Mfahamu vyema mnyama Tembo (Elephant )

Mfahamu vyema mnyama Tembo (Elephant )

Safi,umechambua vizuri,,,nimependa hapo manii yake ni lita TANO za ujazo, na mkonga wake una misuri elfu moja, ivi simba wana uwezo wakumuua tembo mkuu,,kama wanavyomuua nyati
Simba wakiwa wengi kama kumi na tano na kuendelea wanauwezo wa kumshusha tembo lakini mziki unakuja kwenye kumla maana tembo ana ngozi ngumu ajabu unaambiwa ile ngozi hata mshale unadunda
 
Ana milango mingapi ya ufahamu? Anajilindaje?
Ni kama tu ilivyo kwa binadamu lakini kidogo wao hawasikii vizuri ila ni wataalamu wa kunusa pia macho yao hayaoni vizuri wakati wa kula na badala yake hutumia ule mkonga wao kunusia majani kama yanafaa kula kwanza au la. Kwenye swala la kujilinda dhidi ya maadui wao hutumia zaidi miili yao mikubwa kuwatisha maadui na ndio maana tembo na faru ndio wanyama wanaoongoza kwa kuwa na maadui wachache porini ulilinganisha na wanyama wengine kama swala kwa hivyo miili yao ni silaha tosha dhidi ya maadui. Maadui wakubwa wa tembo na faru ni binadamu ambao huwawinda kwa sababu ya pembe zao pamoja na meno na kwa kiasi kidogo simba ambao wao huua zaidi watoto wao.
 
na uzito huo tembo anakimbiaje kwa kasi kubwa namna hiyo
 
Ni kama tu ilivyo kwa binadamu lakini kidogo.

Kwa kuongezeaa.

Tembo ni miongoni mwa wanyama wanaoweka na kuhuzunika pindi mwenzao anapo fariki.

Pia huweka kumbu kumbu ikitokea siku wamepita pale alipofia mwenzao hutulia kwa muda kumkumbuka.

Pia tembo, hutembea kwa makundi kama familia, wa nyuma hushika mkia wa mbele yake ili wasipoteane.

Ingawa na ukubwa wote huo, tembo akitembea kama ananyata haweki vishindo kabisa, pia kwenye mguu wake kuna kama kakucha hivi kanacho tunza kumbukumbu juuu ya sehemu au njia alizo pita.

Hawa jamaaaa wako very agresive wakisikia kelele, hawapendi makelele kabisaaa ndio maana njia moja wapo itumikayo kumuwinda huyu ni kutumia hasira zake pindi apigiwapo kelele na kuchimbiwa mashimo.
 
Mkuu hebu tufafanulie zile task zake kwa kiswahili fasaha huitwaje?
ni meno ya tembo, pembe za tembo au ndovu na je nisahihi tembo kumuita ndovu?
 
Hapana mkuu tembo wana rangi moja ila wakati mwingine huweza kubadilika rangi kutokana na tabia yao yard kujiwekea maji na matope (wallowing ) ili kupunguza joto katika miili yao wakati wa jua kali kwa sababu wao hawana nywele kama wanyama wengine wao ni hairless mammals na pia hii tabia ya wallowing hufanywa na wanyama wengine pia ambao hawana nywele katika miili yao kama mbogo (Buffalo ), faru (Rhino ) na hata ngiri (Warthog )

Mbona tembo wa Manyara wana utofauti wa rangi na tembo wa Ngorongoro crater?
 
Pia kwa kuongezea njia moja wapo ya tembo kuwasiliana ni kwa kutumia vishindi vya miguu yao ambavyo kwa masikio ya mwanadamu huwa havisikiki kabisa lakini kwa tembo huwa na uwezo wa kuvi sense na wave zake husafiri umbali mrefu zaidi ambapo kuna namna huvitoa kulingana na tukio husika mfano hali ya hatari ama upatikanaji wa maji.

japo njia nyingine huwa wanawasiliana kwa kutumia mikonga yao.
pia tembo ni mnyama ambae yupo makini sana katika kumlinda mtoto ili asije jeruhiwa na maadui na huishi katika koo. mbali na hayo pia tembo huwa na kumbukumbu na ndugu zao wa koo moja ambapo pindi wanapokutana hufahamiana na husalimiana kwa kugonganisha mikonga yao na hukaa pamoja kwa muda na baadae kila mmoja huendelea na mihangaiko yake.
 
Mbona tembo wa Manyara wana utofauti wa rangi na tembo wa Ngorongoro crater?
nadhani hii hutokana na athari za jua.
pindi mnyama anapo pingwa na jua muda mwingi rangi yake hupauka mfano ni nyumbu wa kusini na nyumbu wa kaskazini.
huenda wa manyara akawa na rangi ilo iva kutokana na nature ya hifadhi ilivyo maana ni sehemu kubwa ni forest ambapo humsaidia mnyama kujikinga na jua.
nafikili ndo sababu japo sina uhakika.
 
Sio rangi tu mpaka ukubwa wa mwili. Wa Ngorongoro ni wakubwa zaidi ya Manyara.
 
Sio rangi tu mpaka ukubwa wa mwili. Wa Ngorongoro ni wakubwa zaidi ya Manyara.
Wanaweza wakatofautiana rangi na ukubwa lakini wote ni specie moja. Kama mkuu alivyosema hapo juu, ni tofauti za mazingira ndio zinazosababisha hizo tofauti. Sina uhakika sana na hili, nadhani kuna wale tunawaita Forest Elephants na Savannah/Plains Elephants na ukiangalia hata kwenye haya majina tofauti ni mazingira ambayo wanyama hawa wana ustadi nayo na jinsi mazingira hayo yanavyochangia katika tofauti za either kimaumbile au rangi katika wanyama hao.
 
Sio rangi tu mpaka ukubwa wa mwili. Wa Ngorongoro ni wakubwa zaidi ya Manyara.
nshu ya ukubwa hii hutokana na gene za mnyama husika.
ni kweli tembo wa ngorongoro na ruaha hawa huwa na maumbo makubwa kulinganisha na tembo wa maeneo mengine na huwa nasikia tembo wa mikumi huwa na umbo dogo zaidi kuliko wengine.
hata zamani kulikuwa na simba wakubwa ila walimalizwa kwa kuwindwa na jamii za kimasai kutokana na nshu ya kuwa Moran ni mpaka umuue simba dume.
 
Shukrani mkuu.
 
Mkuu hebu tufafanulie zile task zake kwa kiswahili fasaha huitwaje?
ni meno ya tembo, pembe za tembo au ndovu na je nisahihi tembo kumuita ndovu?
Task zile ni meno ya mbele upande wa juu yaliyobadilika na kuwa katika mfumo wa pembe kwa kiswahili fasaha yale ni meno ya tembo na siyo pembe. Ukimwita tembo au ndovu ni sawa yote ni majina yake
 
Back
Top Bottom