Kwa mtazamko wangu mfumo jike ukiimarika bado hauwezi kumsaidia mwanamke kujikomboa . Hii inatokana na kwamba mwanamke aliyeko mbali na mji si rahisi kumfikia kumbuka harakati hizi zina mapungufu mengi. Nakumbuka wakati flani niliona mwanamke ameonewa ie ameumizwa na mumewe hata kusababishiwa ulemavu . Basi taasisi flani ilikwenda kumuona mwanamke yule na ikachukua picha lkn haikufanya chochote zaidi ya taasisi yenyewe kupata mtaji kwa kutumia zile picha .
Sasa hizi harakati za ukombozi wa mwanamke zimezungukwa na waroho so kumfikishia elimu mlengwa itakua kazi sana. Mwaname anaeteseka au anaehitaji ukombozi hasa ni yule aliyeko kijijni mwenye majukumu mengi ikiwemo watoto na wengine kama hao. Mwanamke anayehitaji kuelimishwa ni yule anaeteseka peke yake kuitunza familia baba yuko kwenye ulabu. Mimi bado nina mashaka na hizi harakati za ukombozi wa mwanamke toka kwenye mfumo kandamizi. Unajua kwa sababu gani huyu mwnamke anahitaji kuelimishwa namna mfumo dume unavyomkandamiza na faida za ukombozi . Sasa kama wahusika wanatazama kiendacho kinywani itakua ngumu kuufikia ukombozi na hatimaye utabaki kwenye makaratasi na maofisini bila kusahau safari za ulaya na makongamano mbali mbali.
Nahitimisha kwa kusema itachukua muda mrefu mfumo jike kuimarika na naiona kama nightmare.Pia elimu yoyote inapotolewa inatakiwa ieleze faida na hasara za mfumo dume na mfumo jike. Ni vema walengwa wakapewa elimu juu ya pande zote mbili na mwisho mwanamke na mwanaume afundishwe kuishi kwa kuchanganya mifumo yote miwili kwani ukiishi kwa kufuata mfumo mmoja tu lazima patakua na mapungufu na mwisho tena tutaanza harakati za kumkomboa mwanaume.
++
asante sana sasa sijui mfumo huo utazaliwa vipi? Tutauitaje.....
++
you are real great thinker. We waache wapigew kelele we wasijishughulishe na kusoma na kufanya kazi waendelee kuwategemea wanaume halafu wategemee kuondokana na mfumo dumewanawake mnadai haki kwenye makaratasi
fanyeni kazi muone kama hamtautokomeza mfumo dume kimya kimya.
++Lakini ukikanyagwa lazima useme umeumia Pengine si kelele ni kutaka kusikika?++you are real great thinker. We waache wapigew kelele we wasijishughulishe na kusoma na kufanya kazi waendelee kuwategemea wanaume halafu wategemee kuondokana na mfumo dume
++Na je jitihada hizi zikifika kijijini Itakuwa mfumo jike unaondoka?++Tatizo nilionalo kwa hao wanaotetea mfumo jike kuwa unakandamizwa hakuna la maana walilolifanya kuhakikisha kuwa kuwa wanatetea kile wanachokisema. hakuna uhalisia wala hakuna mtetezi wa hao wanaosemwa kuwa wanateseka kwa kuwepo mfumo dume ila wanaongelea jukwaani tuu na kwenye makaratasi na semina na warsha na makongamano kibao ila ukweli halisi hakuna wanalofanya kumtetea mwanamke anayenyanyasika tena wa kijijini ambako hizo warsha na semina hazifikiYaani imekuwa ni biashara ya kutafuta fedha za wafadhili mbalimbali ila hakuna uhalisia wa kumtetea mwanamke ambaye anahangaika kule kijijini Na inafikia mpaka unaona kuwa hao watetezi wanamjua mwanamke wa mjini tuu ndo maana wanatumia muda na resources nyingi kumtetea huyo wa mjini na wanasahau wanaonyanyasika kwa wingi wako kijijini ambako hata mawasiliano hakuna