Kalaga baho

JF-Expert Member
Sep 27, 2020
5,465
11,236
Habari ya muda huu wanajf. Naimani tuko vizur mnoo, mvua kila Kona shida kwa wafanyakaz biashara ndogondogo. Msikonde ndugu zangu tupambane, tukomae.. life is no longer space for leasure but only struggle to survive.

Midabwada nimekuwa mchangiaji mkubwa sana kwenye madabalimbali nilizokuwa na uwezo nazo. Siasa, uchawi na utaalam wa afya si sana mana Nina utaalam na ufatiliaji mdogo sana kwenye nyanja hizo.

Ndugu zangu tunafaham ukubwa wa tatizo la UKOSEFU WA ajira na Fursa kwa vijana, na ukubwa wa tatizo la mikataba mibovu na mishahara mibaya kwa walioajiriwa. Matatizo haya mawili yanashabihiana na yote yana ulinganifu karibu sawa kimadhara na ki'chanel'.

Kumekuwa na mada nyingi sana zinazoongelea tatizo la ajira, lawama na baadhi ya shuhuda za interview mbalimbali. Hili sina shaka, sina haja ya kuliongelea Tena, hoja nyingi zitajirudia.

Leo nataka kuongelea mikataba ya watu, baadhi yetu kwenye sekta binafsi. Imagine, unapiga intaview utapita unapewa mkataba wa kazi mshahara 300k masaa y kazi kwa siku ni 9.. jmosi unakuja ofisin kukaa kikao bila posho. Hii ni sawa na kusema unfanya kazi siku 6 kati ya 7.

Pamoja na hayo, bos akikupigia evaluation hufanyi kazi, maneno kibao na vitisho. Mbaya zaidi mashine ikikuharibikia mkononi mwako utakatwa mshahara mpaka kinunuliwe kipya. Hali mbaya, vijana wanahangaika sana. Kuna mfumo wa kazi up ukitumika ofisini wafanyakazi wanataabika mno. Naomba niuite "MFUMO FISI"

MFUMO FISI una sifa zifuatazo:

(a) Bosi anajua kila kitu na hashindwi hoja, Hapo haisikilizwi hoja, anasikilizwa aliyetoa hoja. Hoja hata kama mbaya ila akiitoa bos kila mfanyakazi atalazimika kuona positive kwenye hiyo hoja AUTOMATICALLY

(b) Unafukuza sana wafanyakazi na kuajiri wapya kila mwaka. Ukiona Taasisi kila mwaka inaajiri mtu nafasi hiyohiyo ujiandae na wewe, yako yaja shehe

(c) Lawama kila kikao, na lawama hizo anatupiwa mfanyakaz wa chini sana kwenye organogram. Niliwahi kufanya saidia fundi, fundi akikosea kuweka tofali lawama zinafika mpaka kwangu ninayechanganya udongo , eti nimechanganya udongo laini sana.

(d) Wafanyakaz kumuogopa bos kias kwamba akionekana nje ya ofisi kila mtu anaenda chooni.

(e) ofsi hizi nyingi zinapenda kuajiri wafanyakazi wadogo sana kiumri. Ili watawaliwe vizuri na washindwe kuriakti.

TAKE IT:
1. Ukiajiriwa ofsi kama hii, jiandae jibane ili utoke na mtaji walau wa umachinga mana huna muda mrefu

2. Mamlaka hayana uwezo wa kuingilia kati mana mfumo a ajira ni huru sana. Utakuwepo kwani Bado unatoa Fursa kwa vijana. Sera iandae walau mkakati utakaojumyisha Kuna cha mwisho cha kulipa mshahara ili vijana wapate nguvu ya kujitetea

3. Vijana tujitahidi sana kukontrol emotions. mana n kawaida kabisa mfanyakazi kuomekan hafanyi kazi na kutukanwa. Kama ni presentation, prezenta anawez kuishia kulia.

LIFE BLUNTY UNFAIR.
 
'aggressive, brutal, competitive, cutthroat, every person for themselves, and fierce'.
Tupe uzoef wako mkuu tufanyeje vijana, at least tastics tusogee kinaarifa. Nimezungumza kwa manufaa ya wengi sana hapa.

Huu Uzi uwe muhimu kwa wengine. Let's talk!

Can you share with us, what's going on there?
 
Ndivyo ubepari unavyokuwa kwenye nchi ambazo bado sheria hazifuatwi wala kuheshimiwa.
 
Ndivyo ubepari unavyokuwa kwenye nchi ambazo bado sheria hazifuatwi wala kuheshimiwa.
Oh! Una maana nchi zote zenye maisha ya kibepari Iko hivi?.

Una uzoefu wowote kwa Dunia ya Kwanza au SA?
 
ukutane na bossi kichomi sasa ye anakuoverwork tu hataki jua kama anakunyonya wala nini!
Vijana wanapata tabu sana humu makazini. Kila mwaka anarimyliwa mtu eti hajitumi. Can you imagine mshahara wako unaambiwa utenge % kadhaa kwa ajili ya maendeleo ya ofisi.

Unapigiwa simu wikendi uprint kwa hela yako na upeleke nyaraka kwa hela yako, refund ntolee hiyo
 
Vijana wanapata tabu sana humu makazini. Kila mwaka anarimyliwa mtu eti hajitumi. Can you imagine mshahara wako unaambiwa utenge % kadhaa kwa ajili ya maendeleo ya ofisi.

Unapigiwa simu wikendi uprint kwa hela yako na upeleke nyaraka kwa hela yako, refund ntolee hiyo
Duh! Huo ni unyonyaji kabisa mkuu!
Sema Ndoivo mtu hana pengine pa kukimbilia anaona avumilie tu!
Not fair
 
Duh! Huo ni unyonyaji kabisa mkuu!
Sema Ndoivo mtu hana pengine pa kukimbilia anaona avumilie tu!
Not fair
Mi naonaga nafuuz ya wanaojitafuta mitaani huko. Wa ofisin wanakuaga na hali mbaya mnoo kama mshahara hauna kichwa waa miguu
 
Mi naonaga nafuuz ya wanaojitafuta mitaani huko. Wa ofisin wanakuaga na hali mbaya mnoo kama mshahara hauna kichwa waa miguu
Exactly wa ofisini kama mtu ana position kubwa walau ana fursa za kupiga akina hohehahe usipojiongeza hutafanya kitu kikaonekana

Yeah anaejitafuta kwa malengo anatoboa!
Maisha ni kupambana kiukweli!
 
Back
Top Bottom