exit
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 1,670
- 1,808
Hapo sasa unatafuta ugomvi ...Tandu aling’ata sehemu gani?
Hapo sasa unatafuta ugomvi ...Tandu aling’ata sehemu gani?
Just Hahaha!!... Kumbe kutung'ata kote huko huwa wana Kiu tuu?
Safi sanaDawa ya kunguni..ni maji ya moto..narudia tena maji ya moto..mwagia kwenye kona zote za fenicha na vitanda..kila baada ya wiki mbili..hakika utasahau..
Sent using Jamii Forums mobile app
Ya kweli hayo maana kwenye sofa langu wapo wengi nahangaika naoNakumbuka nilikujaga hapa kuomba ushauri juu ya hawa wadudu wahuni kabisa kupata kitokeo kwa usumbbufu
Baada ya kuhangaika na dawa mbali mbali bila mkakati walikua wanaonekana tena baada ya wiki kadhaa
Kuwamaliza nilifanya hivi
Nilianika godoro wiki nzima juani kisha nikanyunyizia maji ya sabuni
Nikamwagia mchanganyiko wa maji na sabuni ya unga na mafuta ya taa na chunvi kisha nikamwagia nyumba nzima kwa kutumia solo, lile bomba la kunynyizia dawa
Nililoweka nguo zangu zoooote ikiwemo mashuka, mapazia, net kwenye sabuni ya unga siku 2
Nikakaa wiki 2 nikarudia zoezi la kunyunyizia mchanganyiko wangu kwa kupiga nyumba nzima tena
Baada ya hapo sijawaona tenaaaa
Hapo kwenye kitambaa cha plastic nimecheka sanaMi sofa zangu ni za kitambaa cha plastic mtaani tunaita leather
Nilipulizia mchanganyiko wangu mara 2, nilirudia baada ya wiki. sofa zililoana haswa haswa
Yaani jiongeze hadii uone hapa kweli dawa imefika kila kona ya sofa
Ni vizuri ukapiga dawa kisha ukarudia tena maana inaonekana mayai ni magumu kufa kwa dawa
So puliza kisha kaa wiki vitoto vikianguliwa piga tena
UbarikiweKosa moja kubwa sana ambalo wengi wetu tunalifanya ni kutumia nguvu nyingi sana kumuangamiza kunguni mwenyewe, mimi naamini bado tunakuwa hatujaondoa tatizo.
Kwa kuwa kunguni kama kunguni ni rahisi sana kumuua, mfano chukua sabuni ya unga changanya na maji ukimwagia kunguni anakufa au maji ya moto au juani anakufa mara moja.
Lakini mpaka hapo bado tutakuwa hatujaondoa tatizo kwa kuwa wengi wetu tunasahau mayai yake! hili ndio janga halisi.
Huwezi kuangamiza mayai yake juani au kwa maji ya moto ni lazima yatabaki, kwa hiyo utakapo anika juani au kutia maji moto ni sawa na kuyaweka kwenye INCUBATOR na baada ya siku tatu au nne vitaibuka vitoto kibaaao na hivi vikija utakoma, maana vinakuwa ni vikali sana.
USHAURI:
Usianike au kutumia maji moto kuwamwagia kwa maana utawauwa kunguni na wakati huohuo unazalisha wengine, cha kufanya tafuta sumu ya kuwauwa na uipulizie humohumo mdani bila kuhamisha chochote, kwa maana kitendo cha kuhamisha hamisha vifaa ni kuawasambaza, piga dawa chumbani pqmoja na godoro na kitanda usisahau madirishani na milangoni na kutani na kwenye matundu na nyufa zote.
Hili tendo lirudiwe zaidi ya mara mbili ili kuhakikisha mayai yote na kunguni wameangamia.
Nimepata ufahamu huo baada ya kunisumbua sana, nilianika juani haikufaa, nlitia maji moto haikufaa, nilitia mafuta taa hola niliwachoma na hair dryer haikufaa nilitumia mchanganyiko wa sabuni na jik kunguni wenyewe wanakufa fasta lakini mayai ni tatizooo mpaka upate sumu ya uhakika.
Sent using Jamii Forums mobile app
diazon...........hii ni kiboko ila sina hakika kama ck hizi zipo madukani.
Kwahiyo uhame nyumba uliyojenga?Hakuna dawa kwa kizazi cha sasa cha Kunguni.... Dawa ya kudumu na itakayokufaa mkuu ni KUHAMA mtaa huo unaoishi....!
Kama mm,Hapo kwenye kitambaa cha plastic nimecheka sana