Tunamzungumzia tembo. Huyu ndiye mnyama mkubwa kuliko wote aishiye nchi kavu na anashika namba mbili duniani kwa ukubwa baada ya nyangumi (Blue whale ambaye ana uzito wa tone 190).
Tembo anapatikana katika bara la Africa na barani Asia pekee katika dunia nzima, yupo katika order inayofahamika kama PROBOSCIDEA na familia yake ni ELEPHANTIDAE na uzito wake ni tone 7 kwa dume na tone 5-6 kwa jike pia la tembo hubeba ujauzito wake kwa kipindi cha takribani miezi 22-24 na huyu ndo mnyama anayebeba ujauzito wake kwa mda mrefu kuliko wanyama wote duniani na mtoto wa tembo anapozaliwa anakuwa na uzito wa kilo 120 na urefu wa futi 3.
Tembo hula nyasi na majani ya juu katika matawi ya miti (Browser ) na hula takribani kilo 300 za majani na hunywa maji lita 150-200 kila siku, pia tembo hupumzika masaa nane pekee kwa siku na masaa mengine 16 yaliyobaki huyatumia kutafuta malisho yake.
Hawa pia ni miongoni mwa wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani kutokana na kuwindwa sana na majangili kwa ajili ya meno yao ambayo yana thamani kubwa katika nchi za uarabuni hasa hasa nchini yemeni.
Kwa kawaida tembo huishi katika makundi na kila kundi la tembo huongozwa na tembo jike (matriarch cow or female leader ) wakati madume wao huishi katika kundi la madume pekee (Bachelor herd ) au wakati mwingine mmoja mmoja (Solitary ) na wakati wa ujamianaji madume huwatafuta majike waliopo kwenye heat kwa njia ya harufu pia madume hupigana kweli kweli kwa ajili ya kugombania majike na atakayeibuka mshindi huyo ndiye atakayejamiana na jike aliopo kwenye heat.
Uume wa dume la tembo una takribani kilo 27 na ukifanya kazi vizuri kwa mama wakati wa tendo humwaga maji (manii )lita tano . Tembo huishi duniani(life span ) kwa kipindi cha miaka 60-70 years na hii ni kutokana na kuwa tembo hutegemea sana meno yao yaani iko hivi tembo wana seti sita za meno na kila seti ya meno hulika na Kung'oka wakati wa tembo akila majani, mfano seti ya kwanza ikilika na Kung'oka seti ya pili huchukua nafasi na ya pili nayo ikilika ya tatu huchukua nafasi hivyohivyo hadi seti ya sita ambayo ndiyo seti ya mwisho na hii seti ya sita ikishalika na Kung'oka hapo tembo hatokuwa tena na uwezo wa kula vyakula vigumu kama mizizi, magome ya miti wala majani magumu na badala yake tembo huamia katika maeneo owevu (Marsh area ) na kula nyasi laini ambazo hizi nyasi hazina uwezo virutubisho vya kutosha kwa tembo na baadaye tembo hufa kwa ugonjwa wa utapia mlo (malnutrition ).
Tembo huvuna majani kwa kutumia mkonga wake ambao umeundwa na zaidi ya misuli 1000 pia mkonga wa tembo una kazi nyingi kama kunywa maji, kupumua na kadhalika.
Licha ya kuwa mzito tembo ana uwezo wa kuogelea bila kuzama na ardhini tembo ana uwezo wa kukimbia takribani kilometers 40 kwa saa.
Hapa nchini Tanzania tembo wanapatikana karibia katika hifadhi zote lakini sehemu nzuri zaidi ya kuwaona hawa kwa kaskazini ni TARANGIRE NATIONAL PARK na kusini ni RUAHA NATIONAL PARK.