Mfahamu vyema mnyama Rhino (Faru)

Mfahamu vyema mnyama Rhino (Faru)

Uume wake una ukubwa gani na bao lake moja ni lita ngapi?anarudia tendo kila baada ya muda gani?
Duh....watu wana mswali magumu sana kwa kweli, anyway wacha aje kujibu mtaalamu wetu
 
Ndio mkuu hawa huwa pamoja dume na jike katika msimu wao wa ujamianaji na sio kwa faru tu hata chui vilevile dume na jike hawawezi kuwa pamoja nje ya msimu wao wa ujamianaji
Nina maana faru dume kutembea na mama yake au watoto wa tumbo moja kufanya sex pamoja. Je ni kweli hufanya hivyo?
 
Shukrani mkuu kwa somo zuri,nimependa hapo jike na dume kila mtu kimpango wake hadi siku ya kujamiiana,ingekuwa hivyo hadi kwa binadam tungekuwa hatuchokani,ila hapo kwa wataalam kuua faru ili watengeneze VIAGRA,na kumbe sio dawa,sasa inakuwaje?ina maana hawakufanya utafiti kwanza?maana watazidi kumaliza hawa wanyama adimu,kwa imani ya viagra wakati sio kweli.
 
Nina maana faru dume kutembea na mama yake au watoto wa tumbo moja kufanya sex pamoja. Je ni kweli hufanya hivyo?
Inategemea mkuu maana watoto wa faru hutengana na mama yao baada ya miaka mitatu sasa inaweza ikatokea akaja kukutana na mama yake baada ya kama miaka kumi na wakajamiana maana unajua kuwa wanyama hawana ufahamu wa kutambua kuwa huyu labda alikuwa mama yangu
 
Shukrani mkuu kwa somo zuri,nimependa hapo jike na dume kila mtu kimpango wake hadi siku ya kujamiiana,ingekuwa hivyo hadi kwa binadam tungekuwa hatuchokani,ila hapo kwa wataalam kuua faru ili watengeneze VIAGRA,na kumbe sio dawa,sasa inakuwaje?ina maana hawakufanya utafiti kwanza?maana watazidi kumaliza hawa wanyama adimu,kwa imani ya viagra wakati sio kweli.
Hiyo ni dhana tu mkuu ya wenzetu waarabu kuamini hivyo maana hawa jamaa wana tatizo sugu la ukosefu wa nguvu za kiume kwa hiyo wao wakaamini kuwa kwa faru kuweza kujamiana kwa mda mrefu labda ile pembe huwa inawasaidia kitu ambacho si kweli na hata wanasayansi wameshathibitisha kuwa pembe za rhino hazina product zozozte za kutengeneza nguvu za kiume
 
d8b2b7fe6381d1a97c259bb2c696dc8a.jpg
Faru kwa kiingereza anafahamika kama Rhino na kiswahili ni Faru na sio kifaru kama wengi wanavyomwita. Mnyama huyu anapatikana katika order inayojulikana kama PERISSODACTYLA na familia yake ni RHINOCEROTIDAE na jina lake la kisayansi ni DICEROUS BICORNIS kwa black rhino na White rhino jina lake la kisayansi anajulikana kama CERATOTHERIUM SIMUM.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao ni BIG FIVE kwa Africa, wengine ni chui, simba, mbogo na tembo. Kuna takribani aina tano za faru duniani na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni WHITE RHINO na BLACK RHINO na aina nyingine tatu silizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya faru ambayo ni Black rhino ingawa pia kuna white rhino wanaopatikana mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa.

Faru pia ni wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na kuwindwa sana na majangili kutokana na pembe zao ambazo zina thamani kubwa barani Asia na pembe hizi hutumika kutengenezea dagger pamoja na dawa maarufu ambayo hutumiwa na akina Baba kuleta heshima nyumbani (VIAGRA) ambayo ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume na wanaamini hivyo kutokana na huyu mnyama FARU kutumia mda mwingi wakati wa kujamiana ambapo anaweza kukaa mgongoni kwa jike kwa zaidi ya dakika 40.

Kutokana na kuwa na nguvu za kujamiana kwa mda mrefu watu wakafikiri kuwa nguvu zake zinatoka katika pembe kitu ambacho kimethibitishwa na wanasayansi kwamba si kweli kuwa pembe zake ndizo zimamsaidia kustahimili mda mrefu wakati wa kujamiana. Kwa kawaida faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja (Solitary ) na dume na jike hukutana tu katika msimu wao wa ujamianaji ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume.

Anabeba ujauzito wake kwa kipindi cha miezi 18 na huwa anazaa mtoto mmoja ( Mapacha huwa ni nadra). Faru pia ni miongoni mwa wanyama wakubwa wanaopatikana nchi kavu ambapo anaweza kufikia hadi uzito wa 2000-2300KG kwa white rhino na 800-1500KG kwa black rhino.

Na tofauti kati ya Black rhino na White rhino ni kuwa ana mdomo mweusi uliochongoka ambao unamwezesha kula majani ya juu katika matawi ya mti (Browser) na white rhino yeye anakuwa na mdomo mpana mweupe kwa ndani ambao unamwezesha kula nyasi(Grazers), tofauti nyingine ni kwamba White rhino akiwa na mtoto huwa anatabia ya kumtanguliza mtoto mbele Kama wafanyavyo wamama wa kizungu ambao humbeba mtoto kwa mbele na kwa upande wa Black rhino yeye huwa mtoto anakaa nyuma ya mama kama wafanyavyo wamama wa kiafrica ambao huwabeba watoto wao mgongoni.

Na tofauti nyingine ni kwamba White Rhino ni mkubwa kuliko Black rhino. Na rhino huishi kwa kipindi cha miaka 30-50 na wanapendelea maeneo tambarare na yenye fichaka na kila mmoja huwa anamiliki eneo lake la himaya ambapo hutumia mkojo kuweka mipaka katika maeneo yao yaani hawa tunawaita territorial (Wanyama ambao humiliki maeneo ya himaya). Na kwa hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa FARU ni NGORONGORO CRATER.
Asante sana
 
Na mimi huwa najiuliza sana kwenye big five anawekwa nyati anaachwa kiboko wakati nyati wanaliwa vizuri sana na simba kitu ambacho sio rahisi kwa mbogo
Mkuu kwenye Big five hawaangalii ukubwa wa mnyama no bali hawa kuitwa big five ni kwamba wanyama hawa walipewa hadhi hiyo na wale wawindaji wa zamani kutokana na ugumu waliokuwa wanapata wakati wa kuwinda hawa wanyama na pia hawa wanyama trophy zao zina thamani kubwa kama meno kwa tembo, pembe kwa faru na ngozi kwa simba na chui
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom