masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,883
- 13,176
Nilipigwa butwaa, kama si kushangaa, mama Samia akiongea na wateule wa mashirika na nafasi mbali mbali za kiuongozi.
Lililonishangaza, eti yule mpendwa wetu Maharage Chande, alipoenguliwa TANESCO na kupelekwa TTCL, "ikagundulika"(mind you baada ya uteuzi) kuwa ana biashara yake inayo gongana kimaslahi na biashara ya TTCL.
Hapo nika pigwa butwaa, mshangao, na kuwa bumbuwazi vyote kwa pamoja, na ni kwa sababu kama mbili tatu hivi.
1 Vetting, kama inavyotakikana basi haijafanyika kabisa, maana kwani Ikulu haikujua kuwa toka mwanzo Maharage Chande ana biashara.
2. Ikulu inakurupuka, hivi hapo Ikulu hawapo watu wenye clear and focused minds?
3. Nchi hii sasa mfanya biashara kuteuliwa kuwa mtendaji serikalini? Hii imekaa vipi?
Haya maswali ni ya kimsingi sana na inabidi tupate majibu yanayostahili, ama sivyo Idara zinazofaya vetting, zinazo simamia uteuzi na hata serikali yenyewe kuwa na foresight ya watendaji wake , huko kuna matatizo.
Sisi wa zamani tulikuwa tukijua kuwa Nchi hii ni ya wafanya kazi na wakulima. Sasa kada ya wafanyabiashara ambao wana interests zao daima, sasa wanakuwa viongozi wa kisiasa au kiutendaji serikalini.
Hapa tanajenga msingi wa matabaka ambayo yatakuwa yakisigana daima. Mama kwa hili sikubaliani na wewe.