Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,655
- 7,521
Jamii ndogo ya faru mweupe wa kaskazini (Northern White Rhino) iko ukingoni mwa kutoweka kabisa duniani, huku ikiwa imesalia na faru wawili tu, ambao wote ni majike.
Faru hao, Najin na Fatu, wanaishi katika hifadhi ya Ol Pejeta nchini Kenya. Faru dume wa mwisho, Sudan, alifariki mwaka 2018, na hivyo kuzifanya jamii hizo mbili zisizoweza kuzaliana kwa njia ya kawaida.
Wanasayansi sasa wanatumia teknolojia ya IVF na utengenezaji wa viinitete kwa kutumia mayai ya faru hao na mbegu zilizohifadhiwa kutoka kwa madume yaliyokufa, katika juhudi za kuokoa jamii hiyo isifutike kabisa duniani.
Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha jambo hili la faru weupe kwa ujumla. Kuna jamii ndogo (Subspecies) za faru weupe wawili, ambao ni Faru weupe wa kusini na Faru weupe wa Kaskazini. Faru weupe wa kusini bado wapo zaidi ya 15,000, na ndio wanaounda karibu idadi yote ya faru weupe waliobaki duniani. Huku faru weupe wa kaskazini wakibaki wawili tu na wote ni majike.
Kwa kifupi: faru mweupe wa kaskazini yuko karibu kutoweka, lakini spishi ya faru mweupe bado haijatoweka.