mnijibu asilani,

Yakikukuta jamani, utafanya jambo gani?

Ukikuta nyoka ndani, utaita seremala?


Wewe umepata nyumba, mtani ukahamia,

Si nyumba hiyo ni jumba, machoni linavutia,

Bustani zimepamba, ndege wazishangilia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita injinia?


Ulipoingia ndani, jumba ukafurahia,

Ukamuomba Manani, ulinzi kukujalia,

Jalali wetu Rabbani, kwake ukajiachia,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita polisi?


Ndipo ukakaa chini, mke na watoto pia,

Mmetulia sebuleni, na nne mmekunjia,

Kuangalia ukutani, kuna ufa wapitia,

Ukikuta nyoka ndani, utaita daktari?


Kuangalia darini, kumbe dari linavuja!

Jikoni mpaka vyumbani, dalili haiko moja,

Furaha yako mtani, kumbe jumba ni kihoja,

Ukikuta nyoka ndani, utamtafuta nani?


Kuliinua zulia, kumbe sakafu ya vumbi!

Kichwa kinazungukia, kama mlewa ugimbi,

Hamaki imeingia, mpaka mawazo ya dhambi,

Ukikuta nyoka ndani, utawaita wakwezi?


Kabla hujatulia, kelele unasikia,

Mama Chanya Analia, “kuna nyoka kaingia!”

Mbio ukakimbilia, kuokoa familia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya jambo gani?


Pale mlipohamia, nyoka alishahamia,

Mayai kajitagia, tena ni mayai mia,

Hivyo ni vinyoka mia, ni moja mia sikia,

Ukikuta nyoka ndani, utafanya nini kwanza?


Patashika imekua, pumzi inakutoka,

Hao nyoka utaua, au utachekacheka?

Uamuzi waujua, ni jasiri kuushika?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Utasema ni mfumo, nyoka ameutumia,

Nyoka kaingia humo, mfumo umeachia,

Utaanza toa somo, mfumo kuangalia?

Ukikuta nyoka ndani, utaziba nyufa kwanza?


Utaita seremala, waliangalie paa?

Ati nyoka wamelala, mzima una kichaa?

Utafanya masihala, ulale mzime taa?

Ukikuta nyoka ndani, utaanza piga maombi?


Nyoka muondoe nyoka, kabla kugeuka joka,

Mkirembesha hakika, mtageuka mahoka,

Mazuri unayotaka, mpaka nyoka katoka,

Ukikuta nyoka ndani, utaanza kulaumu?


Beti zangu nazifunga, kusema nimeshasema,

Anayetaka kupinga, apinge hii hekima,

Kama hajui kutunga, mashairi si lazima,

Ukikuta nyoka ndani, wewe utafanya nini?


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Aprili 11, 2016
Siiti yoyote kati ya hao uliowataja, bali nitamuua.

Ndicho afanyacho anko magu.
 
Yu wapi joka msaka pesa, yule mwenye makengeza?
Sisahau alivyotutesa, kisa kujipendekeza.
Nasasa arudishe pesa, zile alizowekeza.
Naenda kuita Polisi, Nimekuta joka ndani.

Vile anamakengeza, huyu ni wa kuanza nae,
Hakawii kujigeuza, Tukadhani ni mwanae,
Mwisho tukashangaza, pesa tena zisifae
Bora kuita polisi, Huyu Joka atoke ndani.

Wapo wengi washenzi, Tena nyoka wa kijani
mababu tangu enzi, mbinu zao wazi juani
Wametufanya mapenzi, mimba tumesheheni
Daktari sasa aje, bora kumuita yeye.
 
Tunakula vitumbua, Muda wa kutumbuana.
Nyoka atajinasua, vumbi mwisho kurushiana.
Matokeo ni mabua, manyani twatambuana.
Dawa yake tu kuua, ndani nyoka ukikuta.

Kizazi cha nyoka tumechoka, kije cha mjusi tunywe juisi.
Mabazazi bila kuchoka, eti si nyoka bali simbilisi.
Mambo hayo tushachoka, nyie nyoka sie mijusi.
Kwanini aitwe ulimboka, wakati nyoka si mjusi
 
Anza kwa kumuua nyoka halafu bomoa nyumba anza kujenga nyumba uipendayo
 
Daktari sasa yupo, Daktari wa kemia
Hataki pima upepo, Yeye ni kuyatumbua
Yeye ajua yalipo,Na sasa kajitolea
Nyoka hawa ni wajanja, Bora kuweka mitego

Pili pili ukichoma, Yatatoka mashimoni
Mitego iweke vyema,Na yafunge gerezani
Hata wakisema sema, Ulaya na marekani
Nyoka hawa ni wajanja, Bora kuweka mitego

Swila yupo kitandani, Chunga huyo ni mweusi
Usije leta matani, Bora uwe na murusi
Nenda huko uchinani, Wa magharibi mafisi
Nyoka hawa ni wajanja, Bora kuweka mitego

Wamakengeza wasema, Wasemaje mwenyemvi?
Hili jeupe Jinyama, Limesha taga viwavi
Dawa yake ni kuchoma, Na kuondoa ugomvi
Nyoka hawa ni wajanja, Bora kuweka mitego
 
Joka linawakilisha milionea Lowassa au watu wenye tabia mbaya kwenye jamii.Ndicho nilichojifunza kwenye shairi.Waliotetea joka walilaumu mfumo.Walilaumu mfumo ili joka lionekane halina hatia.
 
Mimi kama mwananchi wa kawaida naona kuna kitu kinatakiwa kufanyika kwa ushirikiano wa pamoja......
Hii nchi ni ya wote siyo ya wachache.
Naona tatizo ndani yetu watanzania TUMERUHUSU AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA! Ifike sehemu tujitathimini!
 
Wajenzi Kuibomoa, Kubomoa kwa Ghalama.
Huu kweli ukichaa,Ukichaa wa kiyama
Utaja kuja kulia, Kushindwa hiyo ghalama
Pili pili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Ukiwa hujui Juzwa, Juzwa kisha uelewe
Nyoka apenda maziwa, Pilipili Yakera we
Wajenzi watauliwa,Hilo sasa uelewe
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Uchunguzi wachunguzwa, Huku nyoka kauawa
Mfumo mpya kuundwa,Si Nyumba Kubomolewa
Ziba nyufa sawa sawa, Taa mpya kuwekewa
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Joka lile Joka kubwa, Limefugwa kwa Jirani
Tena sasa Linatumwa, Kuja kuwatishieni
Sasa hivi la nyonyeshwa, Wewe unafanya nini?
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza

Tamati nimefikia, Karamu chini naweka
Najua umesikia, Ukifumba watacheka
Dawa umeshaijua, Siyo Nyumba kubomoka
Pilipili Kuichoma, Moshi utawafukuza
Hilo joka liko nje, Mazalia yako ndani,
Kwa nini nyumba usivunje, Kuua yaliyomo ndani?,
Tungesema tuwakunje, Siyo samaki yakini,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Mazalia ndiyo mengi, Tena yana sumu kali,
Yamejaa kwa wingi, yakiwa na hasira kali,
Ndani yameweka msingi, Yamejenga kwa jabari,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Yanakula na kujinywea, Vitu vya watu wa ndani,
Yanatapa pakutokea, Mjenzi u wapi jamani,
Uhuru yamejitwalia, Hayajifichi yako hadharani,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Yaliyo ndani tuyaue, La nje likafie mbali,
Twapaswa tuyatambue, Yasije kuwa jabali,
Bati mpya tujitwalie, Tuezeke kwenye dali,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?
 
Hilo joka liko nje, Mazalia yako ndani,
Kwa nini nyumba usivunje, Kuua yaliyomo ndani?,
Tungesema tuwakunje, Siyo samaki yakini,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Mazalia ndiyo mengi, Tena yana sumu kali,
Yamejaa kwa wingi, yakiwa na hasira kali,
Ndani yameweka msingi, Yamejenga kwa jabari,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Yanakula na kujinywea, Vitu vya watu wa ndani,
Yanatapa pakutokea, Mjenzi u wapi jamani,
Uhuru yamejitwalia, Hayajifichi yako hadharani,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Yaliyo ndani tuyaue, La nje likafie mbali,
Twapaswa tuyatambue, Yasije kuwa jabali,
Bati mpya tujitwalie, Tuezeke kwenye dali,
Joka liloacha nyumba, Ya nini kusumbuka?

Joka kweli liko nje, limeacha mazalia
Kwa jirani lafanyaje, Kwani wamelipokea
Inabidi walichinje,Kwani litatusumbua
Sumu ya nyoka umwage, Utaua mazalia

Kuvunja nyumba Unyumbu, Utakuwa ni kituko
Sisi sio mambumbumbu, Tunajua tutokako
Si tunazo kumbukumbu, Tunajua tuendako
Sumu ya nyoka umwage, Utaua mazalia

Viringisha viringisha, Urimbombo Urimboni
Mitego tega tegesha, Sebuleni na chumbani
Dondosha kote dondosha, Pili pili mashimoni
Sumu ya nyoka umwage, Utaua mazalia

Vifutu je wawajua? Sio kama wale swila
Wanatulia tulia, Kumbe ndani wanakula
Hawa si wakuchekea, Ni bora we uwe kila
Sumu ya nyoka umwage, Utaua mazalia
 
Nyoka hawa waongea, Si ndiyo haya majipu
Dawa ni kuyatumbua, Yasije leta upupu
Ukicheka we tambua, Yatakufanya mtupu
Haya majipu tumbua, Yatumbue kweli kweli
Tena wewe ukishindwa tuite tukusaidie,hawa tumewachoka wametufanya tulie. Huku wao wakicheka kwanini sisi tuugulie,Tena nchi yetu sote kwanini mali zote wajivunie. Nikikukuta ndani nyoka lazma moto niutie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom