Mfaume Kawawa akutana na Kambarage! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfaume Kawawa akutana na Kambarage!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lole Gwakisa, Jan 2, 2010.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hii imetokea siku ya mwisho ya mwaka 2009, sehemu fulani mawinguni huko!
  Kambarage:Ah! ngoja nikapumzike hapo nje kwenye kibaraza changu hapo
  nje, nimechoka kusoma.
  Mhhh! nani yule anakuja, kama namfahamu,si Rashidi yule??
  Waooo!! Simba wa Vita karibu sana huku kwenye utulivu.
  Nilijua utakuja muda si mrefu, maana jana nilidokezwa na
  Mkuu wa Kaya huku, kuwa yule mwadilifu mliyekuwa pamoja ndio yuko njiani anakuja

  Rashidi : Loh, ahsante sana kaka yangu Julius.
  Kumbe safari uliyoipita ilikuwa ngumu kweli kweli, lakini
  nashukuru nimefika ingawaje nimechoka kweli kweli

  Kambarage: Huku ulikokuja ni kwa watu waadilifu, tena nyumba yako
  ilee inayowaka taa, kuna kila kitu unachopenda mle.

  Rashidi : Duh! na Sofia yumo mle?

  Kambarage: Nilimwona juzi akisafisha safisha sebule, alisikia juu ya
  ujio wako!

  Rashidi :Niambie kaka yangu Julius, Sokoine yu wapi?

  Kambarage: Ngoja kwanza, tulia keti hapo. Nipe habari za huko
  nyumbani Tanzania, nasikia kunaitwa bongo siku hizi!
  Nilimwacha Mkapa kwenye usukani

  Rashidi :Julius, Julius nimefika na moyo mzito sana
  Tulichopigania wakati wa uhuru Mkapa ndo kakirudisha kwa
  wanyonyaji leo hii.
  Kijana yule uliyekataa hata kunywa naye chai leo ndiye
  rais.Lakini yeye hana matatizo ila yule kijana mwingine
  Lowassa uliyemkataa kwa kupata utajiri wa kutisha ana
  msumbua sana Kikwete.

  Kambarage:Loh! Loh! Loh! na chama changu je??

  Rashidi : Huko ndo usiseme!
  Nashindwa kukiita kuwa ni chama cha mapinduzi,bora kinge
  badilishwa kuwa chama cha kuwaasi wananchi.Kuna ufisadi
  yaani wizi wa kila aina.Unakumbuka lile jengo la Vijana
  lililojengwa kwa msaada wa waKorea?,kiwanja kimeuzwa sijui
  au kuingia ubia na wanyonyaji. Vile vile ule mradi wa kina mama
  pale Morocco mambo yale yale! Nina hofu na Lumumba.
  Yule kijana wako Kingunge mkomunisti, leo amekuwa mjasiria
  mali mjanja mjanja .

  Kambarage: Basi ! basi ! Basi! Rashidi tulia kidogo na kapumzike!
  Mimi ngoja nikasali kwa siku nzima ya leo.
  Kesho nionane na Mkuu wa Kaya!
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Lole, hii ingesubiri baada ya kupumzishwa, sometime kwenye very serious issue infront of us, craking a joke may look like insult.
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sorry P, that was not intended.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Gwakisa,

  Kama wewe unatoka kwenye kabila la watani wa marehemu, unaruhusiwa kabisa kutoa utani wa aina hii wakati wa mazishi kule kule mazikoni ukiwa unajitolea kusaidia shughuli za mazishi ili unyutralaizi makali ya majonzi , siyo kwenye mtandao kama huu katika thead ambao haina utani na kuna watu bado wana majonzi.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mbona julius hamwelezi rashid aliko sokoine wetu? au naye alihusika *****?
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hawa watani zangu haswa, tena leo nawapakia vilivyo..!!
  Rashidi ilibidi azikwe pale kwa Mfaranyaki, nyumba hii, bombi hii!!
  Sasa inakuwaje anazikwa Madale kwa Wandengereko?
  Sokoine yulee kazikwa Monduli
  Nyerere ndo Butiama.
  Sasa Rashidi vipi tena
  Mgoni/Mmakua bwana taabu sana!
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Jan 2, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tafadhali sahihisha/hariri hiyo sentensi haraka!
   
 8. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  If only the both didnt believe that the other one is in HELL.. as opposed to where they are now. Religion is funny sometimes, in addition to the fact that it makes little sense. Sasa sijui yupi ndio yuko Heaven..lol
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  This is so funny:), kama ingekuwa kuna kukutana huko basi nadhani Nyerere angetamani kurudi ili aje kuisafisha hii nchi.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nyerere wala asirudi.

  Akirudi basi lazima afahamu kuwa:

  "Lowassa na Mkapa watamkamata na wamgeuzie kibao. Watamtandika hadi aliye MAWEE, mwenyewe atajuta kurudi".

  >> Kama ulifikiri hicho ni kitu kibaya basi umeula wa Chuya<<.

  ++ Kibaya ni pale Mtu ataanza kucheka kama kawaida yake++

  ++ Mitanzania (pamoja na mie) tutaendelea kuwasujudia Mkapa/Lowassa na kuwashukuru kwa kazi nzuri huku Makamba akimsaka yeyote anayelaani NYERERE kupigwa na kumwambia kuwa ni KICHAA. Rweyemamu Silva, Chenge, Balile, RA, Karamage, Chiligati nk nk wataonekana wanachekeleaaaaa++

  Mwisho "tutaombwa" tuwaache Mkapa/Lowassa wapumzike kwa kazi kubwa ya KUMCHAPA na kumtia adabu NYERERE.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Bambi!!
  Umeelezwa ukweli
   
 12. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Masikini Nyerere aliitakia mema sana hii nchi. Tatizo ni kuwa aliikabidhi hii nchi kwa mizimu bila ya yeye kujua ile siku a few days we got our independence aliporuka kaburi kule Bagamoyo. Si mnaikumbuka ile hotuba yake ya kuaga aliyoitoa pale Diamond? Baada ya kuruka tu wale masheikh wakasema 'Julius basi tayari mwingereza ameshindwa na nchi tumeichukua (Nani wemeichukua? Ni mizimu)'. Kuanzia hapo Nyerere bila ya kujua nchi akaikabidhi kwa mizimu yaani nchi ililaaniwa. Na Nyerere alipoingia Ikulu ikawa haswa Ikulu inaongozwa na mizimu. Najua haya niyasemayo ni mazito. Lakini Siyo mimi nasema ni maandiko. Na kila mwaka Watanzania tukiongozwa na serikali tunaukimbiza mwenge na kukesha nao kumbe hiyo ni ibada ya sanamu ya mizimu. Kule kuzunguka na mwenge ni kuzidi kukoleza mizimu iendelee kuitawala nchi. Ndiyo maana lolote tufanyalo halizai matunda mema. Kwa nini? Kwa sababu mizimu katika ulimwengu wa roho ni himaya ya giza na penye giza hakuna mema. Wewe niambie inakuwaje viongozi wetu tena wa awamu zote wanajikuta wanafanya maamuzi ambayo yanaangamiza taifa bila ya wao kupenda? Ni laana. Tanzania ina utajiri lukuki kama nchi ingekuwa amekabidhiwa Mungu na sisi tukafanya toba kwa niaba ya Nyerere tungeneemeka.

  Laana tuliyonayo ni kuwa nchi yetu imegeuzwa kuwa kapu lenye mema ambayo wanufaika wake ni wageni ambao watakuwa wanakuja kuchota tu.

  Nini kifanyike. Wachungaji wote na watu wenye mapenzi mema tuiombee toba nchi yetu na tumkabidhi Mungu. Tuaisafishe na damu ya Yesu. Kama serikali haitaki basi kila mtu kwenye nafasi yake afanye hivyo. Wakati nchi inaangamia wewe uliyetubu Mungu atakubariki kivyako.

  Jamani hii ni siri kubwa sana kwa wale mnaoelewa haya masuala ya kiroho tusaidieni kufafanua.
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ndugu Marigwe inae;ekea katika jamii wewe ni a permanent pessimist.
  Hivyo mizimu unayoitaja kunanguvu kubwa sana inayoizidi, na haiwezi kufua dafu kwa sekunde,
  Waisilamu kwa Wakristo wamekuwa wakiombea amani kwa mafanikio, sas hiyo mizimu imeenda usingizi?
   
Loading...