Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,335
- 24,232
Maharage Ally Chande amekuwa MD wa TANESCO kwa takriban miaka miwili sasa.
Kama kuna vigezo vya kumpima utendaji, basi kwa sasa vimekuwa juu kwa MD wetu maana utendaji unapimwa na output, umeme kwa wananchi, jamii na biashara kwa ujumla.
Wakati wa miaka ya Magufuli, umeme haukuwa unakatwa ovyo pamoja na miaka ya upungufu wa maji.
Sasa basi ndio tunajiuliza kama bwana Maharage asiye na technical background, anaiweza kazi aliyopewa?
Bodi na management iliyokuwepo kabla ya kina Maharage & co. hawajaingia, mbona ilikuwa ina tenda kazi vizuri tu?
Serikali kwa sasa inavuna matokeo ya kubadili badili viongozi isivyoleta tija katika mashirika strategic kama TANESCO.
Unaondoa proffessionals na kuingiza mediocre characters.
At least one mediocre characters , January Makamba, is out.
Serikali ijitathmini na ifanye kazi na proffessionals husika, katika uongozi wa TANESCO.
UPDATE
Bwana Maharage Ally Chande, rasmi sasa AMEONDOLEWA TANESC na Rais Samia Suluhu na kupelekwa TTCL, mahali pa mawasiliano(ina shabibiana na DSTV).
Asant mama, unapitia maoni ingawaje watu kama Nape wanaidharau.