Mfalme Charles wa Uingereza anasimikwa kitini Mei 5

Mfalme Charles wa Uingereza anasimikwa kitini Mei 5

Huyo mfalme ndo anaenda kuuzika ufalme rasmi maana hakubaliki na nchi nyingi za jumuiya ya madola zinataka kumtoa huyo mfalme kama mkuu wa nchi zao wakiongozwa na Jamaica

Si yeye rumors za kuzika falme zimeanza kitambo. Hizi falme ziko at wrong era kizazi hiki cha sasa hakina time kabisa na hayo mambo
 
Basi utuambie maana halisi ya Jumuiya ya Madola. Na ni nani mwenye madaraka ya Nchi zilizomo ndani ya Jumuiya hiyo? Je, katika Nchi hizo zinaweza kufanya maamuzi: kama kupata Katiba mpya bila ridhaa ya Jumuiya? Nani Mkuu wa Jumuiya?
He is not my King.
Tung'oke tu huko. Kuwepo kwetu ni kwa mkakati wa Kibeberu wa Uingereza. In short it is Just an agreement that UK will bolster our Security[Social-political &Social economic] and Governance from other imperialistic Countries and or Nations! In other words Ati ndio kana chombo cha kutesemea(advocacy group) dhidi ya mataifa mengine yenye nguvu kuliko sie, chini ya mwamvuli wa "Supremacy" ya Mfalme! aidha kwenye Umoja wa Mataifa au Kwingine pale. Yaani ni kujisimika kuwa sie ni "Wanyonge"

Tuwe wakweli na kuangalia ni nini haswa kilichopeleka kuanzishwa kwa Umoja huu na kutizama kwa undani kama kweli Tija zilizoorodheshwa haziwezi kupatikana nje ya Umoja huo - Ukiondoa Ubeberu wa Mwingereza na Rasilimali zetu-kuna sababu gani nyingine ya Sisi kuwemo humo?

Na ujibu, Je, tunaweza pata Katiba mpya bila ya Ridhaa ya Mfalme ambaye ndie Mkuu na mwenye madaraka ya Umoja huo?

Asante
Mbona Kenya wapo jumuiya ya madola na wamepata katiba mpya hata Ghana? Ni utashi wa viongozi wa ccm ndio hawataki katiba mpya
 
Mbona Kenya wapo jumuiya ya madola na wamepata katiba mpya hata Ghana? Ni utashi wa viongozi wa ccm ndio hawataki katiba mpya
Fuatilia vizuri Historia ya Ukoloni wa Mwingereza Kenya na Ghana Utaelewa.

Sisi bado ni 'Wakaidi' kwa lugha nyepesi kabisa. Ingawaje tunabadilika na kuanza kuegemea au kukubali kutawaliwa.....Misimamo na Umoja wa Makabila yetu(Jamhuri ya Muungano) umewawia ugumu Waingereza na wengine Kutuchezea. Na uhakika wakati wanagawa walitegemea(nadhani) sie ndie tungeporomoka, lakini wapi....na huo umetokana na umahiri wa J.K Nyerere

The more divided the easy to manipulate.

Katika mataifa mengi Duniani, Tanzania is A True United States, sidhani kama kuna Nchi nyingine yeyote ile Afrika iliyokuwa na mkusanyiko wa karibia Kabila zote kuu Barani Afrika na tumeshikamana kweli kweli, kitu ambacho ni cha Kusheherekea na Kujidai na kujisifu(Bongo hapa)na ndio unaona kuna wale wanaojaribu kutugawanya :kwa kumchafua Nyerere na wengine wengi waliotaka Umoja wa Mwafrika-kwa nguvu kubwa hapa jamvini- kimakabila na kimajimbo ili iwe rahisi kutawaliwa kifikra na kimawazo na hatimaye....mazimaaaa!

Bwana Sony2, nisikuboe na maneno mengi, fuatilia vizuri hizo Statues, Treaties na Declaration ongeza zako mwenyewe uhitimishe mwenyewe. Binafsi naamini zIpo sababu kubwa zaidi ya Utashi wa CCM, na kati ya sababu hizo ni Ridhaa ya Mfalme... kitu ambacho Serikali hawawezi kusema bila ya kuonekana dhaifu.....fuatilia wa Scottish na hatma yao. Fuatilia, aaargh jina limenitoka, ila moja ya Visiwa vya waingereza huko pacific na Katiba zao.

Amani ikutawale
 
Commonwealth realms ni muunganiko wa nchi 14 zilizopo chini ya Ufalme wa Uingereza. Hizi ni nchi ambazo Mkuu wa Nchi yao (Japo ni ceremonial tu) ni Mfalme, kiongozi wa Serikali ni Waziri Mkuu.

Nchi hizi ni kama Uingereza yenyewe, Canada, Australia, Grenada, n.k. Hawa ndiyo wana haki ya kusema "he is not my king" kwa kuwa kodi zao zinatumiwa na Ufalme.

Commonwealth countries ni Muunganiko wa nchi 56 (ukitoa Uingereza) ambazo nyingi zake zilikuwa chini ya Ukoloni wa Uingereza (Nchi nyingine kama Rwanda, Togo, n.k. hayakuwa makoloni ya Uingereza).

Sasa hapa ndiyo kuna nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, n.k. Lengo la Muungano huu ni kutumia Ushawishi wa Uingereza (na Ufalme wake) kupata fursa mbalimbali kama attention juu ya changamoto wanazozikabiri, misaada, faida za kibiashara, n.k.

Hizi nchi hazipo chini ya Ufalme wa Uingereza, sema zinatumia Ushawishi wa Uingereza kufaidika lakini pia Uingereza inaendeleza ushawishi wake kwenye masuala kama ya Demokrasia, n.k.

Raia wa Commonwealth countries hamna haki ya kusema "he is not your king" kwa kuwa hakuna kodi yoyote anayoitumia kutoka kwenu. Nyie ndiyo mnafaidika naye zaidi.
He is still Not my King in the context, he is the Head of the Commonwealth which I find has nothing in Common with us-original Na ieleweke Ninayo haki zote za kumuita vyovyote vile.

Ushawishi maana yake ni nini hapo juu? Ni kwamba sie tuliomo kwenye Umoja huo hatuna letu! What is Common here? Yeye amebaki kuwa De-Facto ruler wa Colonies Former Colonies and Dominions pamoja na kuwa on the surface inaonekana sio hivyo. Sasa basi na kama unaamini kuwa yeye sio De-facto ruler, tunashida gani Kung'oka huko? at this day and age huoni kwamba hatuhitaji huo ushawishi wake... Collectively(Jumuiya)as-Our Supreme White Leader? popote pale tunapohitaji Ushawishi?
 
Hizo Bendera zinapeperushwa sio kwamba ni za nchi za madola bali nchi zilizomo chini ya himaya ya Ufalme dhalimu wa Muingereza. Ni Ukoloni Mamboleo chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Madola.Yaani zinaonyesha ni wapi walipokuwa na madaraka juu ya Serikali na Watu wake....kwa King-Eleza wanaitwa, kwa sasa na baada ya kusimikwa rasmi, King's Subjects! Yaani sie tu vibaraka wake!

Sioni sababu yeyote ile yenye tija kwa Nchi yetu kubakia katika Jumuiya hii ya Madola. Najua, huyu mfalme ndio kikwazo kikubwa cha sisi Watanzania kupata Katiba Mpya, kwani bila ridhaa yake haya ya Katiba mpya tuyasahau.
Naamini tukijiondoa kutoka katika Jumuiya hii itakuwa rahisi kuendelea na Mchakato wa kupata Katiba yetu iliyo huru.

He is not My King.

Hatuna haja ya kwenda kule tukadhalilishwa tena, hatahivyo bendera yetu kupeperushwa, pia, ni Udhalilishishaji tosha.
Imagine!!!
 
Edinburgh University...

Leo tunakula ubwabwa hapa na shule inaendelea

Vipi huko bongo mnaendeleaje ndugu zangu...
 
Edinburgh University...

Leo tunakula ubwabwa hapa na shule inaendelea

Vipi huko bongo mnaendeleaje ndugu zangu...
Mimi nilikuwa nafatilia coronation ya king Charles CNN Hawa tanesco manyoko wamekata umeme aisee, wamenikera sana
 
Huyo mfalme ndo anaenda kuuzika ufalme rasmi maana hakubaliki na nchi nyingi za jumuiya ya madola zinataka kumtoa huyo mfalme kama mkuu wa nchi zao wakiongozwa na Jamaica
Mkuu umeelewa ulichoandika? Kuna utofauti kati ya Mfalme kama Mkuu wa Nchi zilizo chino yake kama vile England, Wales, Scotland, Northern Ireland, Australia, New Zealand, Canada, Jamaica, kutaja chache na Mfalme kama Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola ambayo Tanzania ni miongoni mwa wanachama. Sasa sijajua, unamaanisha nchi zipi ambazo hazimtaki kama kiongozi wao. Nip tayari kwa mjadala!
 
Hivi ni kwanini USA sio member wa hiyo jumuia ya madola wakati na yeye alitawaliwa na Muingereza?
 
Nacheki live hapa
Jamaa bado wanaenzi utamaduni wao mambo ambayo sisi walituambia ni ya kishenzi
 
Watanzania wengi ni wagonjwa, eti mlevi moja anajitokeza kusema kwamba he is not my king🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Eti mfalme wa Uingereza huko ndo kawazuia watanzania kupata katiba yao mpya 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom