Mfahamu vyema mnyama Rhino (Faru)

Mfahamu vyema mnyama Rhino (Faru)

Stori nzuri, japo umesahau kuweka chumvi hizi
1. Kifaru ana upeo mdogo sana wa kuona (impaired eye sight), kwa zaidi anategemea kunusa/upepo
2. Faru hapatani na moto, akiona moto atajitahidi kuuzima kadri awezavyo
3. Ni moja ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kabisa duniani
4. kawaida faru ni wanyama wapole, lakini wana hasira kali sana wanapokorofishwa, tena huwa hawakubali kushindwa
Pia Hawana kumbukumbu imara kama Tembo hivyo hawezi kulipiza kisasi
 
mie mdau sana mambo haya ila kwa kuungaunga, weye unaonekana upo deep......nakuunga mkono kwa safari ya weledi
 
Pia Hawana kumbukumbu imara kama Tembo hivyo hawezi kulipiza kisasi
Unajua tembo wao ni waharibifu wakati mwingine wanaweza wakaingia shambani kwa watu na kufanya uharibifu mkubwa kitu ambacho kinawafanya wao wawe na uadui wa mara kwa mara na binadamu tofauti na faru ambao huwa wanawindwa na binadamu kutokana na zile pembe zao pekee
 
Huyo ndo faru na kadri nitakavyopata mda nitawaleteeni aina tofauti tofauti za wanyama na ndege ambao wanapatikana nchini kwetu Tanzania.
Mkuu shukran kwa material unayotupa.Mkuu ningependa kujua ant-predatory strategy za rhino na mating system yao ipoje.
 
White rhino ndo ambaye kidogo ni mpole lakini kwa upande wa Black huyu ndo ambaye ni aggressive
Huwa naipenda sana hii picha ya faru mweupe na mwanae
110440016.jpg
 
Huwa naipenda sana hii picha ya faru mweupe na mwanae
View attachment 390455
Kumuona faru kuna raha yake bwana. Nakumbuka juzi kati kuna mgeni tulikutana naye ngorongoro akatuambia yeye ni mara ya 4 amekuwa akija tu pale ili awaone faru kwa kweli wanavutia ingawa ndo hvyo tena wako wachache mno na hatua za haraka sisipochukuliwa kuwalinda hawa wanyama basi watabakia tu kwenye vitabu
 
Uko Sahii. Mamlaka husika na umma kwa ujumla inabidi kujipanga vyema kulinda uridhi wetu huu wa asili
 
Huwa naipenda sana hii picha ya faru mweupe na mwanae
View attachment 390455
Na faru wote wana rangi ya kijivu (Grey colour ) ingawa wakati mwingine huweza kubadilika kutokana na tabia ya kufanya wallowing ( kujiwekea vumbi na matope ili kupunguza joto katika miili yao kwa sababu hawa ni hairless mammals wanyama ambao hawana nywele ) ndio maana wakati mwingine unaweza kuta rangi zao kama zina utofauti flani.
 
Back
Top Bottom