tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,039
Video ya kusisimua inayosambaa mtandaoni imeonesha Tembo mmoja anamkumbatia mwanamke kwa upole huku akimsikiliza akiimba, akionesha wazi jinsi Wanyama wanavyoweza kuungana kihisia na binadamu.
Soma pia: Tembo hazikwi na meno yake: wanachadema wanaojiunga CCM mnakaribishwa kwa mikono miwili
Video hiyo imewekwa mtandaoni na Lek Chailert, mwanzilishi wa shirika la Save Elephant Foundation na inaonesha akimwimbia tembo aitwaye Faa Mai, ambaye kwa upendo anamzungusha Mkonga wake shingoni mwa Chailert na kumzuia kuondoka.
Kwa mujibu wa Chailert, tembo wake hupenda sana kusikiliza nyimbo na hasa Faa Mai ambaye huonesha kufurahia kwa dhati kiasi kwamba humzuia kabisa kuacha kuimba.
Kupitia maelezo aliyoyaambatanisha na video hiyo, Chailert aliandika “Kila alasiri ni muda wa kupumzika. Mifugo ya tembo hukusanyika chini ya kivuli cha miti, na huwa muda wangu wa kuwa nao kimya kimya, moja ya mambo wayapendayo ni kunisikiliza nikiimba. Haswa Faa Mai, akifurahia muziki huwa haniachii. Daima huniweka pale nisimame nimwimbie hadi mwisho wa wimbo wake anaoupenda.”
Chailert anaeleza kuwa muziki huwapa furaha tembo na pia husaidia kuyatuliza mioyo yao na kuwafanya kuwa wapole zaidi.
Tukio hilo limewagusa wengi, likionesha kwa uzuri uhusiano wa kina unaoweza kujengwa kati ya binadamu na wanyama, na jinsi muziki unavyoweza kuwa na athari chanya kwa hisia na tabia za tembo.
Chanzo: Ayo tv