Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,191
- 10,925
Joto la vita limeanza kupanda ndani ya Jordan ambayo pamoja na Misri ndizo nchi muhimu kwa usalama wa Israel.
Wananchi wa nchi hiyo hawajaridhishwa na namna nchi yao ambayo ina udugu mkubwa na Palestina kwa namna inavyoshughulikia madhila ya wapalestina na vita vya Gaza. Hata walipomuona mfalme wao akishiriki kudondosha vifurushi vya chakula Gaza haikusaidia kupunguza hamasa zao za kutaka kuingia Jerusalem.
Siku ya leo wananchi hao wamefanya maandamano makubwa wakiimba wanataka mpaka ufunguliwe waende kuwasaidia wenzao wa Palestina wanaokandamizwa na Israel.
Baadhi ya waandamanaji hao walibeba bango linalomuonesha msemaji wa Hamas ambaye hujificha uso aitwaye Abu Ubaida ambaye amepata umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa kiarabu.Msemaji huyo amekuwa akitoa takwimu za kivita kila siku kutoka maeneo yote ya Gaza hata yale yaliyokatiwa mawasilaino ya simu na intaneti.
Sambamba na maandamano hayo ya aina yake kumetokea urushwaji wa risasi kwenye daraja la mfalme Hussein ambalo ndilo lango kuu la kuingia na kutoka kwa wapalestina wanaotoka nje ya eneo lao.Tukio hilo limepelekea kufungw kwa muda kwa daraja hilo