SoC02 Mfumo Huru wa Kompyuta wa Kupigiana Kura. Jina La Mfumo: Fair Election (FAEL)

Stories of Change - 2022 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
995
1,508
UTANGULIZI
Katika Dunia nzima, nchi zote hufanya chaguzi zake ili kupata viongozi wake wa ngazi tofauti tofauti kupitia mfumo wa kupiga kura za mficho. Njia inayotumika kwa sasa nyingi huwa zinasababisha wizi wa kura, gharama kubwa za usimamizi wa uchaguzi, maafa kwa wasimamizi wa uchaguzi na mengine mengi.

Huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo teknolojia imebeba majibu mengi sana,hivyo nimeamua kuleta wazo la kuunda mfumo ambao utatumika kuendesha uchaguzi mkuu.

Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kuratibu uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani katika maeneo yote ndani ya nchi husika.

Mfumo utaratibiwa na kuongozwa na tume huru ya uchaguzi ya nchi husika ama chombo chochote chenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi.

NAMNA MFUMO UTAKAVYO ONEKANA.
Mfumo utakuwa na dashibodi itakayoonesha;
  1. Waangalizi wa uchaguzi kutoka mataifa tofauti, hapa utaweza kuona majina ya waangalizi wa uchaguzi kutoka mataifa mbalimbali ambao kazi yao huwa kuangalia mwenendo wa uchaguzi kama ni wa haki, na wao wataweza kuingia kwenye akaunti zao kupitia hapo.
  2. Nafasi za wagombea (Rais na Makamu wake, Wabunge na Madiwani) ambapo ukifungua sehemu ya Rais, Mbunge ama Diwani utaweza kuona taarifa zake muhimu na wao wataweza kuingia kwenye akaunti zao kupitia hapa.
  3. Majimbo ya uchaguzi, Idadi ya majimbo ya uchaguzi, kata na idadi ya wapiga kura, hapa mtu ataweza kuona majimbo na kata zoote za uchaguzi, mkoa yalimo, idadi ya wapiga kura katika jimbo hisika.
  4. Wasimamizi wa uchaguzi, hapa utapata majina ya wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vyote nchini na vituo wanavyosimamia.
  5. Ulinzi na usalama, hapa utapata idadi ya polisi watakao husika kusimamia uchaguzi na vitendea kazi.

NAMNA MFUMO UTAKAVYO RATIBU ZOEZI LA UPIGAJI KURA.
Mfumo utakuwa wa wazi sana, kupitia mfumo huu, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndiye atakayekuwa “ADMINISTRATOR MKUU” pekee, katika mfumo wa uendeshaji kutakuwa na na waendeshaji wa mfumo kadhaa kutoka Tume ya uchaguzi ambao watakuwa na uwezo wa kuingiza taarifa za wagombea, wapiga kura, waangalizi wa uchaguzi, na wasimamizi wa uchaguzi, ambapo taarifa zikisha ingizwa na kuhifadhiwa muendeshaji yeyote hatoweza kubadili isipokuwa kwa idhini ya administrator mkuu.

Mfumo utamtambua mpiga kura kwa alama za vidole tu ambapo ambapo atakuwa tayari alishasajiriwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia BVR. Wagombea wote wataweza kuingia katika majina ya wagombea na kuona taarifa zao na kupitia hapo ataweza kuingia kwa kodi maalumu ambayo itatengenezwa na mfumo pasipo upande wowote kujua, kupitia kodi hiyo ataweza kuingia na kuona wapinzani wake katika nafasi husika na idadi ya kura zinazogombaniwa kwa ujumla.

Chini ya kila picha kutakuwa na sehemu inayoonesha idadi ya kura alizo pigiwa muhusika tu, kwa wengine itaonesha kimvuli, hii itasaidia mgombea kutathmini mwenendo wa kura anazopigiwa, kura zitakuwa zinajihesabu "automatically".

Kwenye vituo vyote kutakuwa na msimamizi wa uchaguzi ambaye kazi yake itakuwa ni kumuelekeza mpiga kura namna ya kupiga kura kupitia kioo ambapo eneo la kupigia kura kutakuwa na pande mbili(wakupigia kura(Voting side) na wakutolea maelezo (demonstration side),kwa kuwa mpiga kura atakuwa amekwisha elekezwa, msimamizi atamzungusha mpigakura upande wa pili(voting side) kisha yeye atarudi demo side, huko atagusa kitufe kitakachokuwa kina ruhusu mtu kupiga kura, akigusa tu, mpiga kura ataona picha za wagombea kwa awamu ambapo kwa mara ya kwanza itatokea picha cha Rais na makamu wake kwa vyama vyote, na nembo za vyama husika kwa pembeni.Mpiga kura atatakiwa kugusa picha ya mgombea anaye mtaka kwa sekunde kadhaa kwa kutumia kidole,ili mfumo umtambue mpiga kura, ikimaliza itatiki na kupotea na kuingia ngazi ya Mbunge kisha Diwani., akimaliza screen itajifunga yenyewe nakutoa mlio katika lugha itakayokuwa imesetiwa ikiwa na maana kwamba ”HONGERA UMEMALIZA KUPIGA KURA YAKO”, wakati huo msimamizi atakuwa anaona upande wa pili hatua aliyofikia mpiga kura lakini hatakuwa na uwezo wakujua kampigia kura nani.Ila wagombea wataweza kuona jumla ya kura anazopigiwa kwa kila kituo,na jumla kuu.

Kila kituo cha uchaguzi kitakuwa na “CCTV CAMERA” ambazo zitatumia mtandao, kamera hizo zitaonesha matukio yote eneo husika na zitakuwa zimeunganishwa moja kwa moja katika chumba maalumu chakuendeshea uchaguzi ofisi za tume ya uchaguzi lakini pia, wagombea wote kwenye akaunti zao wataweza kuona kadhalika na waangalizi wa uchaguzi nao wataweza kushuhudia mwenendo wa uchaguzi kupitia mfumo huo kwa msaada wa kamera hizi, ikitokea kamera moja imesitishwa kufanya kazi basi hakuna kura itaweza kuhesabiwa kutoka katika kituo husika mpaka pale itakaporekebishwa na kila mgombea, tume na waangalizi huru watapata taarifa kupitia mfomo huo katika kitufe cha “NOTIFICATION” ambacho kitakuwa maaluma kulingana wa wahusika.

Mfumo huu utaweza pia kumruhusu mpiga kura kupiga kura kupitia simu janja kwa njia ya “APPLICATION YA TUME UCHAGUZI TOKA PLAY STORE” kwa utaratibu ule ule,na sharti ni lazima simu iwe ya mpiga kura,haitaweza kuruhusu kupiga kura zaidi ya mtu mmoja.

KURA JUMUISHI.
Kura jumuishi zitafanywa na mfumo wenyewe kwa kila mgombe na ujumuishi huo utafanyika baada ya wasimamizi wa vituo vyote kutuma ripoti yakumaliza zoezi katika kituo husika, hakutakuwa na uwezo wa kurekebisha matokea kwa mtu yeyote Yule, na muda ukifika, basi wagombea wote kwenye akaunti zao ndio wataweza kuona idadi ya kura kwa kila mgombea mwingine hivyo kujua kwa urahisi kama ameshinda ama ameshindwa. Matokeo yote yataonekana katika website ya tume huru ambayo yatatumwa na mfumo wenyewe baada ya muda uliokuwa umewesetiwa kukamilisha zoezi kutimia.

USALAMA WA MFUMO.
Ili mfumo usiweze kuingiliwa na upande wowote, internet yake itaunganishwa na mfumo wa VPN huru itakayokuwa imechaguliwa na kupewa kandarasi na tume ya uchaguzi, na internet hiyo ndiyo itakayotumika nchi nzima pia mfumo utatumia uthibitisho wa njia mbili kwa kila.

FAIDA ZA MFUMO.
  1. Utapunguza gharama za uchaguzi kwa kupunguza idadi ya wasimamizi wa uchaguzi
  2. Utafanya uchaguzi huru na uwazi, hakutakuwa na wizi wa kura.
  3. Utapunguza makosa ya jinai wakati wa uchaguzi.
  4. Utapunguza rushwa
  5. Utaokoa muda wa zoezi la kupiga kura.
  6. Uhuru wa kumchagua mgombea anayehitajika nk
Ahsante!
 
Napendekeza kwa kuwa tuna kampun ya usambazaji internet nvhi nzima kwa kupitia Satelite basi ndo ipewe kandarasi au kama ipo nyigine yenye uwezo huo tender itolewe kwa ushindani
 
Napendekeza kwa kuwa tuna kampun ya usambazaji internet nvhi nzima kwa kupitia Satelite basi ndo ipewe kandarasi au kama ipo nyigine yenye uwezo huo tender itolewe kwa ushindani
Weledi na uwezo nilazima vizingatiwe,lakini pia wazo inategemea wataalam wa system infrastructure watakavyo pendekeze namna bora ya ulinzi
 
Hongera kwa innovation hii lakini kwa uchaguzi wa Tanzania hawawezi kuiruhusu hata siku moja!
 
Hongera kwa innovation hii lakini kwa uchaguzi wa Tanzania hawawezi kuiruhusu hata siku moja!
Kwa nchi za Afrika itachukua muda mrefu sana kuikubali ,lakini kama watu wakutatua matatizo kupitia teknolojia,hatulengi soko ama improvement ya ndani ya nchi tu bali Dunia nzima,mataifa yenye utimamu wake na kiu yamaendeleo watautumiq,yale mbumbumbu yatabaki na umbumbumbu wake.
 
Sidhani kuna mfumo Duniani ambao CCM itashindwa kuu hack. :p
Kaka,hacking inaweza kufanyika kwa kiwango kikubwa kwa accounts,huu mfumo,kampuni itakayo uza soft where ndio itakuwa na uwezo wakufanya chochote,tume ama nchi haitakuwa na uwezo wakufanya chochote,kitu chochote ili kifanyike ni lazima kiwe verified na software owners,,,its a full maped infrastructure.
 
Kaka,hacking inaweza kufanyika kwa kiwango kikubwa kwa accounts,huu mfumo,kampuni itakayo uza soft where ndio itakuwa na uwezo wakufanya chochote,tume ama nchi haitakuwa na uwezo wakufanya chochote,kitu chochote ili kifanyike ni lazima kiwe verified na software owners,,,its a full maped infrastructure.
unafikiri CCM itashidwa kupanga deal na hao software manufacturer? jamaa ni wakongwe Africa kwa wizi wa kura mzee.
 
unafikiri CCM itashidwa kupanga deal na hao software manufacturer? jamaa ni wakongwe Africa kwa wizi wa kura mzee.
Maana yake atakayeshitakiwa si Chama bali developer,na ndio sababu kuu yakufanya developer awe ndio muamuzi
 
Back
Top Bottom