Mfumo dume umejikita kama tattoo mwilini

Mfumo dume umejikita kama tattoo mwilini

SANUKA Na Dk Levy

New Member
Joined
May 21, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Wanawake wanaojiuza hupewa majina mabaya. Kama malaya, changudoa, vicheche, milupo na mengineyo. Wanaume ambao ni wanunuzi huonekana ni wajanja wa wa 'tauni' wanaojua chimbo zote za wajasiriamili hao wa kike.

Thamani ya bikira ni kwa mtoto wa kike tu, wa kiume akitoka na 'demu' umri wa shangazi yake huonekana kashujaa flan hivi. Na binti akipata ujauzito wazazi hukasirika tofauti na wa kiume akimpa ujauzito msichana.

Wazazi hawapendi mtoto wa kike awe na "boi frendi', ila wa kiume akiwa na 'gero frendi' familia yote huchekelea. Ndoa inapovunjika lawama ni kwa mwanmke, mara kaachika, au ndoa imemshinda hata kama huyo mwanamke ndo kamuacha mumewe.

Dada akiona dogo lake la kiume lina 'gero frendi' hakasiriki. Lakini dogo la kiume likiona dada yake ana 'boi frendi' hukasirika sana.

Kaka anaweza kumtuma dada amuunganishie rafiki yake. Lakini ni vita kwa kaka mtu kutoa pasi dada yake kwa masela.

Mwanaume akiwa na wapenzi wengi ni rijali, mwanamke akiwa naa wapenzi wawili tu ni malaya. Uswahilini hata dada ambaye tayari kazalishwa, bado ndugu wa miume wanaumia wakiona yuko na kidume. Na 'samtaimu" ngumi zinatembea.

Hii ni athari ya mfumo dume. Ni wazi Afrika, suala hili ni kama mtu aliyejichora tatuu, haifutiki. Achana na 'jenda balansi' katika ajira na ushirikishwaji kwenye maamuzi mengi. Pia vitabia hivi vidogo vidogo vinautukuza sana mfumo dume.
 
Back
Top Bottom