Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,192
- 10,928
Juhudi za kuwafikishia raia wa Palestina misaada kwa haraka zimepata nguvu baada ya washirika wawili muhimu wa Israel kupaza sauti zao kwa pamoja.
Mfalme Abdallah hapo juzi Alkhamis alitua Cairo bila mwaliko akitokea Italia,Uiengereza na Ujerumani kushauriana na viongozi wa nchi hizo kuhusiana na mashambulizi yanayoendelea huko Gaza kutoka jeshi la Israel.
Katika mkutano wao huo wote walikubaliana kutoruhusu wapalestina kufanywa wakimbizi kwa mara nyengine.Badala yake wamesisitiza Israel wafungue mipaka yake na hasa upande wa Misri ili misaada ya chakula na mahitaji mengine iwafikie wapalestina.
Katika nchi ya Misri maandamano yamepigwa marufuku kwa muda mrefu,hata hivyo jana Ijumaa raisi mwenyewe ndiye aliyeyapa kibali.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa naye ameonekana kukemea kwa ukali kitendo cha Israel kukataa kufungua mpaka ili misaada inayosubiri mpakani iweze kuingia Gaza.
Misaada hiyo imeelezwa isipoingia katika kipindi cha masaa 24 yajayo wapalestina wataanza kufa kwa njaa na kiu kwani wamezuilika kujitafutia riziki zao kutokana na kudondoshewa mabomu mfululizo kutoka jeshi la Israel.