Mfahamu mrithi wa Marehemu Maalim Seif, Mh. Othuman Masoud Othuman

Abdul Nondo

Verified Member
Oct 28, 2016
318
1,000
Anaitwa Othuman Masoud Othuman Sharif Mzanzibari na mtu mashuhuri katika masuala ya sheria. Mh.Othumani alizaliwa kijiji cha Pandani huko Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, tar 7 Februari 1963.Alizaliwa mwaka ambao Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa kisultan mwaka 1963 ,utawala ushirika wa ZNP na ZPPP.Yaani alizaliwa mwaka mmoja kabla ya mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari /1964.

Baba yake mzazi Othumani Masoud anaitwa Sheikh Masoud Bin Othman alikuwa mwalimu wa dini katika madrasa, huko Pandani alikuwa anafundisha elimu ya dini (Quran).

Mh. Othumani Masoud alisoma elimu ya msingi Pandani, akiwa na akili nyingi darasani wanasema kipanga katika miaka yote aliyosoma.

Alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Fidel Castro, huko Chake Chake, Kusini Pemba pia shule ya Sekondari Ben Bella mwaka 1978-1981 .

Mwaka 1982-1986 alijiunga na chuo cha kiswahili na lugha za kigeni akianza soma ngazi ya cheti/astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) katika lugha ya Kiingereza, historia, elimu katika saikolojia.

Mh. Othumani Masoud baadaye mwaka 1986-1989 alidahiliwa kusoma chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B).

Mh.Othuman Masoud aliendelea kuwa kipanga katika Kitivo cha Sheria akiwa na uwezo mzuri darasani na kujenga hoja .Alihitimu chuo kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) mwaka 1989 na shahada ya heshma(LL.B Hons), akarejea Zanzibar sana na kupata kuajiriwa kama wakili wa serikali yaani "State Attorney, na Attorney General's Chambers kuanzia 1989-1993.

Mh.Othuman akiwa ameajiriwa tayari serikalini kama wakili wa serikalini baada ya kuhitimu masomo yake ,mwaka 1991 alijiendeleza kielimu kwa kusoma shahada ya pili au shahada ya uzamili ya Sheria (Masters) au (LL.M) katika chuo cha uingereza (University of London UK) akibobea katika Sheria ya biashara na makampuni akiangazia haswa sheria ya kikodi, Sheria ya biashara za kimataifa,sheria ya makampuni na usuluhishi wa masuala ya kibiashara.Pia mwaka 2006-2007 alisomea tena shahada ya tatu chuo cha Turin, Italy (Masters).

Alipomaliza kusoma Masters, mwaka 1993, akateuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sheria pia naibu mwanasheria mkuu.

Katika kipindi cha uongozi wa awamu ya tano chini ya Dk Salmun Amour kuanzia 1996 hadi 2000 alipata pia kuteuliwa kuwa Katibu mkuu wizara ya Sheria na katiba na kuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali yaani Deputy Attorney General.

Katika utawala wa Aman Abeid Karume mwaka 2000 kuanzia mwezi Novemba hadi Julai 2002 Mh.Othuman aliteuliwa kuwa katibu mkuu Wizara ya utawala Bora, Sheria na katiba ,pia naibu mwanasheria mkuu wa serikali (Deputy Attorney General).

Julai 2002 hadi Machi 2011.Mh.Othuman akaendelea kuaminika serikalini hivyo kuteuliwa na Rais Karume kuwa mkurugenzi wa kwanza wa Mashtaka Zanzibar(DPP). Kwanini tunasema mkurugenzi wa kwanza? Ipo hivi.

Kabla ya mwaka 2000 wa utawala wa Aman Abeid Karume, Zanzibar hakukuwa na Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP),kupatikana kwa Ofisi ya DPP Zanzibar ilikuwa ni moja ya jitihada kubwa za Marhemu Maalim Seif Sharif Hamad,baada ya uchaguzi wa 2000 ,katika hatua ya maridhiano na muafaka wa pili, moja kati ya terms katika muafaka wa pili ilikuwa kuanzisha Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP) Zanzibar na sio kuburuzwa buruzwa na Tanganyika ikiwa Zanzibar kuna mahakama kuu hivyo marekebisho ya 8 na 9 ya katiba ya Zanzibar yakafanyika na kuanzisha Ofisi ya mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hivyo DPP wa kwanza Zanzibar akawa Mh.Othuman Masoud alitumikia nafasi iliyotokana na jitihada za Marhemu Maalim Seif ,Mungu alianza muunganisha Mh.Othuman na Marhemu Maalim Seif mapema.

Novemba 2010 Dk. Ali Mohamed Shein alichaguliwa kuwa Rais wa 7 wa Zanzibar .Moja ya teuzi katika kuunda serikali yake Aprili 2011 alimteua Mh.Othuman Masoud kuwa Mwanasheria mkuu (Attorney General) wa serikali ya Zanzibar ,na Mjumbe wa baraza la mapinduzi pia Mjumbe wa baraza la uwakilishi .Nafasi alizoshika hadi alipotimuliwa na Rais Shein kwa kudhalilishwa,kejeliwa na matusi juu mnamo Oktoba 2014.

Kuna watu baadhi wanauliza Mh.Othuman Masoud anawezaje kuteuliwa kuvaa viatu vya Maalim Seif ,ikiwa hajatumia muda mwingi katika siasa za upinzani?

Watu wanaohoji hayo,wanasema Mh.Othuman alijiunga na upinzani CUF mwaka 2014 baada ya kufukuzwa katika serikali ya Zanzibar na Rais Dr.Shein .Hivyo hadi sasa 2021 ana miaka 7 ndani ya upinzani yaani kuanzia CUF na sasa ACT wazalendo ,ni wazi watu wanaohoji haya hawamjui Mh.Othuman na pia hawajui vyema siasa za Zanzibar na kipi wanachopigania wazanzibari.

Kinachopiganiwa Zanzibar ni mamlaka kamili ya Zanzibar,ni heshima ya Zanzibar, Muungano wenye usawa,manufaa,haki na wa kuheshimiana.Hivyo mtu yeyote ndani ya Zanzibar anayejitoa kupigania maslahi ya Zanzibar bila kujali maslahi yake binafsi huyo sio wa kubeza bali ni shujaa na mpambanaji bila kujali yupo ndani ya chama pinzani kwa muda gani,au yupo chama gani ,kabila gani,au dini gani au hana chama.

Ujasiri wa kupigania maslahi ya Zanzibar na muungano wa haki ,wenye usawa ,manufaa na kuheshimiana ni mambo ambayo wanachama au viongozi wengi wa CCM hawawezi kuyasemea na yeyote anayejitokeza kuyasemea huonekana msaliti,hutukanwa,kubezwa na hata kufukuzwa ndani ya CCM.

Mifano halisi,ni hawa chini bila kujali maslahi yao binafsi walisimama imara ,kuwa na misimamo imara ya kutetea maslahi ya Zanzibar na muungano wenye usawa na manufaa kwa wazanzibari.

Mh.Mansour Yusuf Himid aliyekuwa waziri wa SMZ,muweka hazina wa CCM Zanzibar,muwakilishi Kiembesamaki,mjumbe wa kamati ya maridhiano ya Zanzibar na mtoto wa Brigedia Jenerali Yusuph Himid mkuu wa kwanza wa vikosi vya SMZ ni muhanga wa hili akiwa CCM Agosti 2013, alifukuzwa sababu ya misimamo yake ya kutetea maslahi ya Zanzibar na muungano wenye usawa na manufaa.Baadaye kuzushiwa mambo mengi ya kizushi na kesi za kutengeneza pamoja na kumuweka Lock up ila hakutetereka mwishowe hatimaye akahamia CUF baadaye Act wazalendo na kuwa mshauri Maalum wa Marhemu Maalim Seif hadi mauti ulipomkuta marhem Maalim Seif , Mansour Himid hajawahi kutetereka katika misimamo yake ya kutetea na kudai muungano wenye usawa na manufaa kwa wazanzibari.

Mwingine ni Marhemu Mh.Hassan Nassoro Moyo,muasisi wa CCM, Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano ya Zanzibar.Naye ni muhanga akiwa CCM April ,19,2015 alifukuzwa CCM sababu ya misimamo yake ya kutetea maslahi ya Zanzibar na muungano wenye manufaa, mwingine ni mzee wa ku-delete Mh.Mohamed Ahmed Sultan maarufu Eddy Riyami , Mjumbe kamati ya maridhiano ya Zanzibar aliondoka CCM kwa kuonwa msaliti sababu ya kusemea maslahi ya Zanzibar na kutetea muungano wenye manufaa wakamuona adui wakamsumbua,wakampa kesi za kizushi na kumuweka Lock up ,pia Mh.Othuman Masoud alifukuzwa nafasi ya Mwanasheria mkuu sababu ya misimamo yake ya kutetea Zanzibar na muungano wenye manufaa.Wote hawa ni wanga kutokana na misimamo yao kwa maslahi ya Zanzibar.


Mh.Othuman Masoud akiwa mwanasheria wa Zanzibar wakati wa mchakato wa mabadiliko ya katiba,kutokana na misimamo yake kwenye utetezi wa mambo yahusuyo Zanzibar, uumini wa Serikali tatu na kupunguzwa mambo ya muungano alionekana msaliti ndani ya chama cha mapinduzi na serikali ya Zanzibar Katika sekeseke hilo la mabadiliko ya katiba na misimamo yake, Mh.Othuman alitimuliwa kwa aibu katika Bunge la Katiba chini ya ulinzi wa vyombo ya usalama na kisha kurejeshwa Zanzibar ambako alivuliwa nafasi yake kama Mwanasheria Mkuu wa SMZ mwaka 2014.

Baada ya changamoto hizo Mh.Othuman Masoud aliamua kuingia kwenye siasa na kujiunga na CUF na baadaye Act wazalendo.Akiamini ni njia sahihi na mpya ya kuendelea kusimamia yale anayoyaamini.

Tangu akiwa nje ya Serikali ya Zanzibar na ndani ya siasa za upinzani,popote anapokwenda ndani na nje ya Zanzibar anasimamia mawazo yake na misimamo yake kuhusu haki za Zanzibar ,maslahi ya Zanzibar na muungano wenye manufaa,haki na usawa. Kwa misimamo yake alizushiwa mengi na mabaya ,ya kumchafua na kumdhalilisha ila hakutikisika hadi sasa,yupo imara.

Mh.Othuman Masoud anamiliki kampuni yake binafsi ya masuala ya sheria iliyopo Zanzibar, wateja wake wengi ni watu binafsi na makampuni binafsi, pia hutoa huduma kama mshauri mwelekezi katika mashirika mbali mbali ya kimataifa nje ya nchi.

Marhemu Maalim Seif alikuwa ana andaa na kukuza watu ambao baadaye wangeweza kumrithi yeye,hivyo mbali na Mh.Othuman Masoud bado kuna kapu la watu na viongozi mashuhuri katika siasa za Zanzibar ambao wataweza kuendeleza mawazo na kurudumu la kupigania maslahi ya Zanzibar kwa pamoja sasa hata baadaye ,nina muona Mzee Duni Haji, Mansour Yusuf Himid,Ismail Jussa,Nassoro Mazrui ,Omari Said Shabaan,Hamad Yusuf, na wengine wengi ambao sijawataja.

Mungu amjalie Mh.Othuman Masoud kutekeleza vyema majukumu yake.Mungu amlaze mahali pema mwenyekiti wetu Marhemu Maalim Seif Sharif Hamad.


Abdul Omary Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa Act wazalendo.
IMG_20210302_073720_926.jpg
IMG_20210302_071155_092.jpg
IMG-20210301-WA0316.jpg
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,407
2,000
Ana CV nzuri na ni mtu wa kutetea haki, tatizo langu lipo kwenye cheo chenyewe ambacho hawezi hata kumteua mtendaji wa mtaa wala kukaimu office ya Rais wa Zanzibar.
 

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
254
500
Ni moja ya watu watakaosababisha muungano uvunjwe na baadaye ataishi kwenye historia akilaumiwa na yeye akijilaumu. kwasababu sasa hivi tunapowashikilia kama watoto wanaona wabara hatuna faida, ila tukiachana watatutafuta kwa tochi.
 

Mchokozi wa mambo

Senior Member
Mar 27, 2014
157
225
Abdul Nondo acha ngojera zako humu maana hata wewe tunakujua ni bonge la msanii na uliweza kujiteka mwenyewe kipindi kile ukasema serikali imekuteka. Mtu mwenyewe anaapishwa na Rais wa Zanzibar sasa nguvu yake itakuwa wapi hapo?
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,288
2,000
ni moja ya watu watakaosababisha muungano uvunjwe na baadaye ataishi kwenye historia akilaumiwa na yeye akijilaumu. kwasababu sasaivi tunapowashikilia kama watoto wanaona wabara hatuna faida, ila tukiachana watatutafutak wa tochi.
Kwa mfano sisi Watanganyika tunawasaidia kipi Wazanzibar?

Kujijaza ujinga tu kichwani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom