Mfahamu Stephen Hawking, Mwanasayansi Aliyeitwa Mrithi Sahihi wa Albert Einstein

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
18,147
2,000
Jina lake kamili ni Stephen William Hawking,alizaliwa Oxford uingereza, 8 Januari 1942 na amefariki 14 Machi 2018. Alikuwa mtaalamu wa fizikia na hisabati kutoka Uingereza, mmoja kati ya wataalamu wa fizikia wa kinadharia ulimwenguni.


Jamaa alikuwa haamini kwenye Mungu na enzi anasoma Mwaka 1950 shule ya serikali ya Hertfordshire. Akiwa na umri wa miaka 17, alipitia mtihani wa kujifunza huko Oxford. alichukua masomo ya Chemistry na physics ambayo kwetu madesa hayapandi na kila alichokua anafundishwa kilikua rahisi sana so hata hakusoma wakati wa kujiandaa na mtihani sababu kila alichofundishwa kilikua rahisi sana.
Shuleni alizosoma walimuita #Einstein…nadhani mnamjua huyu jamaa Einstein ndio mwanasayansi ambaye alitabiri mambo ya zaidi ya miaka 100 na yanatokea kweli.

Tafsiri narudia tena TAFSIRI tu ya vitabu vyake ndo viliwezesha Russia kwenda Mwezini.
Ndiye mwenye ile theory ambayo inasema ukienda kwa kasi ya Mwanga unaweza kusimamisha muda.
Ukienda kwa kasi zaidi ya mwanga unaweza kurudisha muda nyuma na ukajiona ukija.

Pole najua hujaelewa hapo..usijali,ni akili kubwa sana.

Ngoja nikulegezee..
Yaani hapa anamaanisha ukimchukua watoto wawili wa miezi 5 alafu mmoja wao ukamuweka kwenye chombo kinachoweza kukimbia kwa kasi zaidi ya mwanga,akienda kwa siku 5 akirudi duniani atakuwa na ileile miezi 5 na siku 5 lakini yule aliyemuacha duniani atakuwa na miaka 85.Umeelewa??

Pole ila najua kwambali kasomo kamekuingia nitakaelezea siku nyingine kama unataka katafute kitu kinaitwa ‘TIME TRAVELLER’ Utawasoma zaidi hawa watu.


Sasa huyo Einstein wa maajabu yote hayo ndo jamaa alikuwa anafananishwa naye.
Aliandika vitabu mashuhuri kuhusu sayansi vinavyolenga watu ambao si wanasayansi.
Ukivisoma lazima uwe na imani sana otherways unaweza kuanza kutoamini dini yako


PITA HAPA PIA: PAKUA FILAMU THEORY OF EVERYTHING FILAMU INAYOHUSU MAISHA YA STEPHEN HAWKING

Hawking alikuwa profesa wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Cambridge nafasi ambayo [HASHTAG]#IsaacNewton[/HASHTAG] aliwahi kuwa nayo.
Alistaafu tarehe 1 Oktoba 2009.
Newton nadhani tunamfahamu tulimsoma sekondari zile Law zake.

Dingi na mama yake walikuwa na akili sana pia,walikutana wakati wa kukaribia vita vya pili vya dunia.
wakati anasoma ndipo ugonjwa wake ulianza kujionyesha.
Alikuwa na shida katika kujinyoosha na kisha hata tu kutembea.
Hata hivyo, alimaliza PhD yake akaandika kuhusu mashimo meusi katika shahada yake.
Mashimo meusi(Blackholes) ni mashimo flani wanayasema wataalamu kuwa yapo angani.
Kwamba Mwanga unamezwa,yaani ni sehemu pekee giza linaushinda mwanga.tatizo hakuna picha iliyowahi kupigwa sababu ni nadharia ya kufikirika.

Alikuwa na ugonjwa wa chembe za neva unaohusiana na ulemavu wa akili unaosababisha mtu kuwa na shida ya kusoma na kuandika (Dyslexia kwa Kiingereza), na kwa sababu hiyo hawezi kutembea au kuzungumza vizuri. Ugonjwa huo ulizidi hata kuwa karibu kabisa na kupooza. Alitumia gurudumu kusonga, na kompyuta ya Intel ili kuzungumza.

Bado hatujajua Mungu ameamua kuonyesha ukuu wake au ni hali ya kawaida tu. Lakini jamaa ndo hivyo bana.

Huyo ndo Mtu Mzima Stephen Hawking, kwa uchache kwa zaidi unaweza kusoma kupitia Mitandao mbalimbali
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
12,093
2,000
Alikuwa Vizuri But Is Not Fair Kumfananisha Sir Issack Newtom Na Einstee coz Hao Watu Ni Hatarim nSi kweli..Newton alikua average!

Einstein alikua popularized na American jewish media machinery...dont get me wrong,he was good,ila media ya Kimarekani ilimpromoti mno...Niels Bor mwenyewe anamkimbiza..Kuna Mjerumani kama Goethe,way ahead of human times!Sema hawakua promoted na media!

Einstein alikua celebrity scientist,ni kama Kim Kardashian of science!
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
12,093
2,000
Kama Newton ni average nitajie mwana physics yoyote alie juu ya Newton kwenye Classical mechanics..
Newton ndio father of classical mechanics

Mkuu

Newton kagundua vitu very basic ila muhimu...Newton hakua prodigy,hakua genius....alikua average ila alikua na juhudi kubwa sana ya kupiga msuli...Hiyo inajulikana!

Mkuu,magenius ni wale walikua wanafunga macho wanaona picha nzima ya dunia na mathematical equations na kila kitu ndio wanaandika na wakija ku-pruvu ni kweli..The likes of Tesla,Einstein na wale Wahindi,na Wajerumani..

Mzee,acha kabisaaa!
 

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,536
2,000
Mkuu

Newton kagundua vitu very basic ila muhimu...Newton hakua prodigy,hakua genius....alikua average ila alikua na juhudi kubwa sana ya kupiga msuli...Hiyo inajulikana!

Mkuu,magenius ni wale walikua wanafunga macho wanaona picha nzima ya dunia na mathematical equations na kila kitu ndio wanaandika na wakija ku-pruvu ni kweli..The likes of Tesla,Einstein na wale Wahindi,na Wajerumani..

Mzee,acha kabisaaa!
Mkuu nimekuuliza kwenye classical mechanics ni mwanaphysics gani yupo juu ya Newton ili Newton awe average
Kama kupiga msuli hakuna anaemzidi Tesla hapo mpaka baba yake akatumiwa barua za kuombwa amtoe mwanae shule otherwise atakufa
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
12,093
2,000
Mkuu nimekuuliza kwenye classical mechanics ni mwanaphysics gani yupo juu ya Newton ili Newton awe average
Kama kupiga msuli hakuna anaemzidi Tesla hapo mpaka baba yake akatumiwa barua za kuombwa amtoe mwanae shule otherwise atakufa

Mkuu
Classical physics ndio basic physics maana yake,kwa kifupi sio ngumu..
Mkali wa classical physics sio mkali kiakili kiivyo...
Basic physics haingii kwenye quantam hata kidogo...
Wababe wa quantam ni vichwa zaidi ya Newton mara kadhaa....Usibishe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom